- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwandishi wa Habari Mlebanoni Pamoja na Kutokuwepo Ahukumiwa Kifungo, ‘Kwa kumkashifu’ Waziri wa Mambo ya Kigeni kupitia Facebook

Mada za Habari: Lebanon, Censorship, Haki za Binadamu, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi

Picha ya Fidaa Itani aliyopigwa kutoka kwenye ukarasa wake wa Facebook. Picha na Wassim Naboulsi

Mwandishi wa habari m-Lebanoni pamoja na kutokuwepo alihukumiwa kwa kumkushifu kaimu waziri wa mambo ya nje na uhamiaji Gebran Bassil [1] kupitia ujumbe wa Facebook.

Tarehe 29 Juni, 2018 mahakama ya mji wa Baada uliopo magharibi mwa Lebanon ilimuhukumu Fidaa Itani miezi minne jera na faini ya milion 10 fedha ya Lebanon (Kama dola 6660 za kimarekani).

Fidaa Itani ni mwandishi wa habari ambaye huandika habari za Syria na mgogoro wa wakimbizi.

Ujumbe wa swali kupitia Facebook ulitoa tahakiki nzito ya matendo ya kisiasa na jeshi yanayofanywa na watendaji wakuu wa serikali nchini Lebanon. Itani alilaumu uvamizi uliofanywa mwaka jana na jeshi la Lebanon katika eneo la Arsal ambao ulisababisha vifo vya wasiria waliokuwa kizuizini. [2] Pia alikosoa msukumo wa kitaifa unaondelea wa kulazimisha kuondolewa kwa wakimbizi katika taifa la Lebanon.

Itani aliendelea kuelezea kuhusu chama cha siasa cha Lebanon na kundi la kijeshi la Hezbollah [3]. Itani amepinga waziwazi jeshi la Hezbollah kuingilia Syria [4] kwa niaba ya utawala wa Assad.

Muda mfupi tu baada ya ujumbe huo, wanasheria wa jeshi na Rais walifungua kesi dhidi ya Itani. Zaidi ya hapo alianza kupata vitisho kutoka kwa watu wenye uhusiano na Hezibollah. Muda mfupi baadaye, alikimbia nchi na kuomba hifadhi katika Nchi ya Uingereza.
Katika mahojiano na gazeti la Francophone la Lebanon L'Orient le Jour, Itani alieleza [5]kwamba shitaka lake kwanza lililofunguliwa na wanasheria waliodai kuwakilisha Rais na jeshi linaonekana kutoweka na nafasi yake imechukuliwa na kesi iliyofunguliwa na Gebran Bassil.

Je ne sais pas comment la première action judiciaire a disparu, ni ce qui a été concocté dans ce cadre entre les services de renseignements de l’armée et le président de la République, ou encore le Hezbollah (également visé par le post, et dont les intimidations contre M. Itani sont derrière son départ pour Londres, NDLR). Il semble toutefois que Gebran Bassil se soit porté volontaire pour intenter une action à leur place.

Sijui jinsi hatua ya kwanza ya kishera ilivyopotea wala kilichokuwa kimetengenezwa na vyombo vya jeshi na Rais, au hata Hezbollah katika kesi ile. Ingawa inaonekana kwamba Gebran bassil alijitolea kuanzisha hatua ile badala yao.

Pia Itani alisema [6] kwamba alikuwa hajapokea uthibitisho rasmi wa hukumu isipokuwa amesikia taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari. Pia aliiambia shilika la Maharat la uhuru wa habari [6], ambalo ni asasi isio ya serikali kwamba kaimu waziri ndugu bassil pamoja na hii amefungua kesi tisa dhidi yake.

Akijibu kupitia Facebook [7] na Twitter, Fidaa Itani hakushangaa maamuzi ya jaji. Akichangia juu ya hukumu yake ya kifungo, alitoa maoni kuwa: “zaidi ni unyanyasaji na unyang’anyi .”

Hukumu ya Itan iliripotiwa, kukosolewa na kushutumiwa na baadhi ya walebanon na mashirika ya kimataifa.

Katika barua pepe iliyotumwa kwa waandishi wa habari na Bassam Khawaja ambaye ni mtafiti wa haki za binadamu Lebanon, alisema:

Kumhukumu mwandishi wa habari miezi jela kwa ujumbe wa Facebook ni shambulio la kikatili kwa uhuru wa kutoa maoni ambalo linaonesha kulinda uhuru wa kutoa mawazo katika Lebanon hakupo. Bunge jipya la Lebanon linatakiwa liondoe haraka sheria ambazo zinafanya kukashifu kuwa jinai na ambazo haziendani, hazifai na zinakiuka sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

Kwa kweli , kanuni ya adhabu ya Lebanon [8] inafanya kukashifu kuwa kosa la jinai na masharti maalumu dhidi ya kumtukana Rais, bendera, na viongozi wengine wa umma. Kanuni ya kijeshi nchini inafanya “kutukana bendera au jeshi” kuwa kosa la jinai. Makosa haya adhabu yake ni kifungo au faini na haitoi msamaha maalumu kwa kazi ya uandishi wa habari.

Kutokana na ripoti ya Freedom House ya mwaka 2016 kuhusu Lebanon [9]:

Waandishi wa habari wa Lebanon wanalaumu kwamba sheria za vyombo vya habari zinachanganya, pingana na hazieleweki. Masharti yahusuyo vyombo vya habari ambayo yanathibitisha kushtakiwa kwa mwandishi wa habari, zinapatikana katika kanuni za adhabu, sheria ya uchapishaji, sheria ya mwaka 1994 ya sauti na picha ya vyombo vya habari na kanuni ya haki za kijeshi .

Kupanda kwa wasiwasi juu ya uhuru wa kutoa mawazo Lebanon

Katika mazingira ya sheria Lebanon, kesi dhidi ya waandishi wa habari sio jambo jipya na matukio hayo yameongezeka [8] katika miezi ya hivi karibuni na kuna fununu za mashtaka dhidi ya waandishi wa habari, waongozaji wa vipindi vya luninga na wachambuzi.

Tarehe 24 Januari 2018 muongozaji wa kipindi cha luninga cha ucheshi Hisham Haddad alishitakiwa [10] kwa kufanya mizaha kwa waziri mkuu Saad Hariri na Mfalme Saudi Mohammad Bin Salman.

Mwezi Machi mwaka 2018 mmiliki wa tovuti ya Lebanon Debate [11]alihukumiwa miezi sita jela [12] na aliamuliwa kulipa milioni 10 kwa fedha ya Lebanon baada ya kukutwa na hatia ya kashfa katika kesi iliyofunguliwa na Mkurungenzi Mkuu wa forodha.
Mwezi Novemba 2017, mwongozaji mashuhuri wa kipindi cha Luninga Lebanon Marcel Ghanem alishtakiwa [13]kwa kuzuia haki baada ya kukataa mashitaka dhidi ya wageni wake wawili wote wakiwa ni waandishi wa habari wa saudi ambao walimushtumu Rais wa Lebanon Aoun na waziri Bassil kuwa ni washirika wa ” Hezbollah katika ugaidi.” Kesi dhidi ya Ghanem [14] ilisimamishwa.

Katika habari nyingine iliyoandikwa na L'Orient Le Jour, Marcel Ghanem alilipoti [15] akisema kwamba kukamatwa kwa waandishi wa habari na hukumu zao ilikuwa ni matokeo ya “uhusiano wa karibu sana unaofanywa na mamlaka zinazotawala kwa kujificha kwenye kivuli cha mapambano dhidi ya ugaidi au Israel “.

Lakini waendesha mashtaka wa serikali sio wao tu ambao ni taasisi za kisheria zinazofungua mashtaka ya kutukana na kukashfu dhidi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari. Tarehe 10 mwezi Januari 2018, mahakama ya kijeshi katili ya Lebanon ilimukumu wakati hayupo [16] mwandishi wa habari mlebanon na mtafiti Hanin ghaddar kwa kukashfu jeshi la Lebanon kwenye mkutano uliofanyika Marekani mwaka 2014. Hukumu yake baadaye ilibadilishwa.

Siku kumi baadaye kitengo cha intelijensia jeshini kilimwita mtetezi wa haki za binadamu Ovada Yousef kwa kutuma ujumbe kupitia Facebook. Yousef aliliambia shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch [8] kwamba aliwekwa chini ya ulinzi [17] na jeshi na polisi kwa siku nne.

Taasisi ya Maharat isiyo ya kiserikali ambayo ni chombo cha habari na uhuru wa habari iliomba mamlaka za mahakama [6] kuzingatia uhuru wa maoni ya umma:

تطالب “مهارات” المجلس النيابي الجديد بالتسريع لإقرار الاصلاحات التي تقدمت به مهارات مع النائب غسان مخيبر وأبرزها الغاء عقوبة الحبس ومنع التوقيف الاحتياطي عن كل من يعبر عن رأيه بأي وسيلة ضمنها الانترنت وتوسيع مفهوم نقد الشخص العام.

Pia Maharat iliomba mahakam mpya kuharakisha marekebisho yaliyoletwa na mbunge Ghassan Mukhaiber hasa ya kuondoa hukumu ya jera na kuzuia kuwekwa kizuizini yeyote anayetoa maoni kwa njia yoyote pamoja na mtandao na kupanua maoni ya wananchi.

Muda utaeleza kama mpango wao utaleta mabadiliko halisi katika mazingira ya uhuru wa kutoa maoni.