- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Tunaelewa Nini Kuhusu Uchaguzi Mkuu Ujao Nchini Msumbiji?

Mada za Habari: Msumbiji, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Vita na Migogoro
[1]

Bango lenye picha ya Rais wa Msumbiji Filpe Nyusi Nyusi. Picha na Dércio Tsandzana, na imetumiwa kwa kibali.

Kwa mara ya sita tangu mwaka 1994, Msumbiji itamchagua Rais wake mwingine mwezi Oktoba 2019 – na kwa mara ya kwanza itawachagua wakuu wa majimbo.

Ingawa ushindani huo haujafunguliwa rasmi, kwa ujumla inategemwa kwamba upinzani ndani ya siasa za Msumbiji utashindana: Frelimo, chama kinachoongoza serikali tangu 1994 na Renamo ambacho ni chama kikuu cha upinzani.,

Itakuwa mara ya kwanza Renamo kupambana bila kiongozi wao wa kihistoria Afonso Dhlakama ambaye amekiongoza chama hicho kwa zaidi ya miongo minne. Dhlakama alifariki tarehe 3 Mei, 2018 [2], kutokana na mshtuko wa moyo. Dhlakama atakumbukwa kama kiongozi wa Renamo ambaye alisaini Makubaliano ya amani na Rais wa zamani Joaquim Chissano mwaka 1992 ambayo yaliiweka Msumbiji katika mstari kuelekea Demokrasia.

Ili kushinda, Renamo imemchagua Ossufo Momade baada ya kupendekezwa na mkutano mkuu wa chama uliofanyika Gorongosa mwezi Juni mwaka 2018, katika jimbo la kati la Sofala ambapo ndio ngome ya Renamo.

Yamkini, ndiye atakuwa mgombea wa Renamo mwezi Oktoba, na inawezekana akapambana na Rais wa sasa Filip Nyusi ambaye anatoka chama Frelimo na Daviz Simango—ambaye anatoka chama kingine cha upinzani cha Demokrasia Msumbuji (MDM).

MDM ilianzishwa mwaka 2009 sambamba na Renamo na Frelimo ndiyo vyama ambavyo vina wawakilishi katika Bunge la Jamhuri au kuongoza manispaa. Daviz Simango amegombea urais na kushindwa katika chaguzi mbili zilizopita za urais.

Upigaji kura wa mwezi Oktoba unaweza kutokea katikati ya makubaliano ya kusitisha mapigano [3] yaliyosainiwa kati ya jeshi la Renamo na majeshi ya serikali mwaka 2016, ambapo hivi karibuni pande hizo zimevutana maeneo ya pembezoni mwa Msumbiji.
Mwezi Februari, 2019, Tume ya taifa ya uchaguzi (CNE) [4] ilitahadharisha umma juu ya ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuratibu uchaguzi nchi nzima.

Tarehe muhimu

  • 01/04 – 15/05: uandikishaji wa wapiga kura
  • 31/08 a 12/10: kuanza kwa kampeni
  • 15/10: Siku ya kupiga kura

Labda muhimu zaidi ni kwamba, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa wanamsumbiji kuchagua magavana wa majimbo. Siku za nyuma, walikuwa wakiteuliwa na Rais.

Mabadiliko hayo ni matokeo ya makubaliano mazito na yaliyochukua muda marefu kati ya Renamo na serikali.

Wakati Rais hajaondoa sheria ambayo itaendana na mabadiliko haya, hata hivyo inaaminika kuwa atafanya hivyo.