- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

“Nilitamani Wajukuu wangu Wakulie kwenye Nyumba Ile”:Ushuhuda wa Mwanamke wa Syria mwenye Miaka 61 kutoka Zamalka

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Syria, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhamiaji na Uhamaji, Vita na Migogoro, Wanawake na Jinsia, The Bridge

Picha ya nyumba yake iliyoharibiwa vibaya. Picha kwa hisani ya Kijana Madogo wa Lens of a Damascene.

Huu ni ushuhuda wa Um Mohammed; mwanamke mwema wa miaka 61 kutoka Zamalka. Ukarimu wa Um Mohammed unawakilishwa na sura yake iliyojawa na mwonekano wa wakati wa utoto wake. Mashavu yake bado yanaweza kuwa myekundu pale anapoghadhibishwa.

Um Mohammed anazioendanyimbo za zamani na amekariri baadhi yake.Kama bibi mwenye upendo, anawasujudu sana watoto na angaliweza naokwa masaa.

Um Mohammed alikuwa akiishi Zamalka, mji uliopo Ghouta Mashariki. Katika sensa ilipita, mji huu ulikadiriwa kuwa na watu laki moja na nusu.
Zamalka uliacha kuwa chini ya uangalizi wa serikaki mwaka 2012. Tangu hapo, umekuwa ukikabiliwa na majanga mabaya, sambamba na miji yote ya Ghouta Mashariki. Zamlaka ilikabiliana na mabomu ya kutupwa mfululizo karibu kila siku.

Katika ushuhuda huu, Um Mohammed aliehamiahwa kwa lzima anaelezea kuhusu nyumbana familia yake huko Zamlka na pia kuhusu uhusino wake na nyumba hiyo pamoja na samani zake:

Ninao watoto watatu wa kike na wa kiume mmoja. Watoto wangu wa kike walibaki nami Ghouta, huku mtoto wangu wa kiume aliondoka miaka saba iliyopita. Mgogoro huu ulinaizuia kushiriki sherehe ya ndoa ya mtoto wangu, au hata kuwa naye pale alipojaaliwa mtoto wake wa kiume.

Niliishi kwenye nyumba ya familia. Nyumba ya zamani sana ambayo mume wangu aliirithi kutoka kwa baba yake ambaye naye aliirithi kutoka kwa baba yake. Kizazi baada ya kizazi kilikulia katika nyumba hiyo. Wale ambao bado wapo hai wana kumbukumbu nzuri sana kuihusu nyumba hiyo. Hata pale nyumba hii ilipohitaji matengenezo, tuliifanya kazi hii kwa unyenyekevu sana ili kuendelea kutunza mwonekano wake wa mwanzo. Tulinuia kulinda uasili wake.
Wakati wa mgogoro vyanzo vyote vya nishati vilikuwa vya kubahatisha sana au kupatikana kwa bei ya juu sana kuliko kawaida. Kwa hiyo ilitubidi tutumie kuni zaidi kwenye upashaji joto, kupikia, kupashia maji ya kuoga na wakati mwingingine hata kutumika kama chanzo cha mwanga.

Jinsi mabomu ya kutupwa yalivyokuwa yakiongezeka katikakipindi cha mwezi Februari, haikuwa rahisi kutoka kwenye basement na kwenda kununua kuni. Kukosekana kwa mfumo mzuri wa hewa safi kwenye basemwnt na hali ya ukungu ilfanya hali ya baridi kuwa mbaya zaidi.
Siku moja katika basement hiyo, wakati mji ukiungua kwa moto wa mabomu, ilitulazimu kutumia samani kama kuni. Sitakaa kusahau bomu hilo lililoharibu kumbukumbu zetu na kumbukumbu za wote waliokuwa karibu yetu. Lilifuta kabisa uwepo wetu mjini Zamalka, eneo letu la asili, kabla ya kuondolewa.
Samani zamkwanza kabisa kuzichoma ilikuwa ni makochi, na hii ilitokaa na njaa. Wajuu wangu walikuwa na njaa, na bahati mbaya mfululizo wa mabomu ulituzuia kwenda kununua kuni. Hata kama mtu angejitokeza kwenda kununua kuni, hakukuwa na yeyote aliyekuwa akiuza kutoka na hali ilivyokuwa mbaya. Mkwe wangu aliniomba alivunje kochi ili tutumie mbao hizo kwa ajili ya kupikia. Nilimkubalia lakini kuna kitu ndani mwangu nilihisi hakikuwa sawa.
Kochi hilo lina kumbukumbu ya kuvutia sana. Mume wangu alilinunua miaka kumi baada ya ndoa yetu. Alikuwa na furaha sana kwa kuweza kulinunua. Tulienda pamoja kulichukua. Ilikuwa ni mara chache sana kutoka pamoja hivi na kuwaacha watoto. Ndio, ninaweza tens kuvipata vitu hivyo, lakini kwa kumbukumbu zinazohusishwa na vitu hivyo, lakini ni kwa namna gani kumbukumbu hizi zitarudishwa tena kwenye vitu hivyo?

Maumivu yalikuwa makubwa zaidi pale tulipotakiwa kuchoma samani za chumba changu cha kulala. Chumba kile kilikitumia kwa miaka 35, tangu nilipoolewa. Kilinipitisha kwenye nyakati nzur na mbaya sana za maisha yangu. Manukato ya marehemu mume wangu yangalipo hadi sasa kwenye chumba hiki. Nilikuwa nikihisi roho yake ikielea chumbani hapo, ndio maana siku zote nilihisi alikuwa pembeni yangu nilipokuwa ninalala.
Nilichoma nguo zangu karibu zote. Mojawapo likiwa gauni nililovaa wakati wa sherehe ya kuolewa kwa mtoto wangu wa kwanza. Ninakumbuka nilivyoenda nae kwa fundi cherehani ili atushonee gauni kwa ajili ya sherehe hiyo, sambamba na gauni lake la harusi. Mavazi yangu mwenyewe, niliyoyatumia tangu nilipokuwa mtu mzima hadi nilipokuwa mzee. Niliweza kutunza moja tu ambalo ningelivaa oale ambapo tungelazimishwa kuhama.

Miongoni mwa vyombo vyangu vya nyumbani vilivyosalimika baada ya mabomu, nilichoma vyombo vyote vya plastiki kwa kuwa viliwaka vizuri sana na kutoa joto la ziada. Kilichokuwa cha muhimu zaidi ilikuwa ni watoto wangu na wajukuu wangu kula na kuota moto.
Kwa utamaduni wetu, familia ya bibi harusi humuoza mtoto wao na kumpeleka kwa mume wake sambamba kabati la glasi ambapo sahani za kifahari na vitu kama vijiko, uma na visu vya kulia viliwekwa. Kwa kawaida, kabati hili hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo mara baada ya vyombo vya kioo kuvunjika kutokana na shambulio la bomu, kabati lile tulilivunjavunja na kutumia mbao zake kama kuni za kupashia maji ya kuoga.

Kama haikutosha, moja ya hali ngumu sana nliyoipitia ni kufanya uamuzi wa kuchoma kabati la nguo la mtoto wangu wa kiume. Mtoto wangu ambaye sikuwahi kuonana naye kwa miaka saba.

Kabati hilo lilikuwa na kumbukumbu nyingi na nzuri za tangu utoto wake. Midoli yake, nguo zake za utotoni na hata kikombe chake alichokipenda sana. Siwezi kubeba vyote hivi katika basi hilo la kuhamishwa kwa lazima. Lakini pia siwezi kuharibu kumbukumbu hizi kwa mikono yangu mwenyewe, wala kuziacha halafu watu wabaya waje kuziiba mara baada ya sisi kuondoka, au kuziona kupitia video zikiwa zinauzwa mitaani. Hatimaye nilifikia uamuzi wa kulivunja kabati na kuchoma nguo zilizokuwemo. Nilibakiza vitu vichache sana ambavyo ningeweza kusafiri navyo.
Hiyo ilikuwa ndio hali ngumu kabisa kuliko yoyote ile. Kwani muda wote nilikuwa na ndoto ya kuja kumpatia mwanangu vifaa vyake vya utotoni, na kumwona mototo wake akivaa nguo za baba yake alipokuwa na umri wake, na pia kumsimulia mjukuu kuhusu picha za baba yake.

Nilipenda wajuu wangu wakulie kwenye nyumba ile ili niwahadithie changamoto walizozipitia wazazi wao. Makazi ambayo ningewarithisha ili nao waje kuwarithisha wajukuu wao; ili wawe wanaiongezea nyumba maisha mapya kila wakati, kama ilivyo kwa kila kizazi cha mababu zetu walivyofanya.

Hatimaye tulilazimika pia kuchoma milango ya nyumba. Nyumba yangu, nyumba ya familia, nyumba ya watoto wangu, iliachwa wazi kabisa, isiyositiriwa na kutelekezwa.

Kufuatia shambulio la mabomu wakati ambapo serikali ya Syria na vikosi vya Urusi vilivyotupeleka kuzimu, tuliondolewa kwa nguvu kutoka Zamalka kama wakimbizi. Hakuwa tena rahisi kwa sisi kuishi chini ya uongozi wa serikali. Serikali ambayo inaweza kumshikilia mkwe wangu au kuwalazimisha kujiunga na vyombo vya ulinzi. Halikuwa jambo rahisi na hususani pale nilifahamu kuwa mototo wangu asingeweza tena kurudi Zamlka.

Niliiacha nyumba ya familia pamoja na kumbukumbu zote ilizozitengeneza. Nilielekea Idlib pamoja na watoto wangu wa kike na familia zao, nikiwa nimekata tamaa kabisa. Jambo moja ambalo lilinipa faraja kwa kiasi fulani ni hatimaye kuungana tena na mototo wangu ambaye sikukaa kuonana naye kwa takribani miaka saba na pia kumbeba mototo wake kwa mikono yangu mwenyewe. Jambo moja linalonipa matumaini ni kuwa nijua kuwa nitamsimulia mjukuu wangu kila kitu kuhusu babu yake, baba yake na nyumba ya familia na kumbukumbu zake zote tangu kuwepo kwa nyumba hiyo.

Mara baada ya kukutana tena na mototo wangu, nilimpatia vitu vichache nilivyoweza kuviokoa kutoka kwenye kabati lake la nguo. Hapo awali, hakuweza kuamini kabisa kuhusu kile alichokiona. Hakumini kabisa kuwa ningeweza kubeba kitu ambacho kingeweza kumkumbusha mbali. Kwa wakati huo, nilitamani sana kuona mwanangu anarudi tena kwenye nyumba ile kuijenga tena upya na kuwakuzia pale watoto wake.

Kwa sasa ninaishi na mtoto wangu na familia yake, huku tukihamahama kutoka nyumba moja kwenda nyingine hadi tutakapoweza kupata sehemu ya kamazi ya muda, ambayo nina hakika kuwa, kamwe haitaweza kuwa mbadala wa nyumba yangu.