- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wafahamu Wagombea wa Kiti cha Urais Naijeria katika Uchaguzi wa 2019

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Naijeria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Utawala

Wagombea wa kiti cha Urais wa Nigeria mwaka 2019 [Picha zimechanganywa na Nwachukwu Egbunike].

Naijeria, nchi ya Afrika yenye watu wengi zaidi watafanya uchaguzi wake wa Rais hapo Februari 16, 2019. Ingawa kuna wagombea wa urais 73 [1], mpambano wa kuwania Aso Rock — kiti cha urais wa Naijeria, zitakuwa kati ya wagombea na wapinzani wawili wakuu kutoka kwenye upande unaofahamika kama “nguvu ya tatu”, kikundi cha wenye matumaini ambao inaonekana ni wageni kwa siasa za Nigeria.

Vyama vikuu vya siasa vya Naijeria vya Chama cha Maendeleo kwa wote na Chama cha Demokrasia Kwa Watu,vitakuwa vinawapambania wagombea wake:

Raisi wa Nigeria Muhammad Buhari. Picha ya Creative Commons

Muhammadu Buhari [2]

Mgombea anayemaliza muda wake kutoka chama cha Maendeleo kwa watu wote. Buhari alishinda kiti cha Uraisi mwaka 2011 baada ya kumshinda rais wa zamani Goodluck Jonathan. Kuibuka kwa Buhari madarakani kulitokana na uadilifu wake na kudhaniwa kuwa angeweza kutokomeza rushwa na wanamgambo wa Boko Haram [3]. Hata hivyo, chini ya uongozi wake Nigeria imeendelea kushuhudia uvunjifu wa amani na migogoro [4] baina ya wafugaji na wakulima ambapo wafugaji kutoka kaskazini wamesogea kusini zaidi wakitafuta ardhi ya malisho. Pia, haki za binadamu [5] zimevunjwa sana katika utawala wake, ukatili na rushwa vimeonekana katika ngazi za juu za serikali.

Atiku Abubakar [Picha kutoka katika tovuti ya Kampeni].

Atiku Abubakar [6]

Abubakar ni makamu wa rais wa zamani na mgombea wa Chama cha Demokrasia kwa Watu. Amekuwa akijaribu kwa mara mbili mfululizo lakini hakufanikiwa kushinda urais kwa mara zote. Hata hivyo kampeni zake zimepata kuungwa mkono baada ya kupatanishwa na bosi wake, Rais wa zamani Olusegun Obasanjo [7] — ambaye ameuelezea uongozi wa Buhari kama serikali iliyoshindwa. Kama makamu wa raisi Abubakar alisimamia ubinafsishwaji [8] na uuzwaji wa mashirika ya Umma yaliyokuwa yakiendeshwa kwa hasara.

Wagombea wengine ambao wana matumaini kuwaangalia ni:

Oby Ezekwesili [picha ilitolewa na mwangalizi wa kampeni kwa ajili ya media]

Obiageli [Oby] Ezekwesili [9] 

Ezekwesili, mwanamke pekee katika kinyang'anyiro cha mwaka huu, alishawahi kuwa waziri wa madini na kisha waziri wa elimu katika kipindi cha Olusegun Obasanjo kati ya 1999 mpaka 2007. Pia alikuwa makamu wa Raisi wa Benki ya Dunia divisheni ya Afrika kuanzia Mei 2007 mpaka Mei 2012. Ezekwesili amekuwa mstari wa mbele katika kupambana kuwaokoa wasichana 200 [10] wa shule ambao walitekwa na kikundi cha wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram mwaka 2014. Ni mwanzilishi mwenza wa kampeni ya #WarudisheniMabintiZetu (BBOG). Pia ni mpeperusha bendera ya Urais kwa chama cha Washirika Cha Nigeria.

Kingsley Moghalu [Picha kutoka katika tovuti ya kampeni].

Kingsley Moghalu [11]

Moghalu ni profesa wa biashara za kimataifa na sera za umma huko Fletcher shule ya sheria na Diplomasia katika chuo kikuu cha Tufts huko Massachusetts, Marekani. Hapo kabla Moghalu alifanya kazi na umoja wa mataifa kuanzia mwaka 1992 hadi 2008. Alikuwa naibu gavana wa Benki kuu ya Nigeria kuanzia mwaka 2009 hadi 2014, ambapo “aliongoza mabadiliko makubwa [12] katika mfumo wa benki wa Nigeria baada ya mgogoro wa kiuchumi wa dunia.” Ni mgombea wa Chama cha Maendeleo ya Vijana Nigeria.

Omoyele Sowore [Picha kutoka kwa skrini wakati wa mahojiano na kituo cha CNBCAfrica, Dec 13, 2018].

Omoyole Sowore [13]

Sowore ni muanzilishi na mchapishaji wa Wanahabari wa Sahara [14] (SR), ambalo ni gazeti la habari za uchunguzi la mtandaoni. SR imekuwa ikielezewa kuwa kama mtandao wa Wikileaks ya Afrika [15]. Mwanaharakati huyu wa haki za binadamu anagombea chini ya bendera ya African Action Congress.

Mbio hizi ni kwa ajili ya maisha yajayo ya Nigeria

Buhari na Abubakar ndio wagombea wakuu katika uchaguzi huu. Wanaume hawa wameshakuwa katika uwanja wa siasa za Nigeria kwa muda mrefu. Kwa upande mwingine, Ezekwesili, Moghalu, Sowore, ambao ndio “nguvu ya tatu” ndilo kundi linaloingia katika siasa za kusaidiana kwa mara ya kwanza.

Buhari atakuwa ananadi “mafanikio” ya utawala wake kwa kipindi cha miaka mitatu na ni lazima agombee akiwa na ukweli kuwa Nigeria ilitangazwa kama mji mkuu wa umaskini wa dunia [16]. Gazeti la the Punch lilielezea uteuzi wa “kujuana wa Buhari [17]” kama “usio wa kawaida”na ameiacha nchi ikiwa imegawanyika sana. Vita yake dhidi ya rushwa ilionekana yenye upendeleo na uonevu. Hatua yake ya hivi karibu [18] ya kumshitaki Jaji mkuu wakati uchaguzi umekaribia ilitafsiriwa na chama cha Majaji kuwa ni muendelezo wa mashambulizi [19] dhidi ya wakuu wa taasisi mbili huru za serikali” chini ya utawala wa Buhari.

Kwa upande mwingine Abubakar yeye anajinadi kwa sera za “mafanikio” ya “faida nyingi [20] zilizotokana na biashara”. Hata hivyo ana kikwazo kikubwa cha kuwaza kuhusu nguvu ya mpinzani wake mkuu anayemaliza muda wake.

Hata hivyo, yeyote atakayeshinda uchaguzi wa 2019 atakumbana na changamoto nyingi ikiwamo kuimarisha uchumi [21], usalama wa ndani [22], kupanga mamlaka upya  [23]na kupunguza mamlaka ya viongozi [24], na kuondoa siasa za kidini na [25] kikabila.

Angalizo la Mwandishi: Nakala ya mwanzo ya chapisho hili lilieleza kuwa kuna wagombea 35 wa urais na imehuishwa na kuonesha kuwa wapo wagombea wa Urais 73.