Mpambano wa Majenerali Wastaafu wa Jeshi la Naijeria na Mchango wao Katika Uchaguzi wa Rais 2019

Rais Mstaafu wa Naijeria Olusegun Obasanjo. [Creative Commons (CC BY 2.0)/ Flickr, June 27, 2011.]

Wakati Nigeria wakijiandaa na uchaguzi mwingine wa Rais mwezi wa pili, maafisa wa jeshi wastaafu waliogeuka kuwa wanasiasa wamekuwa kielelezo cha kuelewa uelekeo wa siasa za Nigeria. Naigeria imekuwa ikiongozwa na labda Jenerali Mstaafu au wale wanaoungwa mkono na majenerali hao tango 1999 pale mfumo wa serikali ya kidemokrasia uliporejea.

Mgongano wa wazi wa hivi karibuni kati ya Rais wa zamani  Olusegun Obasanjo na Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari — wote wakiwa Madikteta wastaafu wa jeshi — una mchango mkubwa katika uchaguzi wa mwezi wa pili.

Katika barua ya wazi isiyo ya kawaida kwa Buhari, Obasanjo alimtuhumu kwa kupanga kuiba kura katika uchaguzi wa 2019. Aliandika:

Demokrasia hukosa maana kama uchaguzi utafanywa na watu ambao wanatakiwa wasiwe na upendeleo na wawe na maamuzi yasiyoegemea upande wowote lakini wanaonyesha kutokuwa na uaminifu wakitenda kwa upendeleo bila kificho tena kwa kurudia rudia na kwa upumbavu.

Obasanjo alisisitiza kuwa Buhari anaweza asiitishe uchaguzi “huru na wa haki” na akaonya kuwa “yanayotokea wakati wa Buhari yanaweza yakawa kama tuliyoshuhudia wakati wa Jenerali Sani Abacha.”

Mwaka 1998, Sani Abacha, Dikteta wa kijeshi, aliitisha uchaguzi mkuu lakini ilikuwa wazi hakuwa mpango wa kukabidhi madaraka kwa wananchi. Vyama vitano vya siasa kwa wakati huo vilimsimamisha Abacha kama mgombea wao pekee wa Urais. Abacha ambaye kwa sasa ni marehemu amekuwa sio maarufu miongoni mwa wananchi kwa sababu alikandamiza haki za binadamu na alikula rushwa. Obasanjo alidai kuwa Buhari anapita “njia ile ile” ya Abacha “ndani ya ukichaa wa kukata tamaa.”

Shehu Garba, afisa habari msaidizi wa Rais Buhari, aliipuzia barua ya Obasanjo:

Uchaguzi unaoanza mwezi Februari utakuwa huru na haki kama Rais Buhari alivyouhaidi umma na jumuiya za kimataifa.

Obasanjo, mwandishi wa barua?

Olusegun Obasanjo, Mwanajeshi na mkuu wa jeshi mstaafu (1976-1979) na baadaye Rais wa Naijeria aliyechaguliwa kidemokrasia (1999-2007), amekuwa akizikosoa mara kwa mara serikali za Nigeria zilizokuja baada yake.

Mwaka jana, Obasanjo alimshauri Buhari asitafute kipindi cha pili cha Urais katika uchaguzi unaokuja badala yake “afikirie kupumzika kwa kuwa anastahili kwa sababu ya nyakati na pia umri. “Ushauri huu ulileta mgawanyiko nchini Naijeria kwa sababu Obasanjo alimuunga mkono mkuu Buhari wakati wa uchaguzi wa Rais 2015.

Hapo kabla Obasanjo alimkosoa Rais Goodluck Jonathan katika barua ya wazi aliyoiandika mwaka 2013, Obasanjo akimtuhumu Jonathan “kuipeleka nchi katika uharibifu kwa kuruhusu udanganyifu, rushwa na kutokuaminiana kuchana vazi la taifa.”

Cha kushanza ni kuwa pia  Obasanjo aliunga mkono uchaguzi wa Jonathan hapo 2011. Na mwaka 2007, alichochea kuchaguliwa kwa mtangulizi wa Jonathan, Umaru Musa Yar’Adua. Hata hivyo, Obasanjo alikwenda kinyume na Yar’Adua alipougua na hakukabidhi mamlaka ipasavyo kwa Jonathan, aliyekuwa Makamu wake wakati huo.

Rais Mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan akiwa na Rais mpya aliyeapishwa Rais Muhammadu Buhari katika sherehe za kuapishwa kwake Mei 29, 2015. Picha za Masijala ya Umma kutoka Idara Nchi-Marekani.

Majenerali waliostaafu Nigeria huwa hawapumziki

Mazingira ya siasa za Nigeria yameshikiliwa na majenerali wastaafu wa jeshi au maswaiba zao. Kwa mfano Obasanjo, amekuwa kiungo kikubwa katika kupatikana kwa maraisi wa Nigeria kuanzia 2007 mpaka 2015. Hata hivyo ukiacha raia Yar’Adua na Jonathan – ambao aliwaunga mkono na kisha kuwakosoa, kwa namna fulani Buhari ni tofauti.

Ingawa Obasanjo aliunga mkono uchaguzi wa Buhari 2015, hawezi akachukua heshima hiyo mwenyewe. Na hii ni kwa sababu kuingia madarakani kwa Buhari iliwezekana kwa sababu alifanya ushirikiano na marehemu Bola Tinubu wa chama cha Action Congress of Nigeria (ACN). Baadaye Chama cha Buhari Congress for Progressive Change (CPC) kiliungana na ACN, mwezi Februari 2013, na kuunda Chama cha Maendeleo kwa Wote (APC) .

Kwa kuongezea, Buhari alikuwa Mkuu wa jeshi mstaafu (1983-1985) ni mwanachama wa “klabu” ya Majenerali wastaafu ambao wameshikilia ulimwengu wa siasa za Nigeria. Kwa hiyo, haijalishi karipio la Obasanjo ni kali namna gani, mengi yatategemea mwenendo wa mfumo wa mamlaka nzima ambapo wote ni wahusika.

Hata hivyo Obasanjo hayupo mwenyewe katika kumkosoa Buhari.

Theophilus Danjuma, ambaye ni Jenerali Mstaafu wa jeshi mwezi Machi mwaka jana alilituhumu “jeshi la Nigeria kufadhili mauaji yanayoendelea nchini Nigeria .” Danjuma, ambaye ni mkuu wa majeshi mstaafu na baadaye akawa waziri wa ulinzi alilaumu jeshi kwa kuwa na upendeleo katika mgogoro baina ya Wakulima na wafugaji nchini, na hasa huko nyumbani kwake, Jimbo la Taraba. Vilevile, hivi karibuni Danjuma alitoa tahadhari kuhusu mipango ya kutumia “wanajeshi na polisi” kuendesha uchaguzi wa 2019.

Vile vile, Februari mwaka jana, mkuu wa jeshi mstaafu Ibrahim Babangida alimshauri hadharani Rais Buhari kutokugombea tena katika uchaguzi huu akisema kuwa katika karne hii ya 21, Nigeria inahitaji kizazi kipya . Anaamini kuwa “zitakuja nyakati katika maisha ambapo maslahi binafsi hayawezi kupindua maslahi ya Taifa.”

Lakini itachukua muda kidogo mpaka Nigeria ije ipate Rais wa Kiraia ambaye ahusiani au hana ushirika na ‘klabu’ ya Majenerali wajeshi wastaafu..

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.