Umri Mkubwa, Hotuba Za Chuki Uhuru wa Habari: Ajenda Kuu Katika Uchaguzi wa Rais Nigeria 2019

Upigaji kura ukiendelea wakati wa uchaguzi wa Rais Machi 28, 2015 huko Abuja Nigeria. Picha na Ubalozi wa Marekani/Idika Onyukwu. Nakshi za picha: Sio ya Kibiashara 2.0 Generic (CC BY-NC 2.0)

Nigeria itafanya uchaguzi wa Raisi hapo Februari 16, 2019 na macho yote yapo katika uchaguzi huu kuthibitisha nguvu ya mila, desturi na umoja katika demokrasia ya Nigeria.

Mwaka huu kuna  wagombea wakuu watano kati ya wagombea wote 73wa kinyang'anyiro hiki cha Uraisi.. Wagombea wakuu wawili akiwepo Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari (Chama cha Maendeleo kwa Wote) na mgombea kutoka chama cha Upinzani; Makamu wa Raisi wa zamani Atiku Abubakar (Chama cha Demokrasia kwa Watu).

Wagombea wengine watatu ni Obiageli Ezekwesili, Kingsley Moghalu na Omoyole Sowore, ambao wameitwa “Nguvu ya tatu” kwa sababu wanakosa uzoefu katika siasa lakini wanawakilisha upinzani muhimu.

Huku kukiwa na manung'uniko kuhusu kampeni za uchaguzi na mahudhurio ya wanaounga mkono wagombea mitandaoni na nje ya mitandao haya ni mambo ya msingi ambayo yanaweza kupotelea ndani ya manung'uniko hayo.

Kiwewe cha Mzee na Mwenye nguvu

Wagombea wakuu wa urais wa urais wa Nigeria Buhari, 76 na Atiku, 72, wote wana historia ndefu katika kujihusisha na siasa za Nigeria wakiacha maswali mengi kuhusu afya zao na urefu wa muda wao kama watarajiwa wa Urais.

Ukiwa mwisho wa watawala wa muda mrefu kama vile Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, 76 na wa Zimbabwe Robert Mugabe 94 ambaye alilazimishwa kutoka madarakani baada ya miaka 37 kama rais, imekuwa kama vile ndio mwisho wa utawala unaoongozwa na wazee  Afrika. Lakini tumaini hilo halikudumu sana baada ya Paul Biya, 84, kuchaguliwa tena kama Rais wa Cameroon na kuwa kiongozi wa kisiasa mwenye umri mkubwa zaidi Afrika katika ukanda wa Sahara Afrika.

Afya ya viongozi wa Nigeria imekuwa kigezo kikuu cha kisiasa baada ya Rais Umaru Musa Yar’Adua kufariki akiwa ofisini Mei 5, 2010. Ugonjwa wa Yar’Adua na kuendelea kutokuonekana kulitengeneza Ombwe la uongozi kwa sababu hakumkabidhi ofisi makamu wake, Goodluck Jonathan, kabla hajasafiri kwenda ughaibuni kwa matibabu.

Raisi anayemaliza muda wake Rais Buhari ameshafanya zaidi ya safari kumi kwenda Uingereza kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa ambao haujawekwa wazi. Ameshatumia “zaidi ya siku 170 akiwa London kwa likizo rasmi ya ugonjwa tangu awe Rais mwaka 2015,” kulingana na New York Times.

Je mgombea kijana anaweza kupata nafasi? Mwaka huu kuna wagombea 10 ambao wana umri chini ya miaka 40 na wagombea 16 wenye miaka kati ya 45-49. Lakini wagombea vijana wanaweza wasivuke salama kwa sababu ya historia ndefu ya uongozi iliyotengeneza utamaduni kushikamana na wanasiasa wenye utajiri wa kufadhili siasa za chama na hili huchukua muda na huitaji mtandao kulifanikisha.
Buhari na Abubakar wote wana msingi imara wa kisiasa. Buhari anao wafuasi waaminifu kutoka upande wa kaskazini mwa nchi wakati inaaminika kuwa Abubakar anakubalika kwa upana zaidi katika makabila na dini mbali mbali pote nchini. Miaka yao haionekani kuwa kikwazo katika kuungwa mkono.

Ukabila na Udini

Nigeria inajulikana kama nchi iliyo mstari wa mbele katika ukabila ambapo ukabila na udini umechukua nafasi kubwa sana katika chaguzi na siasa kwa ujumla. Uchaguzi wa 2015 ulionesha kuwa wagombea “wakuu wawili walipata kura nyingi kutoka katika majimbo mbalimbali na maeneo yao ya kisiasa,” na hii ni kulingana na makala kutoka  Jarida la Chaguzi za Afrika. Pia, hisia za kikabilazilitumika kuwarubunj wapiga kura. Hotuba zenye chuki za kikabila ziliongezeka mitaani na mitandaoni, kabla nabaada ya uchaguzi wa Rais wa 2015.

Vilevile mwaka 2017, baadhi ya waandishi some Wa Nigeria walipiga kelele kuhusu hotuba yenye chuki ya kikabila ambayo kidogo ilimeze taifa. Rais wa zamani Goodluck Jonathan alipoteza kura kwa sababu alishindwa kudhibiti kikundi cha wanamgambo wa Kiislamu cha Boko Haram  mabomu yaliyorindima nchini na kusababisha kuenea kwa hofu ya haki ya usalama.  Boko Haram kuteka wasichana wa shule huko Chibok kulileta kilio Cha #WarudisheniMabintiZetu kote ulimwenguni baada ya raia kugundua kuwa serikali haifanyi juhudi zozote za kuingilia kati.

Buhari na Abubakar wote watategemea miungano ya kidini au kikabila kushinda uchaguzi. Buhari kutoka kaskazini kwa (waFulani/Waislam), amemshikilia Yemi Osibanjo kama makamu wake kati ugombea wa uraisi ili kuvuna kura kutoka kwa watu wa kusini ambapo ni sehemu ya nchi ya (Wayoruba/Wakristo). Abubakar, ni kutoka kaskazini (Fulani/Muislam) amemchagua mgombea mwenza wa urais kutoka kusini mwa nchi ambapo ni sehemu ya (Waigbo/Wakristo)

Kwa sababu Buhari na Abubakar Wanatokea katika kikundi kimoja cha kidini msukumo unaweza usiwe mkubwa kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo ilikuwa kati ya Jonathan Goodluck kutoka kusini kwenye kabila dogo la Ijaw na Mkristo dhidi ya Buhari.

Uhuru wa Habari na Kujieleza

Utawala wa Buhari umekuwa ukituhumiwa kwa uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu na hashtagi nyingi zilivuma katika mitandao ya kijamii mwaka 2018 zikitaka kufunguliwa kwa raia wa mitandaoni na wanahabari.

Hapo Machi 17, 2016, Mwandishi wa habari wa Nigeria Yomi Olomofe alishambuliwa kikatili na kuwekwa kizuizini na polisi wa Nigeria wakizuia uhuru wa kujieleza. Mwanahabari wa Nigeria Daniel Elombah na kaka yake Timothy Elombah, waliwekwa kizuizuni siku ya mwaka mpya 2017 kwa sababu ya habari ambayo hata hawakuiandika. Agosti mwaka ule, mfanyabishara wa Nigeria Joe Fortemose Chinakwe alikamatwa kwa kumpa mbwa wake wa kufugwa jina la “Buhari”.

Jones Abiri, mchapishaji wa Chazo cha Wiki alikamatwa Julai 21, 2016 na maajenti wa usalama wa Taifa (DSS) akiwa ofisini kwake huko Yenagoa, Jimbo la Bayelsa. #MfungueniJonesAbiri ilivuma kwa siku kadhaa huko Twita mpaka Abiri alipoachiliwa Agosti 15, 2018, baada ya kukaa kizuizini kwa miaka miwili.

#MwachieniSamuelOgundipe ilivuma pale mwanahabari wa Nigeria Samuel Ogundipe alipowekwa kizuizini kwa siku tatu na kikosi maalum baada ya kukataa kutaja chanzo chake cha taarifa kuhusu kuwazuia kwa nguvu watunga sheria kuingia katika ukumbi wa Bunge la Nigeria mwanzoni mwa Agosti 2018.

Deji Adeyanju, mwanaharakati wa kisiasa na mwanachama cha upinzani alikamatwa tena Disemba 2018 na amekuwa kizuizini tangu hapo kwa sababu ya “mswada mpya.”

Kwa uwazi kabisa Buhari amekuwa akionesha chuki dhidi ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari. Katika hotuba yake kwa wanasheria mwaka jana, alisema kuwa “utawala wa sheria ni lazima uwe chini na mamlaka ya mkuu wa ulinzi na kwa maslahi ya nchi.”

Upande mwingine Abubakar ameahidi kuendesha serikali ” ya mfumo shirikishi” ambayo itaunganisha utofauti wa Wanigeria na kuweka “mazingira sawa na ya haki ambapo haki za raia wote zitalindwa na serikali yenye uwazi.”

Ni muda pekee utakaoonesha ni jinsi gani mambo haya yatakavyojifunua katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya hapo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.