Ajentina Yahalalisha Utoaji Mimba

Kikundi cha kitambaa cha kijani kikiwa kwenye jengo la Bunge. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Kampeni ya Kitaifa kwa Haki ya “Utoaji Mimba Salama, wa Kisheria na Huru”, imesambazwa sana mtandaoni.

Mnamo June 13, mkutano wa baraza la wawakilishi nchini Argentina, wakiwemo wasaidizi wao, litafikia tamati ya kupitisha muswada wa kuhalalisha utoaji mimba nchini humo. Mjadala huo ulianza rasmi mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu, kama hatua moja wapo katika harakati za kutatea haki za uzazi kwenye nchi hiyo.

Kwa kipindi cha miezi miwili, baraza la wasaidizi limesikiliza maoni mbalimbali ya waungaji mkno na wapinzani wa suala hilo. Muda wa majailiano ulitoa fursa ya maboresho fulani kwa muswada huo ili kupata kura kutoka kwa wasaidizi ambao bado walikua kimya. Ingawa watu wenye sauti kubwa katika hili  ni madaktari ambao ndio washika silaha mkononi ambao wametoa mtazamo hasi, ingawa  baadhi yao wameliafiki suala hili. Wakishauri kwamba uangalizi wa walezi uwepo kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 16.

Wakati huo huo, mjadala mwingine ulikua ukiendelea katika mitandao ya kijamii kila siku ya Jumanne tangu ilipotimu mwezi Aprili, ambapo mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali ya kutetea haki za binadamu na vikundi vya kujitolea vya kiraia, vilivyoitishwa na Kampeni ya Kitaifa kwa Haki ya “Utoaji Mimba Salama, wa Kisheria na Huru”, vikikutana mbele ya jengo la makutano ya baraza la wawakilishi wakishikilia juu vitambaa vya kijani kama ishara ya kupambana kilizuia swala hilo. Wakiwa na kauli mbiu: “Elimu ya uzazi ni maamuzi, uzazi wa mpango kuzuia utoaji mimba, utoaji mimba halali kuepuka kifo”. Pia kumekua na udadavuaji wa muswada huu ukiongozwa na mashirika ya kidini na vikundi vinavyolipingana na muswada huu. Wote wakiwa na kauli mbiu “Tuokoe maisha ya wote.”

Juni 13, mkesha unatarajiwa kufanyika mbele ya mkutano wa baraza la wasaidizi.  Mawazo ya wengi wameafikiana na muswada huu. Kuthibitisha hilo hata mwandishi wa habari maarufu aliyekuwa akilipinga swala zima la upitishwaji wa muswada huu aliandika ujumbe mfupi kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa hakufurahishwa na matokeo hayo.:

“Piga kura. Unaunga mkono au unapinga utoaji mimba kwa mujibu wa sheria, salama na huru?” [78% wanaunga mkono, 16% wanapinga, 6% hawakuwa na majibu].

Hata hivyo, mchanganuo wa kura za matakwa ya baraza la wawakilishi waliopiga kura unaonesha muelekeo wa kupinga uhalalishwaji. Bado zipo kura nyingi ambazo bado hazieleweki, ingawa hali hii inaweza kuwa inapelekewa na kutotolewa tamko rasmi kutoka baraza la wawakilishi hivyo basi si rahisi kwao kuonyesha msimamo wao uko wapi ili tu kuepuka ushindani na vitisho vinavyoweza kujitokekeza  kwa wakati huu.

Siku ya mwisho ulipofanyika muhadhara halali ilitolewa hotuba nzito na waziri wa Afya  Adolfo Rubinstei iliyounga mkono hoja ya kuondoa sheriai:

Llevamos 35 años de democracia. El aborto es un tema que ha estado escondido bajo la alfombra. […] La evidencia es muy sólida respecto a que la despenalización reduce la mortalidad materna y el número de abortos totales. De alguna manera tenemos que actuar.

Tumekuwa na demokrasia kwa miaka 35. Utoaji mimba limekua ni jambo lililofunikiwa sakafuni  […] Bila ushahidi: kuondoa sheria kutapunguza vifo vya kinamama na idadi ya utoaji mimba. Kwa njia moja, au nyingine, tuchukue hatua.

Ikiwa hapo awali itapitishwa, muswada utafikishwa kwa Bunge la Seneti, ambapo kwa sasa kura nyingi zinapinga uhalalishwaji. Hata hivyo, hali hii inaweza kutokana na matokeo ya mhadhara uliofanywa na baraza la wawakilishi, ambao maamuzi yao ndio muhimu.

“Mimi mtu tu nimeshikilia kitambaa cha kijani hapa mbele ya mjengo”

Sio rahisi kupinga maamuzi ya umma, sio tu kwa kura lakini pia kwa kupitia similizi mbalimbali  binafsi za watu katika mitandao.

Kwenye ushuhuda mmoja, mwanamke huyu bila kutaja majina ya madaktari alieleza adha alizozipata pale alipohijaji kutoa mimba ili kuokoa maisha yake, akieleza namna ambavyo wengne waalikataa kumsaidia wakkitaka kiwango kikubwa cha pesa kwanza:

Mi cabeza y mi cuerpo no habían logrado resetearse y seguían aún con la angustia grabada de aquél momento en el que en vez de recibir la ayuda y contención médica e institucional que necesitaba, me encontré saltando al vacío sin red. Cuando dormía tenía pesadillas con el Dr. N y el Dr. B. […] No puedo dejar de pensar en el médico B. Sobre todo después de verlo en el Congreso argumentando a favor de la vida.

Nikiwa nimeinamisha kichwa bila kujua nianzie wapi. Bado nikiwa mwenye wasiwasi kwa wakati huo, ambapo badala ya kupata msaada ila kunyanyapaliwa kutoka kwa madaktari nilijikuta nikirukia kitandani pasipo na chandarua. Kila nilipolala nilijiwa na ndoto za Dk. N and Dk. B […] bila kumsahau  Dk. B. tena baada ya kumwona pele mjengoni akihoji kuokoa maisha.

Akitoa hitimisho:

Siento que nos estamos jugando mucho en estos días. Algunas amigas me dan valor, como si me dieran la mano, como aquélla vez […] Soy sólo un pañuelo verde más mirando al Congreso y pidiéndole que vote la legalización del aborto.

Nafikiri tumekuwa tukihatarisha vingi nyakati hizi. Baadhi ya marafiki wa kike hunipa nguvu . [huwa ninajihisi kama] wameishikilia mikono yangu , ni kama [wamefanya hivyo] siku ile  […] Mimi ni mtu tu nilieshikilia kitambaacha kijani nimesimama mbele ya mjemgo nikitazama na kuomba wapitishe utoaji mimba.

Huko Twitter, watu wamejitokeza wakiwa na yao mazito kuelezea maoni yao juu ya muswada huu:

Umaja wa Mataifa umefanya kitendo cha utoaji mimba kuwa kosa la jinai kama njia moja wapo ya kuumiza watu. Kama sheria haitapitishwa, wale wanaowajibika na utesaji na hatimaye vifo watakuwa wasaidizi wa wale wanaowaunga mkono. Watalazimika kumbeba kila mwanamke anayepoteza damu mpaka kufa kwa ajili ya dhamira zao. Utoaji mimba upo, iwe kwa mujibu wa sheria au kinyume.

[Kama uisema] “naunga mkono utoaji halai wa mimba kwa waliobakwa , kama sio, wacha wawekwe ndani kwa kuachia miguu yao”, kupitia hili hamjali kuhusu kuokoa maisha [kuokoa] “maisha ya wote” [waliokuwa kinyume na mmuswada huu walisema; mnachotaka ni kuwaadhibu wanawake au sio? utoaji mimba ni hali au usio halali?, hilo ndio swali.

Kama sheria hii itapitishwa , Argentina itakuwa ni nchi ya pili merika ya Kusini kufuata msafara huu wa kupitisha sheria ya uhalalishwaji wa kutoa mimba. Nchi ya kwanza ilikuwa Uruguay mwaka 2012. Ikirekodiwa kuwa na idadi ndogo ya uzazi  ya pili kutoka mwisho ikilinganishwa nanchi nyingine huko Amerika ya Kusini.

Hebu tuwe kama nchi tunazotaka ziwe. Bila rushwa, tumejumuishwa duniani, tukiwa nauchumi mkubwa wenye kuwajibika kwa wahusika wa uchumi mkubwa, uhifadhi ya jamii, majadiliano ya kisiasa…na utoaji mimba kwa mujibu wa sheria.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.