Waziri Mkuu wa Zamani wa Pakistan Nawaz Sharif na Binti Yake Anarudi Pakistani Akikabiliwa na Hukumu ya rushwa

Waziri Mkuu Zamni wa Pakistan Mian Muhammad Nawaz Sharif akiwa Umoja wa Matiafia tarehe 27 Septemba 2015. Picha kutoka Flickr na Wanawake Umoja wa Mataifa. CC: BY-NC-ND 2.0

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Mian Muhammad Nawaz Sharif anatarajia kurudi pakistan akitokea Uingereza baada ya mahakama ya uwajibikaji ya Pakistan kumhukumu miaka kumi jera kwa kumiliki mali Uingereza zisizo halali.

Binti yake Sharif Maryam Nawaz alitangaza mjini London, Uingereza kuwa yeye na baba yake waturudi Islamabad, Pakistan tarehe 13 Julai 2018 wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu Pakistan wa tarehe 25 Julai. Wanatarajia kukata rufaa dhidi ya hukumu ya rushwa ya siku ya Ijumaa, tarehe 6 Julai.

Sharif na binti yake wamekuwa mjini London kumhudumia mke wake Kulsoom Nawaz ambaye anapata matibabu ya kansa na yuko mahututi.

Katika kesi iliyojulikana kama kumbukumbuku ya Avenfield chini ya wakala wa kuzuia rushwa Pakistan ofisi ya uwajibikaji ya taifa , Sharif alishtakiwa kununua vyumba mjini London kwa fedha aliyochukua kwa udanganyifu nchini Pakistani. Alihukumiwa jumla ya miaka 11 jera na faini ya paundi za Uingereza milioni 8 (sawa na rupia bilioni 1.3 ya Pakistan).

Binti yake Maryam alihukumiwa miaka minane na faini na faini ya paundi ya Uingereza milioni 2 (sawa na milioni 335 Rupia ya Pakistan). Pia, mme wake kapteni (Rtd) Safdar alihukumiwa mwaka mmoja jera.

Safdar alijisalimisha kwenye Ofisi ya uwajibikaji ya Taifa Islamabad tarehe 9 Julai:

Kaptein Safdar alikamatwa Rawalpindi wakati Imran Khan akihutubia maandamano Haripur na kumuonya Nawaz Sharif kwamba asijifanye kuwa Nelson Mandela. Nawaz Sharif na Maryam N. Sharif wanategemea kurudi ili kukakamatwa. Kuna wingu baya lililopo juu ya uchaguzi huu.

Mohammad Taqi ambaye ni mwandishi wa habari anapendekezakwamba kesi ile dhidi ya Sharif ilikuwa njia ya mahakama kuu ya Pakistan ” kumrudikia kesi dhidi yake” kwa kuunganisha hukumu na sakata la Panama ambapo “watoto wake walitajwa kuvujisha habari.” Taqi alieleza:

Kesi hii ilikuwa ni ahueni kwa jeshi lililosaidiwa na kutolewa kwa kile kilichojulikana nyaraka za Panama . Watoto wa waziri mkuu wa zamani walitajwa katika taarifa iliyovujishwa ya umiliki wa makampuni ya pwani ya biashara na mali, lakini yeye hakutajwa. Mahakama kuu ya Pakistani iliweka kando mchakato na yenyewe kubadilisha na kuanzia suala la nyaraka za panama dhidi ya Sharifa.

Pamoja na kufanya uchunguzi makini, lakini mahakama kuu ya Pakistan haikupata ushahidi wowote wa kufanya makosa lakini Sharif alihukumiwa kwa kosa dogo la kutotaja mapato yake. Hata hivyo Mahakama kuu– ilifanya kila liwezekanalo kupata ishara kutoka jeshini — Kilichofanyika ni kuongeza staha ya kisheria dhidi ya Sharif. Mwaka mmoja uliopita, mahakama kuu ilimtangaza kuwa na hatia ya kutokuwa mwaminifu na kushindwa kuendelea kuwa katika ofisi ya umma.

Kufuatia hukumu ya mahakama kuu mwezi Julai 2017, Sharif alilazimishwa kuondoka katika ofisi ya waziri mkuu. Maryam na Safdar waliondolewa uhalali wa kugombea katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Julai 2018.

Je ni kuunga mkono au kukosoa hukumu?

Wengi wanaona kesi na hukumu iliyotolewa hivi karibuni juu ya familia ya Sharif kama mpango wa kisiasa kuwazuia wanafamilia hiyo kugombea katika uchaguzi ujao. Akina Sharif ni wajumbe wa udhamini wa waislam Pakistan (PML-N) na wengi wanategemea binti Maryam Sharif kufuata nyayo za baba yake:

Rais wa zamani wa chama cha SC Bar Ali Ahmad Kurd anasema kila mmoja anajua jinsi Nawaz Sharrif alivyoondolewa na kuhukumiwa pamoja na Maryam N.Sharif. Wabunifu wa kuanzisha na kutekeleza haya ni lazima waache kuchezea hatima ya taifa, kama uchaguzi umegeuka kuwa ubaguzi, watu hawatakubali.

PML-N imeteua mgombea ambaye ni mbadala wa Maryam Nawaz katika uchaguzi

Sasa hivi vyumba vya Avenfield vinne katika mji London vilichukuliwa na serikali ya shirikisho la Pakistan. Wafuasi wa chama pinzani cha siasa Pakistan Tehreek-e-Insaaf (PTI) walikusanyika nje ya Avenfield katika kuunga mkono hukumu.

Mwanaharakati wa mitandao ya kijamii Hamza Khan alitwiiti:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.