Wahalifu na Vita vya Kibiashara: Ni Mexico ya Aina Gani Inayomsubiri Rais Mpya?

Taarifa kutoka kwenye picha zimetengenezwa na Pictoline. Namba zinamaanisha idadi ya wanasiasa waliouawa katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi. “Mexico ipo katika kipindi cha vurugu za mchakato wa uchaguzi katika miaka ya hivi karibuni na takwimu ni za kutisha”. Picha imetumika kwa ruhusa.

Hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wetu wa uchaguzi wa Mexico unaofanyika hapo Julai 1, 2018. Katika chapisho la awali tumeangalia historia ya Demokrasia ya Mexico baada ya miaka 70 ya chama tawala. Sehemu ya pili tuliangalia kwa ufupi kila mgombea kati ya wagombea wanne wa urais. Katika chapisho hili la sasa, tunaangalia mitazamo ya kura za maoni na hali ya nchi kwa ujumla.

Kura za maoni zinasemaje?

Kufuatia midahalo mitatu iliyoandaliwa na mamlaka rasmi za uchaguzi, zimebaki angalau wiki mbili Mexico iingie katika sanduku la kura. Watafiti wa masuala ya uchaguzi (Consulta MitofskyB&LGCE kwa kuwataja wachache) na wachambuzi wa uwiano katika upigaji kura (Oraculus) wote walimtambua kiongozi sawia. Mara kwa mara wote waliripoti kuwa Andrés M. López ndiye alikuwa akiongoza akikaribia asilimia 50% kwa kura zilizohesabiwa, akifuatiwa lakini sio kwa karibu na Ricardo Anaya.

Kama tulivyojadiliana katika sehemu ya mwisho ya mfululizo huu, Andrés M. López aliwekwa kugombea tena na chama alichokiunda mwenyewe (Movimiento Regeneración Nacional – MORENA) baada ya hapo nyuma kujaribu mara mbili na kushindwa.

Kama ilivyonukuliwa katika sehemu ya kwanza, Mexico imekuwa ikiathiriwa na mgogoro wa kivita tangu 2006 pale Rais wa wakati huo Felipe Calderón alipotangaza ‘vita’ dhidi ya uhalifu. Tangu hapo vurugu zimeongezeka zaidi. Hakuna makubaliano ya kuweka silaha chini wala kusimamisha mapigano hata katika kipindi cha uchaguzi.

Katika muktadha huu, wanasiasa 112 wameshauawa katika vinyang'anyiro vya chaguzi hizi, kama kielelezo hiki cha Pictoline kinavyoonesha:

Picha kutoka Tweeter: wanasiasa 112 wameshauawa nchini Mexico tangu kipindi cha uchaguzi kimeanza; 42 walikuwa wagombea au watu waliokuwa wanapendwa kugombea nafasi fulani, idadi kubwa ya mauaji imefanyika huko Guerrero, Oaxaca, Puebla, Veracruz, na jimbo la Mexico.

Tweet iliyofuata: Mexico inapitia kipindi cha vurugu za uchaguzi katika miaka ya hivi karibuni. Na idadi ni ya kutisha.

“Tunauhakika kuwa wahalifu watashinda”

Kulingana na mwanaharakati Orlando Camacho:

La violencia es lamentable, es un reflejo de la debilidad institucional; estas elecciones están siendo la radiografía exacta de la realidad del país en materia de violencia.

Vurugu ni mbaya, inaakisi udhahifu wa taasisi; chaguzi hizi ni picha halisi ya uhalisia wa vurugu nchini.

Profesa Jesús Silva-Herzog aliandika:

Hace unas semanas Eduardo Guerrero anunciaba en su artículo de El financiero al seguro ganador de las elecciones del 2018. No hacía proyecciones con los datos que arrojan las encuestas. No se refería a la elección presidencial. Hablaba de las organizaciones criminales que, sin aparecer formalmente en la boleta, están decidiendo la elección. Podemos estar seguros de que ganarán los criminales, adelantaba el experto en seguridad. Ganarán porque están eliminando a sus enemigos y porque han sometido a quienes ocuparán puestos en las alcaldías que son vitales para sus intereses.

Wiki chache zilizopita Eduardo Guerrero alimtaja mshindi kwa hakika katika uchaguzi wa 2018 katika makala yake ya El Financiero. Hakutoa makadirio kupitia takwimu zilizochukuliwa na mamlaka za uchaguzi. Hakumaanisha uchaguzi wa urais. Alikuwa akizungumzia vikundi vya uhalifu ambavyo bila hata kupiga kura huamua uchaguzi. Tuna uhakika kuwa vikundi vya uhalifu vitashinda, mtaalam wa masuala ya ulinzi alisema. Watashinda kwa sababu ya kuwaondoa maadui zao na kwa sababu wanawahodhi wale watakaoshikilia nafasi hizo katika mamlaka za miji ambapo ni muhimu kwa maslahi yao.

Alihitimisha:

Hoy en México no se accede al poder mediante las armas pero se define el acceso al poder mediante las armas.

Leo ndani ya Mexico mtu hapati mamlaka kwa silaha lakini anahodhi njia ya kupata mamlaka kwa silaha

Sio kwamba hali ya vurugu nchini kwa ujumla haijaonwa na vyanzo vya habari vya kimataifa kama El País ambacho kiliripoti kuwa wagombea wawili wa Oaxaca na Puebla (Kusini mwa Mexico) waliuawa ndani ya kipindi cha saa 24.

Makubaliano ya kibiashara au ni vita vya biashara?

Wakati haya yakitokea, Mexico ipo tena katika mchakato wa makubaliano ya Mkataba wa Biashara Huria kwa Amerika ya Kaskazini (NAFTA; TLCAN kwa Kihispania) na wabia wake wa biashara na majirani zake wa kanda Marekani na Canada.

Majadiliano hayo yanafanyika yakifuatiwa na ahadi za kampeni za mgombea wa Marekani Donald Trump aliyewahakikishia wale wanaomuunga mkono kuwa atafanya mabadiliko ambayo yatainufaisha nchi yake.

Rais Trump alisema kuwa Mexico wananufaika na NAFTA isivyohaki na alitoa lugha chafu dhidi ya wahamiaji. Mfano wa hivi karibuni ni pale alipowaita “wanyama” watu wanaowasili nchini Marekani kupitia mpaka wa Mexico.

Hata hivyo, tukirudi katika masuala ya uchumi, hali ya biashara kwa Mexico imekuwa ngumu kutokana na Marekani kuweka kodi na ushuru kwa bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi, kwa amri ya Trump ambapo imesababisha Mexico kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

Baadhi ya vyanzo vya habari ndani ya Mexico, miongoni vikiwemo SinEmbargo, vimeielezea hali hiyo kama “vita ya kibiashara”.

Fuatilia sehemu nyingine ya mfululizo ujao, ambapo tutaangalia uchaguzi wa Urais nchini Mexico katika mtazamo wa uhuru wa vyombo vya habari na tutajadili kuhusu majibizano makali yaliyofanyika katika mitandao ya kijamii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.