- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Samoa Yamkamata Bloga Maarufu ‘Mfaume Faipopo’ kwa Tuhuma za Kumkashifu Waziri Mkuu

Mada za Habari: Nchi za Visiwani, Samoa, Censorship, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi
[1]

Bloga Malele Paulo ambaye anajulikana kama mfalme Faipopo. Chanzo: Facebook

Askari wa Samoa walimkamata [2] bloga Malele Paulo aishie Australia tarehe 8 Februari wakati akitembelea nchi hiyo kuhudhuria mazishi ya mama yake. Malele ambaye huikosoa sana serikali kwa jina la kalamu ya Mfalme Faipopo [3].

Askari wamethibitisha kwamba Malele alikamatwa kwa “kutoa kauli za uongo kwa nia ya kumwuumiza mjumbe wa jumuia ya heshima ya Samoa.”

Mwezi Agosti 2018, Waziri Mkuu Tuilaepa Sailele Malielegaoi alisajili mahakamani malalamiko ya kukashfiwa dhidi ya Malele na yamesababisha kukamatwa kwake alipoingia nchini mapema mwezi Februari. Awali Malele aliachiwa [4] kwa dhamana tarehe 9 Februari, na kwa sababu hiyo aliweza kuhudhuria mazishi ya mama yake.

Mwaka 2013, Samoa [5] iliondoa sheria dhidi ya maandishi yenye lengo la kukashfu [5] katika sheria yake ya jinai kama mkakati wa mageuzi ya sheria ya vyombo vya habari. Lakini mabadiliko hayo hayakudumu. Mwishoni mwa mwaka 2017, Bunge la nchi ya kisiwa cha Polynesian walipiga kura bila kupingwa juu ya kurudisha [6]sheria yake ya jinai ya maandishi ya kukashfu baada ya waziri mkuu Tuilaepa Sailele Malielegaoi kusema [7] inapaswa “kupambana na waandishi waongo na wakorofi,” licha ya upinzani mkali kutoka kwa mawakili wa vyombo vya habari. Serikali ya Tuilaepa ilisema sheria hiyo itatumika dhidi ya mabloga na watumiaji wa Facebook wasiojulikana ambao wanasambaza uongo na habari za upotoshaji.

Waziri Mkuu alirejea sheria hii katika malalamiko yake dhidi ya Malele ambaye ameshitakiwa kwa kutuma habari za uongo juu yake na siasa za Samoa. Ililipotiwa kuwa Malele aliandika kwenye Blogi yake kwamba Tuilaepa alifanya mauaji, wizi, rushwa na biashara ya magendo ya usafirishaji ya silaha.

Tuilaepa alisisitiza [8] kuwa hayupo dhidi ya wananchi wanaotoa mawazo yao:

Sizuii yeyote kutumia haki yake ya uhuru wa kutoa mawazo au uhuru wa kujieleza bali nachukua hatua pale haki za watu wasio na hatia, kama mimi, zinapovunjwa kupitia uongo na udanganyifu. Sheria iliundwa kuzuia aina hii ya kuongopa na kushambulia wajumbe wa jumuia kupitia vyombo vya habari.

Baada ya Tuilaepa kusajili mahakamani malalamiko ya kukashfiwa, serikali yake inatafuta namna ya kumrudisha Malele nchini kutoka Australia.

Pia, kauli ya polisi juu ya kukamatwa kwa Malele ilitahadharisha [9] umma kuepuka kutoa kauli za kukashfu kupitia vyombo vya habari:

Maumivu yaliyosababishwa kupitia vyombo vya habari kwa baadhi ya wajumbe wa jumuia ni suala ambalo sheria hizi zimeundwa kwa ajili hiyo. Tutajitahidi kufanya kadri ya uwezo wetu kuwasaidia wale wanaothiriwa na kauli za uongo kwenye majukwaa ya vyombo ya vya habari pindi tu polisi wanapoleta malalamiko.

Mwenyekiti wa baraza la uhuru wa Pacific Bernadette Carreon wa Palau alieleza juu ya [10] kukamatwa kwa Malele kama shambulio dhidi ya uhuru wa kutoa maoni:

Lenga kupambana na rushwa na sio uhuru wa kutoa maoni.

Sheria mpya, ambayo imetokana na sheria ya zamani ya maandishi ya kukashfu, tangu ukoloni, imewasukuma viongozi wa Samoa kugeuka na kuangalia nyuma badala ya kuangalia mbele.

Bloga Ole Palemia ambaye ni mkosoaji mwingine wa serikali, alikosoa [11] uamuzi wa kumkamata Malele:

Kitu ambacho watu mara nyingi hukumbuka na wanachotaka kujua ni kwamba mla rushwa waziri Mkuu Tuilaepa na wanasiasa wote ni viongozi wa umma kwa hiyo wanapaswa kukosolewa na umma – hiyo ndiyo inayoitwa demokrasia.

Kukamatwa kwa Malele kumeibua mjadala mkali katika Samoa. Taarifa ya habari iliyotafiti [12] maoni ya baadhi ya wananchi ambao walieleza juu ya kukamatwa kwa Malele na wengine walikubalina na kesi hiyo ya kukashfu na wakashauri wakosoaji kuwa na heshima kwa waziri mkuu wa nchi.

Malele amepangiwa [13] kufikishwa mahakamani tarehe 5 Machi.