- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Guinea Inataabika Chini ya Rais Condé Anayeungwa mkono na Urusi Kubadili Katiba Agombee Awamu ya Tatu

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Guinea, Urusi, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Utawala

[1]

Picha ya Skrini kutoka katika video ya Balozi wa Urusi akihutubia katika kituo cha runinga cha Africa Guinee TV huko YouTube [kwa Kifaransa]

Hapo Januari 9, 2019, Alexander Bregadze, Balozi wa Shirikisho la Urusi kwa Jamuhuri ya Guinea alituma salamu za Mwaka mpya kumpongeza Rais Alpha Condé, wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Alirekodi video hiyo ya salamu akiwa huko Conakry, mji mkuu, ambapo ndipo ofisi yake ya kidiplomasia ipo-na katika hotuba yake, alilenga [2]jambo la msingi, uwezekano wa Wa-Guinea kubadilisha katiba yao na kumruhusu Rais Condé kugombea kwa kipindi cha tatu baada ya muhula wake kuisha hapo 2020:

Depuis que la Guinée est devenue la Guinée d’Alpha Condé, elle est vraiment en marche. Monsieur le Président vous êtes un exemple phare pour la jeunesse guinéenne. Malheureusement, le principe d’alternance qui domine beaucoup de Constitutions dans le monde, mais pas toutes heureusement, impose la mentalité de revanche: ‘C’est notre tour, maintenant c’est nous qui devons diriger le pays…’

Mais les Constitutions ne sont pas ni dogme, ni Bible, ni Coran.

Tangu Guinea imekuwa Guinea ya Alpha Condé, kwa kweli imekuwa katika mwendo. Mheshimiwa Rais, wewe ni kielelezo kwa vijana wa nchi hii. Bahati mbaya, utaratibu wa kukabidhiana madaraka, ambayo imetawala katiba nyingi duniani, sio wote wanafurahia kuweka msingi wa mtazamo wa kulipa fadhila: ‘Ni muda wetu sasa, lazima tuiendeshe nchi….’

Lakini katiba sio Biblia au Msahafu .

“Katiba zijiakisi katika uhalisia”, aliendelea kusema mbele ya Condé, akiweka wazi kuwa, uhalisia haujajiakisi katika Katiba yenyewe: “Hata kwa Wakristo, kuna Agano Jipya na Agano la Kale.”

Kulingana na balozi, mambo yote ni sawa ndani ya Guinea. Lakini hata hivyo hali halisi inaonesha ukweli mwingine.

Waalimu waliingia katika mgomo wa pamoja mwaka huu ambao ulidumu kwa miezi mitatu [3], ukosefu wa ajira umeongezeka maradufu na imegundulika kuwa wahamiaji wengi haramu wanaoingia huko Ulaya kwa mwaka 2018 asili yao ni nchini Guinea, takwimu zikioneshwa wanakaribia watu 13,068 [4].

Bado balozi aliendelea kusema [5]:

Sous nos yeux la Guinée devient le pays le plus électrifié de l’Afrique. D’une année à l’autre,  on circule mieux sur les routes entre Conakry et les régions guinéennes.

Mbele ya macho yetu, Guinea inakuwa nchi iliyosambaa huduma ya umeme zaidi Afrika. Mwaka hadi mwaka barabara kati ya Conakry na mikoani zinarahisha usafirishaji.

Katika makala ya gazeti la Vision Guinée, mwandishi wa habari Pathé Bah aliandika kuwa Ousmane Kaba, mshauri wa mipango wa zamani wa Rais Condé, alifahamika [6] kwa kusimamia maslahi ya umma:

La Guinée est dans l’obscurité, Il n’y a pas d’électricité dans notre pays. C’est pourquoi, je me suis battu pour avoir l’argent pour construire Kaleta sur le Konkouré. On se bat pour avoir beaucoup de barrages sur le Konkouré, parce que cela fait avancer le pays.

Guinea iko gizani. Hakuna umeme katika nchi yetu. Ndiyo maana nilipigania fedha za kujenga Kaleta [kinu cha kufulia umeme wa maji] katika mto Konkouré. Tunapambana kupata mgawo mkubwa kwa ajili ya Konkouré, kwa sababu unaipeleka nchi mbele.

Na kwa uchumi wa nchi, waziri wa fedha alikadiria [7] kiwango cha ukuaji kuwa kwa asilimia 5.8 kwa mwaka 2018, kukiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 8.  Benki ya Maendeleo ya Afrika [8] ilihakiki kuwa Guinea imefikia kukua kwa pato la ndani kwa asilimia 6.6 kwa mwaka 2016 na asilimia 6.4 kwa mwaka 2017 — lakini hilo halikumzuia balozi kutangaza [9] namba zilizokuzwa tu ili kuonesha uchumi unakua:

Ces dernières années on a constaté la croissance entre 10,5% en 2016 et de 6 au 7% en 2018 avec le pronostic de 7% en 2019…Connaissez-vous beaucoup de pays en Afrique qui font mieux ?

… Kwa miaka michache iliyopita, tumeona ongezeko la kukua kwa uchumi kati ya asilimia 10.5 mwaka 2016 na kuanzia asilimia 6 hasi 7 asilimia kwa mwaka 2018 likiwa na matarajio ya asilimia 7 kwa mwaka 2019. Mnafahamu ni nchi ngapi za Afrika zinazofanya vyema?

Balozi aliongezea hali ya barabara katika litania yake ya sifa kwa Raisi. Hata hivyo, Alimou Sow, bloga maarufu wa Guinea alishirikisha [10] habari yenye ukinzani katika blogu yake:

Je suis debout dès potron-minet pour affronter, en solitaire, le tronçon jugé le plus difficile, Conakry-Kindia — 135 km que l’on accomplissait, il y a quelques années, en un peu moins de deux heures montre en main. Maintenant, il faut rajouter deux heures supplémentaires pour crapahuter sur la même distance devenue un parcours de rêve pour un rallye raid de type «Paris-Dakar», tant la route est en piteux état.

Nimekuwa macho tangu kulipopambazuka nikipambana mwenyewe na barabara inayosadikiwa kuwa korofi zaidi ya kutoka Conakry kwenda Kindia kilomita 135, ambapo miaka michache iliyopita ungetumia chini ya masaa mawili ukipima muda. Sasa, lazima uongeze japo saa nyingine mbili kutambaa umbali ule ule, na imegeuka kuwa barabara ya ndoto kwa ajili ya mbio za magari za uvumilivu za à la ‘Paris-Dakar’, ni hatari sana kwa hali hiyo ya barabara.

Mwaka 2016, wanachama wa chama cha mabloga wa Guinea, walianzisha kampeni ya kuamsha uelewa kuhusu hali ya barabara  za nchini na walionesha kukasirishwa kwao kwa kutumia hashtagi #montronsnosroutes [tuoneshe barabara zetu].

[11]

“Chama cha Mabloga Guinea wataanzisha kampeni kukemea hali ya barabara za Guinea. Wazo kuu ni kushirikisha picha katika mitandao ya kijamii zikiwa na kauli mbiu #TuonesheBarabaraZetu.” Picha ya ufunguzi wa kampeni ya Chama cha Mabloga wa Guinea #montronsnosroutes. Imetumika kwa ruhusa.

Hotuba ya Balozi wa Urusi imeleta fadhaa kwa jamii na jumuiya za kiraia na zile za kidiplomasia. Kiongozi wa upinzani wa Guinea, Cellou Dalein Diallo, amekosoa mtazamo wa mwanadiplomasia huyo kwa kuelezea [12], imenukuliwa na Balla Yombouno katika gazeti la Le Djely:

Il a été manipulé par Alpha Condé [le Président de la Guinée] lui-même. Et nous savons qu’il est le représentant d’une grande nation, d’un grand pays qui a participé activement à la décolonisation du continent africain, et qui a eu une relation exemplaire avec la Guinée dans le respect du principe de non-ingérence dans les affaires intérieures […] Nous allons essayer aussi de saisir le gouvernement russe pour faire état de cette prise de position …

Amekuwa akiendeshwa na Condé mwenyewe. Na tunajua kuwa yeye ni mwakilishi wa nchi kubwa, nchi yenye nguvu iliyoshiriki kikamilifu katika kuuondoa ukoloni barani Afrika, na ambayo imekuwa na uhusiano wa mfano na Guinea kwa kuheshimu kanuni ya kutokuingilia masuala ya ndani ya nchi. Tunapambana kuwasiliana ma serikali ya Urusi ili kuweka msisitizo katika eneo hilo …

Akiongea kwa niaba ya wanaharakati wa mashirika ya kijamii, Gabriel Haba, Rais wa Brigedi ya Hatua za Kiraia, alielezea [13]  hasira iliyoamshwa na balozi kwa kuunga mkono huko; mwanahabari Ibrahima Sory Barry aliandika katika mtandao wa Aminata.com:

La question de l’alternance est une question de souveraineté. Et la souveraineté appartient au peuple. Il n’est pas du rôle d’un ambassadeur de dicter à la Guinée sa destinée. C’est de l’ingérence dans les affaires internes de notre pays.

Suala la kupokezana madaraka kisiasa ni suala huru. Na uhuru uko kwa wananchi. Sio sehemu ya majukumu ya balozi kusimamia majaliwa ya Guinea. Hii ni kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu.

Shirika la Juimiya ya Kiraia Cellule Balai Citoyen (Citizen's Sweep Up) walitoa waraka [14] kwa vyombo vya habari uliokuwa unasomeka hivi kwa sehemu:

La Guinée vit sous le risque d’un embrassement sans précèdent susceptible de découler d’un forcing politico-social en faveur d’un 3e mandat en violation de l’actuelle constitution mais aussi de l’éthique dans la gouvernance démocratique. Cette tentative qui se fait de plus en plus sentir peut être source d’une violence politique aux graves violations de droits de l’homme dans notre pays qui peine encore à cicatriser le lourd passif dans cette matière, de l’indépendance à nos jours.

Guinea ipo katika hatari ya aibu ambayo haijawahi kutokea na hii ni endapo kutachomekwa kipindi cha tatu kutokana na msukumo wa kisiasa na kijamii na kuvunja katiba iliyopo na hakika taratibu za utawala wa kidemokrasia. Majaribio yanayoonekana kuongezeka yanaweza kuamsha vurugu za kisiasa yakiwa na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu katika nchi yetu, ambayo bado inapambana kujiweka kumbukumbu nzuri na nzito ya urithi tangu uhuru mpaka sasa.

Huko Facebook, mwandishi na mtoa maoni Ibrahim Marie Sanoh aliandika [15]:

C'est fort abstrus que ce soit un étranger qui doit saluer les prouesses du pouvoir guinéen et plaider à ce qu'il lui soit accordé d'autres années pour faire du pays le plus électrifié du contient le plus industriel du monde, tandis que le peuple qui l'a investi manifeste une cruelle indifférence et ne pipe mot.

Ni namna ya kipekee na inayopendeza kuona raia wa kigeni akitoa mchango wake katika uongozi wa Guinea kwa kuomba uongozi huo upewe miaka zaidi ili kuifanya nchi hiyo iwe nchi iliyosambaa umeme kuliko nchi zote za bara lenye viwanda vingi zaidi duniani, wakati watu waliouweka uongozi huo madarakani wanatendwa kikatili na hawana la kusema .

Wakati huo huo, tabia za mabalozi wengine zilivuta [16] hisia za bloga wa Guinea Nouhou Baldé:

Cette déclaration est tellement grave que le silence des autres n'est pas à excuser si facilement. D'autant que certains de ceux qui ont pris la parole par la suite (l'ambassadeur du Maroc, le représentant de la Banque mondiale…) ont dit ne pas dire mieux que le russe. Personne ne s'est désolidarisé de cette déclaration et aucune ambassade n'a publié un communiqué…

Azimio hili ni hatari kiasi kwamba ukimya wa mabalozi wengine hauwezi ukachukuliwa kirahisi. Wote ni sawa tu hata na wale waliozungumziwa (balozi wa Morocco na mwakilishi wa Benki ya Dunia..) wamesema yaleyale, hivyo ni kusema hawana utofauti na mwenzao,  balozi wa Urusi. Hakuna hata mmoja aliyejiengua katika tamko hilo na hakuna ubalozi ulishatoa waraka kuhusu jambo hilo….

Hapo Januari 14, mamlaka za ulinzi zilitawanya  [17]maandamano yaliyoandaliwa nje ya ubalozi wa Urusi na  mashirika ya kiraia yakipinga kuhusu maoni ya balozi.