Australia Waikumbuka Jumamosi Nyeusi kwa Kuadhimisha Miaka 10 ya Janga la Moto wa Nyika

Jumamosi ya Giza- Anguko la ardhi

Anguko la ardhi hapo April 8, 2009 – Picha na hisank ya Elizabeth Donoghue  katika akaunti ya Flickr 
(CC BY-NC-ND 2.0)

Miaka kumi iliyopita siku ya Jumamosi 7 Februari 2009, Victoria ilipatwa na janga la nyika kuwaka moto ambapo watu 173 waliuawa na zaidi ya mia nne kujeruhiwa na makazi zaidi ya elfu mbili kuharibiwa na moto huo. Watu saba walifariki baadaye kutokana na majeraha.

Katika Juma la maadhimisho hayo kwa mwaka 2019, wakazi wa Victoria waliikumbuka Jumamosi Nyeusi  , kwa vyombo vikubwa vya habari kuonesha habari nyingi za watu binafsi kuhusu moto huo. ABC Melbourne, chombo cha habari cha huko kilikumbuka wahanga kwa kushirikisha habari za manusura wa janga hilo.

Wengine walishirikisha kumbukumbu zao mitandaoni. Indya, katika blogu yake ya Mtembezi Mdogo, alielezea jinsi alivyopoteza makazi yake na akashirikisha madhara ya moto ule katika maisha yake kuanzia wakati ule:

Miaka kumi yote imepita lakini sidhani kama ipo siku moja inapita bila mimi kutamka au kufikiria kuhusu moto.

[…] Hakika bado nina kihoro na nina wasiwasi ninapokuwa karibu na vitu vya moto kama vile oveni, hita na hata viberiti. Kama muokaji unaweza kuona ni kwa kiasi gani napata tabu nikiwa na hofu hizo hasa ninapoenda kutoa kitu kwenye oveni halafu ghafla jambo linaenda kinyume na matarajio au kitu kingine kama hicho huwa napata hofu ya ghafla na kufadhaika.

[…] Kesho nitakuwa nawaza kuhusu wote waliopatwa na mabaya kuliko mimi na naamini kuwa wale walio hai bado na waliopoteza vitu vingi wanaendelea vyema. Lakini pia nitakuwa natafakari juu yangu na kuruhusu kujisikia vyovyote nitakavyojisikia kwa sababu hisia zangu ni sahihi pia. Hofu yangu na huzuni ni sahihi pia na imekuwa hivyo mara zote imekuwa hivyo ila nilichelewa kutambua hilo.

Dianne McNamara aliposti ujumbe pekee wa pili katika ukaunti hii akisema:

Mwanasheria wa Melbourne, Georgia alikuwa na miaka kumi na tano wakati huo. Aliwakilisha hisia za wengi:

Robin Steenberg alishirikisha kumbukumbu ya kusikitisha:

Watu wengi wanaunganisha janga la Jumamosi Nyeusi na hali mbaya ya hewa ya sasa ambayo inaleta madhara katika maeneo mengine ya nchi. Janga lingine la asili la mafuriko limeikumba ukanda wa Kaskazini mwa Queensland ikifuatiwa na mvua. Blair Drysdale alielezea baadhi ya madhara katika maeneo ya bara:

Hali katika mji wa Pwani wa Townsville hali ilikuwa mbaya pia. Kampuni ya uzalishaji video ya Ruptly ilirekodi mafuriko hayo:

Mkazi wa Melbourne Ann Moorfield aliunganisha matukio:

Elizabeth Donoghue alichukua picha yenye kichwa cha habari “kutoka katika njia ambayo watu wengi wanaielezea kama mtego wa kifo, njia ambayo nimeikwepa hadi leo. Uendeshaji huu wa kutisha ulistahili!”. Aliposti miezi miwili baada ya moto kutokea huko Flickr:

Sasa kika mtu anafaham kuwa nchi hii iliyokuwa imeungua sana hapo Februari haikuharibika moja kwa moja ila inafanya vile nguvu ya asili ilitaka na sasa inajihuisha kama nguvu ya asili ilivyotaka, ngoja nikuoneshe maeneo ya kuvutia. Inakupa wazo la ukubwa wa janga la moto na pia inakuonesha mikunjo na mirindimo ya ardhi chini ya uwanda na nyika. Nimepiga Picha hii katika barabara ambayo wengi huielezea kama mtego wa kifo, barabara ambayo nimekuwa nikiikwepa mara zote mpaka sasa. Lakini uendeshaji huu hatari ulistahili!

Hatimaye, Adrian Cutts aliangazia ukuaji wa mitandao ya kijamii tangu siku ya Jumamosi Nyeusi:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.