- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanaharakati wa Cuba Waanzisha Ajenda Kuhusu Haki za Mashoga Nchini Cuba

Mada za Habari: Amerika Kusini, Cuba, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala
[1]

“Bendera ya mashoga nchini Cuba.” Imepewa leseni ya Creative Commons- Unaweza kusambaza kwa leseni ya 4.0 kimataifa.

Hapo Mei 11, 2018, kundi la wasomi na wanaharakati wa Cuba walizindua ajenda nzito [2] kuhusu haki za wasagaji, mashoga, watu wenye jinsia mbili, waliobadili jinsia na watu wote wenye hisia mchanganyiko dhidi ya mapenzi nchini Cuba. Kulingana na kilichowasilishwa:

Basados en los principios de Yogyakarta [3] sobre la aplicación de la legislación internacional de derechos humanos en relación con la orientación sexual y la identidad de género, en la Declaración de derechos sexuales de la Asociación Mundial para la Salud Sexual (WAS) [4] y en virtud de las próximas reformas constitucionales y jurídicas en Cuba, integrantes de la comunidad LGBTIQ cubana nos hemos reunido para promover esta agenda.

Kulingana na kanuni za Yogyakarta [5] katika maombi ya sheria ya kimataifa kuhusu mahusiano na utambulisho wa jinsia, katika Azimio la Haki za Kujamiiana la Jumuiya ya Afya ya Kujamiiana (Declaration of Sexual Rights of the World Association for Sexual Health (WAS)) [6] na kwa sababu ya marekebisho ya katiba na sheria yanayokuja nchini Cuba, wanachama wa jumuiya ya mashoga Cuba wamekutana kuhamasisha ajenda hiyo.

Andiko hilo linaanza kwa kutambua mirengo ya kujamiiana na utambuzi wa jinsia kuwa ni vitu vya asili katika utu wa binadamu. Lengo sio tu andiko hilo litumike kama tamko la pamoja lakini pia litumike kama pendekezo ambalo wachangiaji wataendelea kujazia mawazo na mapendekezo yao. Andiko hili pia lilipendekeza baadhi ya vipengele ambavyo vinaweza kuanza kutumika kwa ajili ya utafiti na kuanzisha sera za umma kama Isbel Díaz Torres anavyoelezea [7] katika Havana Times.

Mkakati huu ni wa kwanza na wa aina yake nchini Cuba, umeandaliwa moja kwa moja na wanajamii na umelenga katika haki za wanachama wa umoja wa mashoga. Kwa kuongezea, limehusisha mahitaji 63 na limegawanyika katika sehemu kuu mbili: mitazamo ya kisheria, kisera, mipango na mikakati.

Muongoza sinema wa Cuba Yaíma Pardo aliweka utangulizi muhimu kwa mahitaji yaliyotolewa katika makala yake ya Causas y Azares (Sababu na Nafasi), tafsiri kwa kiingereza inapatikana [8]. Utangulizi mwingine ulikuwa wa chapisho [9] lilioandikwa na mwanaharakati na mwanablogu Alberto Roque [10]. Makala ilionesha chambuzi kadhaa kuhusu hali ya sasa ya haki za wanaLGBTQI nchini Cuba na mitazamo na mabadiliko muhimu ya kitaasisi kuhakikisha inafanya kazi ipasavyo.

Mercedes García na Yasmin Silvia Portales Machado ni wanaharakati wawili ambao walishiriki katika makala hiyo, walifafanua mambo muhimu ya kutambua na kuzingatia katika kutambua na kuzilinda haki za mashoga Cuba. Katika kanuni wameelezea jinsi serikali ya Cuba isivyotambua ugumu wa muundo wa kijinsia au utofauti wa kujamiiana baina ya binadamu. García alichambua mapungufu ya Cuba katika hili:
Lamentablemente el proyecto social socialista heredó esa discriminación, esos falsos conceptos, esa ignorancia sobre la sexualidad humana; y en el caso Cuba se ha demorado, para mi gusto, demasiado en enfrentar esa realidad y transformarla

Jambo la kusikitisha, mradi wa jamii ya Ujamaa umerithi unyanyapaa, mitazamo hasi, umbumbumbu kuhusu kujamiiana kwa binadamu na katika shauri la Cuba imechukua muda mrefu sana kwa mtazamo wangu, kuukabili ukweli huu na kuubadilisha.

Machado aliipanua mada hii na kuonesha jinsi misingi ya historia na utamaduni wa mitazamo ya siasa za Cuba zinavyozuia upekee wa maisha ya raia wake:
El Marxismo surgió como una filosofía en occidente de un hombre blanco. No reconoce la diversidad de las sexualidades ni de las identidades que las personas cargan como parte de su cultura. No todo es la lucha de clases. Cada clase social está atravesada por un montón de identidades culturales y sexuales… y laborales… y artísticas. Reconocer eso es lo que permite que las políticas [creadas] para emancipar a las personas atiendan verdaderamente a las personas y no a los ideales [que el Estado tiene] de las personas… [es ahí] donde ha fallado hasta ahora el socialismo.

Ajenda ya Haki za LGBTIQ nchini Cuba [11] inahamasisha mjadala mkubwa na mpana kuhusu haki za binadamu na kutaka mahitaji yao yafikiriwe na Bunge laTaifa la Nguvu ya Umma, Baraza la Mawaziri na wale wote wanaotengeneza sera, mipango na mikakati nchini Cuba.