- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwanini Serikali za Afrika Zinapinga na Uhuru wa Vyombo vya Habari na Kutoa Maoni? Inawezekana Sababu ni Nguvu Kubwa Nyuma Yake

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ethiopia, Naijeria, Tanzania, Uganda, Zambia, Censorship, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Sheria, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, GV Utetezi
    Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Haromaya nchini Ethiopia wakionesha alama ya kupinga serikali. Picha imeenea kwenye mitandao ya kijamii.

Hali ya hewa  ya mihadhara ya wazi na upinzani katika barani Afrika kudhohofika hatua kwa hatua, ambapo  mara kwa mara imekuwa ikifungiwa. Kisheria name kimasharti ya kiuchumi, gharama ya kuzungumza imepanda barani humo.

Wakati huohuo serikali nyingi zikisemekana kuwa ni zile za kidemokrasia ambazo hufanya chaguzi zake kupitia mfumo wa vyama vingi na ushirikishaji wa mawazo zimekuwa zikifanya kazi kwa udikteta huku zikitoa viashiria vya kuongeza nguvu kwa kadri siku zinavyosonga mbele.

Cameroon [1], Tanzania [2], Uganda [3], Ethiopia [4], Nigeria [5], na Benin [6] zikishuhudia kufungwa kwa mitandao, kuanzishwa kwa Kodi kwa wanablogu na watumiaji wa mitandao ya Kiwami sambamba na kukamatwa kwa waandishi wa habari. Wafanyakazi wa vyombo vya habari wakifungwa kwa madai ya kuchapisha makala yaliyoandikwa taarifa za uongo ambayo hupelekea kuvujishwa kwa siri za serikali au matukio ya ugaidi.

Siku chache zilizopita kulifanyika mhadhara kujadili uhuru wa mitandao huko Accra, Ghana ukienda kwa jina la Forum of Internet Freedom in Africa (FIFA), ambapo kundi la wakilishi waliotokea nchi tofauti tofauti barani Afrika walisema wanaogopa kuwa huenda ikawa serikali za kiafrika zina mpango wa kudhibiti teknologia ya kiganjani ili kuweza kuwaangalia wananchi wake kwa ukaribu zaidi.

Nchi nyingi zina amri na sheria ambazo zinatetea haki ya uhuru wa kuongea. Nigeria, ikitajwa kama mfano, kipengele cha Uhuru wa Habari kinatetea haki ya wananchi kudai taarifa kutoka kwa shirika lolote la kiserikali. Sehemu ya 22 kwenye katiba ya mwaka 1999 [7] inatoa uhuru kwa vyombo vya habari na Sehemu ya 39 ikitilia mkazo kwamba “kila mtu ana haki ya kuongea, ikiwem uhuru wa kushikilia na kupokea taarifa na kutoa mawazo na taarifa bila kuingiliana …”

Bado, Nigeria iliweka sheria nyingine ambazo zilitoa mamlaka ya kukana sheria zilizotajwa hapo awali.

Sehemu ya 24 ya Kipengele cha Uhalifu wa Mitandaoni nchini Nigeria kinasema “yeyote anayesambaza arafa za kwenye mitandao anafanya makosa, kwa kusudi la kusababisha udhalikishaji, kutoelewana, hatari, vizuizi, matusi, kujeruhi, hofu ya jinai, uadui, chuki, kwa dhumuni la kudhoofisha au wasiwasi isiyotakiwa kwa mwingine au kupelekea tu kufikishwa kwa ujumbe husika.”

Huku zikiuundwa sheria zenye kuleta wasiwasi zikipewa misemo ya vitisho katikati yake kana kwamba kuongea kwa watu kutaleta usumbufu au chuki. Serikali na mawakala wao wakitumia hili kufunika haki ya uhuru wa kuongea.

Nani anaweza kuamua ufafanuzi wa chuki? Lazima viongozi wa umma wategemee kuliendeleza hili? Ukiangalia katika sehemu nyingi za dunia, wananchi wana haki ya kukosoa viongozi wa umma. Kwa nini waafrika hawana haki hiyo ikiwa kama sehemu muhimu kwenye uhuru wa kuongea?

Mwaka 2017 na 2016, Wanahabari nchini Nigeria na wanablogu Abubakar Sidiq Usman [8] na Kemi Olunloyo [9] waliwekwa ndani kwa tuhuma za uhalifu wa mtandao kufuatia sheria za kitengo cha Uhalifu wa mitandaoni.

Usiteseke katika hali ya ukimya — endelea kuongea

Kuwepo kwa changamoto hizi za kisheria kunawaambia wananchi kwamba sauti zao zinaleta tija. Kutoka kuzuiliwa usambazaji wa taarifa za “uongo, udanganyifu, kupotosha au zisizo na usahihi” taarifa kuhusu kodi ta mtandao nchini Uganda zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo imelenga kupuuza “uvula”, kelele zilizopigwa kwenye majukwaa mbalimbali mitandaoni zinawaogopesha serikali zinazofanya ukandamizaji, hali inaweza kupelekea kuacha vitendo hivi vya ukandamizaji.

Kwa uzoefu wa wanablogu wa Ethiopia maarufu kama wanablogu wa Zone9 nchini Ethiopia [10] wanatoa mfano huu hapa wenye nguvu kwelikweli.

Mnamo mwaka 2014, waandishi tisa wananchi wa Ethiopia walifungwa jela na kuteswa kwa sababu ya kushiriki kwao kwenye mradi wa blogu ambapo waliandika kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliokua ukifanywa na serikali iliyopita nchini humo Ethiopia, kuthubutu kwao kuandika ukweli uliowahusu wenye nguvu. Serikali ikawaita magaidi kwa kitendo hicho na kuwafunga kwa muda uliopata miezi kumi na nane.

Wanachama wa Zone9 Mahlet (kushoto) na Zelalem (kulia) wakifurahia kuachiwa huru kwa Befeqadu Hailu (wa pili kutoka kulia, mwenye kitambaa shingoni) mwezi Oktoba 2015. Picha umewekwa kwenye mtandao wa Twita na Zelalem Kiberet.

Sita kati yao kwa sasa ni wanachama wa kikundi huru waliofanya makutano yao kama mawaziri wa kimataifa nchini Ghana wakati wa mkutano wa FIFA: Atnaf Berhane, Befeqadu Hailu Techane, Zelalem Kibret, Natnael Feleke Aberra, na Abel Wabella were all in attendance. Jomanex Kasaye, ambaye alifanya kazi na kikundi hapo awali hadi kufikia wakati ambapo wenzake wote walipokamatwa ( lakini yeye hakukamatwa) nae alipata wasaha wa kuhudhuria.

Wanachama mbalimbali walitoa ushirikiano kwa Global Voices kuandika na kutafsiri hadithi Kiamhari.Kama wanachama wa jumuiya Global Voices nayo ilifanya kampeni sambamba na kuhamasisha jumuiya ya haki za binadamu kiduni kwanzia usiku wa kwanza walipokamatwa  [11].

Baada miezi kadhaa kupita huku tukienaandika simulizi zilizowalenga kukuza kesi ya waandishi hao waliokuwa wamekamatwa kupitia mtandao waTwitter, hukumu ya kimataifa kufuatia kutekamatwa kwa waandishi hawa na mkakati wa kuachiwa ulianza kufuata mkondo kutoka serikalini huku viongozi maarufu wa haki za binadamu wakisaidizana na maelfu ya watu waliotoa ushirikiano kwenye mtandao. Pande zote kuu nne za dunia ziliangua kilio kikubwa kuwataka serikali ya Ethiopia iwaweke huru waandishi hao waliofahamika kama Zone9 bloggers.

Tukiwanukuu kwa maneno yao waliplutana kwenye FIFA, wanablogu hao wanasema uanachama wao kwenye jumuiya ya Global Voices ndio ulikuwa ufunguo uliopelekea wao kuonekana wakati walipokuwa wamekamatwa. Kwenye kikao cha jopo, n their panel session, walitoa shukurani zao kwa kutambua mchango wa kampeni zilizofanywa na Global Voices kuwaweka hai.

Berhan Taye, msimamizi wa jopo aliwataka wanakikundi hao waliokamatwa kuelezea baadhi ya mambo waliokutana nayo walipokua wamekamatwa. Na walipoanza kueleza taa zilizokua zikiwaka jukwaani zilizimwa. Hivyo sauti zao zenye nguvu zilitanda ukumbini.

Abel Wabella, aliyewai kuwa kiongozi wa wa tovuti ya Kiamhari, alipoteza uwezo wa sikio lake moja kusikia ikiwa ni baada ya kustahimili mateso makali alipokataa kusaini ukiri wa uongo.

Atnaf Berhane akikumbuka moja kati ya mateso aliyopata mpaka saa nane ya usiku na kuendelea baada ya kupewa masaa machache kulala.

Moja kati ya mawakala waliomkamata Zelalem Kibret aliwai kuwa mwanafunzi wake katika chuo alichofundisha.

Jomanex Kasaye alielezea uchungu wa akili alioupata kuondoka Ethiopia kabla marafiki hawajakamatwa — maumivu ya udhaifu — hali ya sintofahamu  na hofu ya marafiki zake kupoteza maisha.

Wanablogu wa Zone9 wakiwa pamoja jijini Addis Ababa, 2012. Kutoka kushoto: Endalk, Soleyana, Natnael, Abel, Befeqadu, Mahlet, Zelalem, Atnaf, Jomanex. Picha ya Endalk Chala.

Kwa ujasiri, wanablogu wa Zone 9 walisema: “Sisi si watu imara au majasiri…tunachofurahia ni kuwapa watu matumiani.”

Bado, waandishi hao walirejea kwenye maana halisi ya uzalendo kwa maneno na matendo yao. Inabidi kuzama kwenye ujasiri mkubwa mtu kufikia hatua ya kuipenda nchi yake kwa dhati hata baada ya kupitia maumivu kwa mikono yake ya kuzungumza nje.

Mwandishi wa habari kutoka nchini Uganda Charles Onyango-Obbo, alikua miongoni mwa waliohudhuria mhadhara huo wa FIFA, akiwaambia wengine methali maarufu inayojulikana kwa asili ya Igbo iliyokuzwa umaarufu na mwandishi mmoja wa Nigeria  Chinua Achebe isemayo:

Tanguia pale mwindaji alipojifunza kulenga bila kukosea, na ndege pia amejifunza kuruka bila kutua.

Akimaanisha, ili kurudisha uhuru wa mitandao mahali pake, wanaojihusisha na hili lazima watumie mbinu mpya za kijuhami.

Wanaharakati walio mstari wa mbele kutetea hili kwenye nchi za chini ya Jwangwa la Sahara Afrika na nyinginezo duniani hawawezi kustahimili kufanya kazi chini chini au bila sauti wakiwa wamechanganyikiwa na kushindwa. Tukileta pamoja nguvu zetu kwa umoja, hii mihadhara ya wazi, na uhuru wa mitandao vitachiwa huru kupanua wigo wa demokrasia kupitia mitetemo mahiri.