Wanaharakati Dhidi ya Rushwa Nchini Urusi Wafungwa kwa “Kuchochea Maandamano” kwa Walichokiandika kwenye Mtandao wa Twita

Kikosi cha polisi wakiwazuia waandamanaji hapo Mei 5, 2018 mjini Moscow // DonSimon, CC0

Wanaharakati wa kupinga rushwa walioandamana wakipings kuapishwa kwa Vladimir Putin kwa mara ya nne kama rais wameona machapisho yao waliyotuma na yale ya watu wengine walioshirikisha katika mtandao yakitumiwa na mamlaka kama ushahidi dhidi yao kwa kuchochea usumbufu kwa umma. 

Hapo Mei 5, Shirika la kupambana na Rushwa (FBK), likiwa ndio chama cha upinzani kinachoongoza nchini Urusi, kiliandaa maandamano nchini kote wakitumia kauli mbiu moja ya “yeye sio Tzar kwetu.”  Maandamano hayo yalikutana na upinzani mkali kutoka kwa polisi na vikundi vinavyomuunga mkono Putin .

Ndani ya Moscow, maandamano katika viwanja vya Pushkinskaya yalishambuliwa na wanaume waliokuwa wamevaa sare za waCossack (ambao serikali huwatumia mara nyingi kama kikosi cha wanajeshi cha kuwabughudhi wapinzani wakati wakiepuka lawama za polisi  kujihusisha moja kwa moja,) pia kama mgambo na polisi wa kuzuia ghasia. Mamia ya watu walijeruhiwa wakiwemo wanahabari wapatao 25 na watu zaidi ya 1600 waliwekwa kizuizini.

Mamia kadhaa ya washiriki walipelekwa mahakamani kwa “Kushiriki katika maandamano yaliyozuiliwa” au “kubishana na polisi.” Kiongozi ws FBK Alexey Navalny, ambaye alikamatwa katika maandamano ya Moscow alihukumiwa kwenda gerezani kwa siku 30 kwa “kurudia rudia kuvunja usalama wa umma.”

Ukamataji zaidi ulikuja baada ya Mei 5. Kwa majuma yaliyofuata waandaaji na wanaharakati 28 wa FBK kwa ujumla waliwekwa kizuizini, wakishtakiwa kwa makosa ya kuchochea maandamano kulingana na machapisho yao katika mitandao ya tweeter,  kulingana na mwanasheria wa shirika, Ivan Zhdanov — ambaye naye alikamatwa Mei 24. Wakati baadhi yao walipigwa faini na kuachiliwa, wengine walifungwa siku 30 ambapo ni vifungo virefu zaidi katika sheria ya makosa madogo ya Urusi.

Leonid Volkov, ambaye ni meneja wa kampeni siku nyingi wa Navalny alisema:

Ivan Zhdanov amekamatwa nje ya ofisi yetu. Atakumbana na kifungu kile kile cha 20.2 [“kuvunja taratibu zilizowekwa katika kuandaa mikutano, maandamano au migomo” cha uvunjifu wa sheria za utawala za Urusi] (lakini hii ni mara yake ya kwanza kwa hiyo atafungwa siku 10 tu na sio 30), hivyo hii tena inakuwa ni “kuandaa maandamano kwa njia ya kushirikisha machapisho ya tweeter” Inaonyesha kuwa kipindi hiki wanamfunga kila mtu.

Elena Malakhovskaya, Mtangazaji wa habari wa Navalny LIVE, ambayo ni chaneli ya FBK huko YouTube alikamatwa karibu na nyumbani kwake kwa kurusha maandamano ya Mei 5 katika chaneli au ” kuandaa maandamo yasiyo na kibali,” kulingana na polisi.

Mtangazaji wa habari @elmalakhovskaya amekamatwa karibu na nyumbani kwake.

Katika kesi nyingine, ushahidi wa kuwatia hatiani baadhi ya wanaharakati wa FBK ulikuwa ni machapisho yao huko tweeter au kushirikisha machapisho ya watu wengine. Kwa mfano, Kira Yarmysh, afisa habari wa Navalny alihukumiwa siki 25 gerezani kwa sababu ya ujumbe ufuatao:

Hatukuwapigia kura hao waliopo madarakani. Kutoka na kuandamana hapo Mei 5 ni sawa na kujiambia wewe na wale wanaokuzunguka kuwa: Siafikiani na yale yanayotokea. Kwa kuwa tumenyimwa haki yetu ya kuchagua, njia pekee ya kufanya sauti zetu zisikike ni hii:  https://t.co/2k3nFrTs1S

Chapisho hili la Yarmysh liliunganishwa na video kutoka chaneli ya Youtube ya Navalny iliyokuwa ikihamasisha maandamano ya Mei 5. Video hiyo imejikusanyia zaidi ya waangaliaji zaidi ya milioni 3 kwa wakati alipobandika chapisho hilo.

Mtangazaji mwingine wa Navalny LIVE Ruslan Shavetdinov, alifungwa gerezani siku 30 kutokana na kushirikisha ujumbe huo huo wa chapisho la tweeter ingawa alikuwa mmoja wa maelfu ya watu waliofanya hivyo.

  1. Makundi ya Haki za Binadamu yanasema kuwa hii ni moja ya mwenendo mkubwa ambapo Warusi zaidi na zaidi wanafungwa kutokana na shughuli zao za mitandaoni. . Agora, taasisi ya kisheria inayotoa huduma za kisheria bure kwa watuhumiwa katika makosa kama hayo wanasema idadi ya watuhumiwa kutokana na machapisho mitandaoni au kushirikisha machapisho katika mitandao ya jamii nchini Urusi inaongezeka kwa kasi sana. Kulingana na taarifa yao ya hivi karibuni, mwaka 2017 kwa kila siku nane mtumiaji mmoja wa mtandao huko Urusi alikuwa akipelekwa gerezani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.