- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wasomaji wa Global Voices wamefuatilia nini juma lililopita?

Mada za Habari: Amerika Kusini, Asia Mashariki, Asia ya Kati, Asia ya Kusini, Marekani ya Kaskazini, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Nchi za Caribiani, Nchi za Visiwani, Ulaya Magharibi, Ulaya Mashariki na Kati, Uandishi wa Habari za Kiraia
[1]

Picha ya mtumiaji wa Flickr Rob McDonald. CC BY 2.0

Hapa Global Voices, wanafamilia wetu hufanya tafiti, kuandika, huhariri, na kutafsiri habari kwa lengo la kuunga mkono haki za binadamu na kutengeneza madaraja ya uelewa baina ya nchi, tamaduni na lugha.

Hatuchapishi habari kwa lengo la kupata watu wanaobofya vichwa vyetu vya habari au kufualia habari mpya. Tunapenda, hata hivyo, tunapenda kufuatilia namna ambayo bidii yetu inawagusa watu duniani.

Mpaka hapo, kipimo kimoja wapo ni namna wasomaji wetu wanavyoitikia habari na tafsiri zetu. Kwa hiyo hebu tuone wasomaji wetu wametoka wapi na kitu gani kiliwagusa katika kipindi cha kati ya Mei 7 -13, 2018.

Wasomaji wa Global Voices wanapatikana wapi?

Juma lililopita, habari na tafsiri zetu ziliwavuta wasomaji kutoka kwenye nchi 207! Nchi 20 za juu kabisa kutoka kwenye tovuti zote za Global Voices zilikuwa ni:

1. Marekani
2. Brazil
3. Japan
4. Uhispania
5. Ufaransa
6. Mexico
7. Ajentina
8. Colombia
9. Peru
10. Taiwan
11. Italia
12. Uingereza
13. Bangladesh
14. Ujerumani
15. Ecuador
16. Urusi
17. India
18. Canada
19. Indonesia
20. Chile

Lakini hiyo ni tone tu la upana wa usomaji wake. Tuangalie zana za True Random Number Generator [2] kutoka Random.org na kuangalie nchi chache kwenye orodha hii:

177. Iceland
61. Kazakhstan
111. Bahrain
49. Costa Rica
68. Cameroon

Global Voices kwa Kiingereza

Tovuti ya Kiingereza ndiko ambako maudhui ya awali huchaishwa hapa Global Voices. Habari tano zilizosomwa zaidi kwenye juma lililopita:

1. Madai ya wizi wa kura kwenye uchaguzi uliokiwezesha chama tawala nchini Malaysia kushinda (ilichapiswa 2013).
2. 
‘Peppa Pig’ iemvuka mipaka kwa ufuatiliaji wa habari China [3]
3. Majukwaa ya mitandao ya kijamii yafungiwa wakati wa-Turuki wakisema ‘imetosha’ kwa Rais Erdogan [4]
4. Hijab na sketi fupi: Kile usichotakiwa kukivaa ukiwa Tajikistan [5]
5. Nchini Uhispania, uamuzi wa kashfa ya ngono ya “la manada” wachochea maandamano makubwa [6]

Global Voices Lingua

Lingua ni mradi unaotafsiri habari za Global Voices kwenda kwenye lugha nyinginezo zaidi ya Kiingereza. Kuna zaidi ya tovuti 30 zilizo hai. Hapa chini ni habari na tafsiri zilizosomwa zaidi wiki iliyopita kwa kila tovuti hai:

Kiarabu

Bangla

Catalan

Kichina (kilichorahisishwa)

Kichina (cha asili)

Czech

Kidachi

Farsi

Ufaransa

Ujerumani

Ugiriki

Hindi

Kiindonesia

Italia

kijapani

Kikudi

Macedonia

Malagasy

Nepali

Polish

Kireno

Punjabi

Romanian

Russian

Serbian

Spanish

Swahili

Urdu