- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Miongo Minane Chuki Bado Ipo Kati ya Wajordani na Wapalestina

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Jordan, Palestina, Historia, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uhamiaji na Uhamaji

Mwanaume aliyevaa kilemba (kwa mila za wapalestina) akiongea na mwanaume akiwa amevaa kilemba (cha mila ya Kijordan). Picha imetolewa kwa umma na: gazeti la Garaa [1].

Karibu asilimia 70 [2] ya idadi ya watu wa Jordani ni wa asili ya Palestina na kwa ujumla wapalestina hao wameingiliana na jamii za Jordan. Wajordani na Wapalestina wamekuwa wakiishi pamoja tangu vita ya waarabu-waisraeli na palestina Nakba mwaka 1948 [3], na hata kabla ya hapo.

Hata hivyo, ukiongea na wapalestina na Wajordani kila siku, unaweza kupata simulizi za ndani zinazoelezea mgogoro kati ya makundi haya.

Sara Suod anayetokea Madaba, katikati ya Jodan, aliambia Global Voices kwamba wazazi wake walikuwa hawamruhusu kwenda kutembea kwa rafiki zake wakipalestina:

“Ninatokea Madaba, na familia yangu inafurahia sana kuwa [mjordani] . Wanajivuna sana kiasi kwamba walinikataza mimi na dada zangu kutembelea watoto wakipalestina rafiki zetu nyumbani kwao .”

Wakati kuishi pamoja kumejenga amani mingoni mwa makundi haya, lakini amani kamili bado haipo. Ndoa na michezo ni nyanja mbili ambapo bado tunaweza kuona migogoro yao vizuri zaidi.

Je, ndoa kati ya wajordani na wapalestina bado ni mwiko?

Kati ya wanawake 82,000 wa Jordani wameolewa na wageni, na karibu wanawake 53,000 wameolewa na palestina [4]. Idadi kubwa hii ingeonesha ulinganifu wa ndoa za watu wajordani na palestina lakini idadi hiyo nayo inapotosha.

Kutokana na taarifa kutoka kwa raia wa Jordani (awe wa asili ya Jordani au wapalestina) ndoa hizi zinaonesha picha tofauti ya uhusiano wa jamii ya Jordani. Hata kama ndoa sio mwiko kabisa, zinaweza kutofautiana kutegemea eneo na familia — kuna familia zinaona ndoa kama kawaida, nyingine zinichukia na nyingine zinaiona kama haramu. .

Ukianzia na hadithi ya familia ambazo zina amani katika suala la ndoa, taarifa ya Ahmad Khalil ambaye ni mpalestina na mke wake mjordani inaonesha kuwa ndoa yao ilikuwa yenye mafanikio, aliiambia Global Voices kwamba:

Tulikutana chuoni na tukachumbiana baada ya kumaliza masomo yetu. Tangia mwanzo, familia yake na ya kwangu pia zilijua. Hakuna mtu aliyekataa kitu chochote, na mambo yote yalikwenda vizuri katika uchumba. Hakukua na matatizo makubwa yaliyotoke mbali na mgongano wa baaadhi tu ya sheria za kijadi kati ya wakwe na wala haukuhusu tofauti za makabila yetu. Nafikiri ni kwa sababu mama yangu ni mjodani na wajomba zake wameoa wapalestina, kwa hiyo familia yetu yote wamekumbana na hali hiyo.

Ahmad na mke wake wana bahati kuzaliwa katika familia ambayo inamchanganyiko kwa hiyo tatizo la chuki au ubaguzi wa rangi ni dogo kwa kuwa kila mwanafamilia ana asili ya kutoka pande zote mbili.

Hata hivyo sio kila mmoja amekumbwa na hali kama ya Ahmad. Sara Majali ni mwanamke mwenye miaka 26 ambaye anatoka Al-salt katikati mwa magharibi ya Jordan alielezea Global Voices maoni yaliyotolewa na mme wake ambaye ni mpalestina na familia yake kuhusu ndoa yake:

Katika kukua kwangu, familia yangu hawakuwa wakali juu ya ndugu zangu na kuolewa na mpalestina hata nilipowambia nataka kuolewa naye wala hawakujali pia. Waliniambia ni bora nikaolewa na binamu yangu ambaye pia anatokea Al-Salt au angalau yeyote anayetokea hapo. Mwanzoni kabisa mama yangu alikataa nisifunge ndoa hiyo kwa kuniambia nitafute kijana ambaye ni wa ‘ukoo wetu’ lakini baba hakuwa na maoni yoyote.

Mwishoni mama yake alikubaliana na ndoa hiyo.

Mwoshowe mama yangu alikubali niolewe baada ya miezi kadhaa ya kumshawishi, lakini alikuwa bado hajaridhika moyoni kubariki ndoa hiyo. Mimi na mchumba tulipofuatilia zaidi, mara kwa mara maneno yaliyokuwa yanatoka kinywani mwa mama yangu yalikuwa “ingekuwa vizuri kama ungeolewa na….?” na kisha alitamka jina la kijana yeyote aliyezaliwa Salt.

Aliendelea:

Wazazi wa mchumba wangu, ingawa hawakuwa wakali juu ya ndoa hiyo kama alivyokuwa kwa mama yangu lakini walimsumbua. Haliogopa ukweli kuwa ninatoka katika familia kubwa kitu ambacho walifikiri ningetumia kwa mme wangu, kwa kejeli walimshauri atafute yeyote kutoka katika ukoo wao. Tofauti na wake wa shemeji zangu waliokuwa wapalestina ambao walipokelewa haraka na kuwa kama sehemu ya familia— baada ya miaka mitatu ya ndoa, walinielewa vizuri, ingawa nilijihisi kama waliniwekea mipaka katika kuchanyikana nao.

Hadithi ya Sara inaakisi mawazo ya chini kwa chini ambayo yamekuwepo katika jamii za Jordan tangu wapalestina wavyohamia kwa mara kwanza Jordan mwaka 1948—familia za wajordan ni kubwa na wenye nguvu zaidi, wakati zile za wapalestina (kwa kuwa wahamiaji) hazina “msingi.”

Kusema kuwa “hazina msingi” ni namna ya dharau ya kuziambia familia za wapalestina kuwa ni ndogo au hazikuungana vizuri kama zile za wajordan. Hii inamaanisha kuwa mwanaume au mwanamke mjordan anakuwa na nguvu katika udhibiti wa ndoa kwa sababu wana familia na nguvu ya kufanya hivyo.

Ndio maana familia nyingi za kipalestina wanasita kuoana na familia ya Kijordan na familia ya kijordan vivyo hivyo.

Uadui kati ya mashabiki wa mpira wa miguu

Al-Faisaly in moja ya timu mashuhuri sana katika ligi ya mpira wa miguu Jordan na imekuwa ndiyo ishara au nembo ya raia wa Jordan kwa urithi wa Jordan.

Al-wehdat iliyoundwa katika kambi ya pili kwa ukubwa ya wapalestina nayo ni mashuhuri na ni ishara au nembo ya raia wa Jordan kwa urithi wa wapalestina.

Mara nyingi mashabiki huwa na kawaida ya kushaingilia timu hizi zinapokuwa zinacheza na timu nyingine lakini zinapokutana timu hizi kunakuwa na ushabiki wa kutambiana kati ya mashabiki wake..

Kushambuliana [5] ni kawaida na ilifika hatua ambapo mashabiki 250 walijeruhiwa [6]. Maduka na magari yanayomilikiwa na watazamaji mara nyingi huchomwa [6]bila sababu ya msingi isipokuwa ni kuibuka kwa vurugu za uhasama.

Mara nyingi askari polisi na uongozi wa timu hizo mbili [6] huhusishwa ili kujaribu kuwafundisha masahabiki wao adabu kwa kuwafungia kujihusiha na michezo wale wanaoanzisha vurugu [7]—kitu ambacho hakijaonekana wakati timu hizo zikicheza zenyewe na timu nyingine.
Mwaka 2009 leaked US diplomatic cable ilisema kwamba [8]:

Wito wa uzuiaji wa uhuni wa kipalestina na kuwavunjia heshima wapalestina wenye asili ya Malkia na Mfalme ilipelekea kuahirishwa kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya klabu zenye upinzani mkali za Faisal and Wahdat ambapo timu ya Faisal huwakilisha East Banker na Wahdat huwakilisha jamii za kipalestina.

Hitimisho linaweza kufikiwa kuwa ghasia, uchomaji mali za watu kwa makusudi na tabia mbaya ni zaidi ya soka, ni kile ambacho timu hizo zinawakilisha ambacho ni ubaguzi wa rangi. Hoja hii ilitolewa na Raisi wa kipalestina wa timu ya Wehdat katika mahojiano na Ulimwengu wa soka [8]:

Asilimia 99 ya mashabiki wa Wehdat ni wapalestina , huwezi kuona shabiki yeyote wa kijordan wa timu ya Wehdat. .