Kufuatia Shinikizo la Vyombo vya Ulinzi, Fahari ya Beirut kwa Mwaka 2018 “Yaahirishwa kwa Muda”

Bangili ziligawanywa na Fahari ya Beirut. Chanzo: Ukurasa wa Facebook.

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Fahari ya Beirut kwa ushirikiano na makundi mengine yanayounga mkono na kutetea haki za mashoga wameandaa mijadala na matamasha yanayopinga chuki na unyanyapaa wa kijinsia dhidi ya tofauti katika kujamiiana.

Fahari ya Beirut 2018 ilizinduliwa hapo Mei 12 wakati wa mlo wa mchana wakisherehekea “wazazi ambao wamezitunza familia zao, ambao hawakuwatenga watoto wao walipogundulika kuwa wanajihusisha na ngono za jinsia moja au angalau wazazi waliotaka kuziweka familia zao pamoja.”

Lakini mwaka huu, mamlaka ya Ulinzi ya Lebanoni ilizuia kufanyika kwa tamasha moja lililokuwa limepangwa la kusoma tamthilia wakisema kuwa tamasha hilo liliandaliwa kinyume na sheria. Hata hivyo wenye ukumbi href=”https://www.beirutpride.org/arrest2018-en/”> walimhoji Mkuu wa Ulinzi, ambaye kusimamia ‘ udhibiti wa vyombo vya habari‘ ni moja kati ya kazi zake, kuwa kama kusoma tamthilia inahitaji kuhakikiwa na ofisi ya udhibiti. Mkuu wa ulinzi akasema haihitaji.

Tamasha hili lililokatazwa ilikuwa lifanyike katika ukumbi wa Zoukak Beirut. Wajumbe wa kamati ya ulinzi na tawi la polisi la upelelezi waliwasili katika ukumbi huo na kusimamisha utaratibu, uliokuwa umewekwa wa kusoma na kutafsiri bure tamthilia ya Kifaransa ” Zimwi” Yann Verburgh kwa lugha ya Kiarabu.

Muandaaji mmoja wa Fahari ya Beirut Hadi Damien, alikuwa ameshikiliwa kwa usiku mmoja na baada ya shuruti kutoka kwa mkuu wa ulinzi, Fahari ya Beirut waliamua kuahirisha matamasha yao “ kwa muda“.

Damien alishikiliwa usiku wa Mei 14-15 katika kituo cha polisi cha Hobeiche ambacho kinafahamika kwa matukio ya utesaji kama moja ya matukio yaliyoripotiwa huko Lebanoni na gazeti la kila siku la lugha ya Kifaransa L'Orient Le Jour (OLJ), ambapo wapenzi wawili ambao ni mashoga walikamatwa na walitendwa vibaya kwa kuteswa huko Hobeiche na katika vizuizi vingine huko Lebanon.

Kulingana na vyanzo vya polisi vilivyoongea na OLJ, Hadi Damien alishikiliwa kwa amri ya mwendesha mashtaka wa umma wa Lebanoni. Aliamriwa kuchagua kati ya kusaini mkataba kuwa hatajihusisha na matamasha ya Fahari ya Beirut au shauri lake kupelekwa kwa jaji ambae atahojiana naye kwa misingi ya kifungu cha “kujihusisha na kuchochea; na kukiuka maadali ya jamii kwa kuandaa matamasha hayo”.

Kwa ushauri wa mwanasheria wake, Damien aliamua kusaini mkataba huo na muandaaji huyo wa Fahari ya Beirut aliruhusiwa kuondoka katika kituo hicho cha polisi.

Hapo Mei 15, Fahari ya Beirut ilitoa waraka ufuatao:

تمّ إطلاق سراح هادي دميان المشروط وبيروت برايد آمنة. نعلّق في الوقت الرّاهن الفعاليّلات المُدرجة تحت عنوان بيروت برايد حتّى العشرين من أيّار ٢٠١٨. شكرًا لاهتمامكم ولتعاطفكم، ونرجو من الجميع إنتظار بيانًا مفصّلًا عند السّاعة التّاسعة مساءً وعدم إصدار تخمينات غير صحيحة تثير الرّيبة وتضلّل الرّأي العام.

Hakuna mtu yeyote aliye kizuizini kwa sasa, na Fahari ya Beirut ni salama. Matamasha yalikuwa yametangazwa katika mabango ya Fahari ya Beirut hadi Mei 20, 2018, yamefutwa kwa sasa. Tunawashukuru kwa kujali kwenu na ninawaomba mjiepushe na uvumi. Tutatoa taarifa kamili hapo saa tatu usiku kuwaelezea kinachojiri.

Shinikizo kutoka kwenye mamlaka lililaaniwa na mashirika ya kijamii. Fahari ya Lebanon, ambayo hufanya kazi ili “kuwezesha ulinzi, uwezeshwaji, na usawa katika makundi ya pembezoni kupitia kazi za huduma za kijamii”, walilaani kunyamazishwa kwa shughuli zinazofanywa kwa amani, wakiongeza kuwa:

Mara zote Lebanoni inajulikana kwa kuheshimu utofauti na husemwa kuwa ni nchi yenye umoja kwa wananchi wake wote, pamoja na tofauti zao. Lakini kwa miaka kadhaa sasa tumeshuhudia ususiaji wa harakati za mashoga katika kupaza sauti na kuelezea hitaji la uwepo wao katika jamii kulindwa na kupokelewa na kila mmoja.

Mpambano dhidi ya hofu ya ushoga unaoendelea nchini Lebanon

Nchini Lebanon, mahusiano ya jinsia moja yamekatazwa kwa misingi ya “kutokuwa ya kawaida”: kifungu 534 cha adhabu cha Lebanoni kinazuia ushoga “kujamiiana kuwe kulingana na utaratibu wa asili”. Hata hivyo, kati ya 2007 na 2017, majaji wanne waliona kuwa sheria isitumike dhidi ya ngono ya jinsia moja kwa watu wenye umri sawa waliokubaliana.

Lakini hili halijakomesha kuenea kwa unyanyasaji wa serikali ya Lebanoni. Hivi karibuni Shirika la Haki za Binadamu (HRW) liliripoti kuwa wanaume mashoga na wanawake waliobadilisha jinsia nchini Lebanoni wamekuwa wakipigwa kwa nyaya za umeme na kubwakwa kwa kutumia fimbo za vyuma. Shirika la Haki za Binadamu liligundua kuwa wakati makundi ya wanaharakati nchini Lebanoni wakifanikiwa ” kuziaibisha” huduma za polisi Usalama wa Ndani kwa “kuandika kuhusu ukatili na kuweka wazi taarifa za wahanga”, Mkuu wa Ulinzi “amehusishwa kidogo hivyo shinikizo la umma linapata ugumu katika kukabiliana na unyanyasaji wa mashoga unaofanywa na Mkuu huyo wa Ulinzi.”

Moja ya matamasha ya Fahari ya Beirut ya 2017 yalifutwa pia kwa sababu ya vitisho kutoka kwa Kikundi cha Wanazuoni wa Kiislamu (Ulamaa) wa Lebanon (هيئة علماء المسلمين في لبنان). Wanachama wa Kikundi cha Wakristo Waorthodox pia waliombwa “kuomba dhidi ya tishio la ushoga”

Katika tovuti, yake Fahari ya Beirut hujiita “jukwaa shirikishi ambalo huchukua misimamo chanya dhidi ya chuki na unyanyapaa unaolenga utofauti wa jinsia na kujamiiana. […] Baina ya Mei 17, Fahari ya Beirut ilitajwa katika Siku ya Kimataifa Dhidi ya Hofu ya Ushoga na Ubadilishaji Jinsia.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.