- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwa Sasa Bunge la Cuba Lina Makamu wa Rais Watatu Weusi. Inakuwaje Hali Hiyo Haikutengeneza Habari?

Mada za Habari: Amerika Kusini, Cuba, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Utawala, The Bridge
[1]

(kutoka kushoto kuelekea kulia) Inés María Chapman Waugh [2], Beatriz Jhonson Urrutia [3] na Salvador Valdés Mesa [4]. Picha na mwandishi kutoka EcuRed.

Tarehe 19 Aprili, 2018, Jamhuri ya Cuba ilimuapisha Profesa wa zamani wa Chuo kikuu Miguel Díaz-Canel Bermúdez [5] kama Rais wake mpya na bunge la 9 la taifa ambalo —ndiyo chombo cha juu chenye nguvu serikalini —lilichagua Halmashauri mpya ya taifa. Lakini furaha na wasiwasi vipo ukizingatia “Cuba kutokuwa na Castro” na masuala mengine yanayohusiana yamezuia maendeleo makubwa: Kuwepo kwa viongozi wanne weusi ambao ni sehemu ya serikali mpya hadi mwaka 2023.

Wacuba weusi ni asilimia 10 ya idadi ya watu wa Cuba [6] lakini uwakilishi katika awamu za serikali umekuwa mdogo mno ingawa baada ya mapinduzi ya Cuba kumekuwa na dhana ya usawa.

Kabla ya Bermúdez , bunge lililopita lilikuwa na wacuba weusi wawili wa kiume katika nafasi za juu: Makamu wa kwanza wa Rais Juan Esteban Lazo Hernández [7] and Salvador Valdés Mesa [4], ambaye alikuwa rais wa bunge la taifa. Kuteuliwa kwa Inés María Chapman Waugh na Beatriz Jhonson Urrutia kama makamu wa Rais, nchi ya Cuba imeongeza “rangi zaidi” katika serikali.

Kabla ya kuwajawadili wanawake wawili, nitumie dakika chache kuelezea Valdés Mesa na Lazo Hernández.

Valdés, ambaye alishika nafasi ya katibu wa muungano mkuu wa wafanyakazi nchini Cuba, waziri wa kazi na hifadhi ya jamii, na pia Katibu wa umoja wafanyakazi wa kilimo si miongoni mwa kizazi cha “los históricos” yenye maana wale waliongoza mapinduzi nchini Cuba mwaka 1959, na ambao wamekuwa wakiachiwa madaraka pindi wenzao wanapoondolewa au kufa. Kama ilivyo kwa Lazo ambaye alichanguliwa kuwa Rais wa Bunge la taifa mwaka 2013, anatokea katika kizazi kilichofuata na atakuwa katika nafasi hiyo hadi mwaka 2023, atakapokuwa na miaka 79.

Lazo ana historia ndefu katika siasa za Cuba; amekuwa ni katibu wa chama cha kikomunisti cha Matanzas huko Santiago Cuba na mikoa ya Havana, mbunge wa bunge la Cuba tangu mwaka 1981, na makamu wa rais wa Halmashauri ya taifa tangu 1992. Pia, Lazo ameiwakilisha Cuba katika masuala ya mambo ya nje katika Karibi, Afrika na Asia. Alichaguliwa kuwa rais wa bunge la taifa la nguvu ya umma tarehe 25 Feburuari 2013.

Makali mapya ya uchunguzi

Wanawake wawili wapya ambao ni makamu wa rais kwa vigezo vya bunge ni vijana kama tukiangalia umri wao bungeni—ni karibu asilimia 13 ya wabunge wana umri chini ya miaka 35.
Ines María Chapman Wa [8]ugh [8], ni mhandisi kutoka Holguín. Kwa sasa ni rais wa taasisi ya taifa ya rasilimali ya maji. Kwa watu wa Cuba ana jina litumikalo na wengi. Kwa muda sasa, amekuwa ni nembo ya shirika analoliongoza,kwa kuwa huhabarisha umma habari muhimu kipindi cha majira ya kimbunga. Alikuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa uliotangulia bunge la taifa na ni mjumbe wa halmashauri ya taifa tangu 2008. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama cha Kikomunisti cha Cuba.

Pia, Beatriz Jhonson Urrutia [9] ni mhandisi. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa makamu wa raisi wa baraza kuu la mkoa la nguvu ya umma katika mkoa wake alikozaliwa wa Santiago, Cuba. Hatimaye akawa rais wa chama hicho mwaka 2016. Muongo ulioyopita katika bunge la saba alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu na akawa mbunge mwaka 2013.

Kwa pamoja Chapman Waugh and Jhonson Urrutia wanatoka vijijini na tangu mapema walijiendeleza katika kazi za kitaaluma au katika vyama vyao. Kama wanawake weusi , hadi hatua hii, wamefanya kazi kwa bidii katika kupata shahada na kujenga taaluma za kazi zao na teuzi za hivi karibuni hazimaanishi kuwa wamefika. Sasa wameingia katika sehemu ngumu si muda mrefu sana ambapo “watajaribiwa” kutokana na weusi wao na kulazimika kuchunguzwa na inategemewa wanaweza kuharibu majukumu.

ukimya pia ni ubaguzi wa rangi.

Kwa nini watu wa Cuba na vyombo vya habari vya kimataifa na umma kwa ujumla hawajakumbatia na kusifia maendeleo haya kwa shauku? Naona kuwa ina tia shaka, nikifikilia, huu ni mshangao mkubwa zaidi kwa mazingira ya sasa ya kisiasa, kwa Diaz-Canel, yeye uteuzi wake ulitegemewa. Hivi sasa vyombo vya habari vimeelekeza macho yao kwa mke wa Rais na viongozi wengine huku vikiendelea kutojali habari hii muhimu.
Kufanya vitu visijulikane ni njia mojawapo ya ubaguzi wa rangi kutenda kazi. Muda mwingine ukimya unazungumza zaidi ya maneno ambavyo yangeweza. Kitu kilichopo hapa kazini ninachofikiria ni maisha ya kila siku ambapo kuna mchanganyiko wa uoga wa weusi na ubaguzi wa kawaida wa rangi wa kisasa. Hii hujumuisha dhana rasmi iliyopo Cuba kuwa ukiongelea weusi na ubaguzi wa rangi unaingawa nchi.

Kwa kuongezea wazo hilo la mwisho, ni kwamba hata miongoni mwa wanaharakati wa kisiasa na kijamii wenye msimamo na watu wa kawaida kwa namna fulani masuala ya ubaguzi wa rangi hufikiriwa kuwa yanafifilisha “lengo kuu”. Ni kutokana na msimamo huu mawazo yanayotokana na isitilahi ya “mcuba mweusi” hata kama ni ubaguzi wa rangi wa matabaka uliyopo nchini yanapingwa.
Ni vizuri kufikiria kwamba hakutakuwa na badiliko katika sera zinazuhusu ubaguzi wa rangi, ni muhimu kusema kuwa kuingia kwa hawa wabunge weusi, hasa wanawake wawili kutapelekea msukumo kuelekea ushirikishwaji. Au inaonesha kuwa katika kisiwa hiki angalau ushirikishwaji umezingatiwa katika nafasi za juu za serikali.

Tunaweza kuamini kuwa hakuna mwenye nafasi katika Baraza kuu la taifa ambaye ana ajenda bayana ya kisiasa inayopinga ubaguzi wa rangi. Kama wabunge wa bunge la Cuba wangewezaje? Na ninaona hii kama ushahidi wa ubaguzi wa rangi, pamoja na ukamilifu wa mfumo wa uchaguzi wa Cuba, vikwazo na namna ya kuwa “mwanasiasa” katika Cuba. Hii ni nchi ambayo wanaharakati waliopigania uhuru huwekwa pembeni ya nafasi halali serikalini—ambayo hujenga hali ya ajabu kwa watu hukosa kabisa hamu ya kisiasa au uelewa wa umma unaweza kukaa kwa miaka mitano katika mhimili mkuu wa serikali.

Kubadilisha hilo kunahitaji kushawishi walioko madarakani wajue kuwa ubaguzi wa rangi kwa sasa ni tatizo kubwa sana Cuba. Tatizo hilo limeunganika na mambo mengine kama umaskini na linazuia kufurahia haki za msingi na za binadamu wote kama upatikanaji wa elimu ya chuo kikuu.
Woga wa kushughulikia jambo hilo unaonekana hata kwa wenye mamlaka wa Cuba wanavyoshughulikia kwa namna ya chini matokeo ya machapisho, utafiti na tasnifu zinazohusu ubaguzi wa rangi. Mimi ninashangaa, ni kitu gani zaidi kinatakiwa ili kulikiri na kila kinachususiana na tatizo hilo — na yafuatie mapendekezo ya sera ya umma kushughulikia ubaguzi wa rangi.

Masuala ya ubaguzi wa rangi hayajaorodheshwa kama mada /malengo na makundi kumi ya kudumu yanayofanya kazi katika Baraza kuu la taifa la nguvu ya umma. Angalau naweza kufiria makundi matatu yanayohusika na suala la ubaguzi wa rangi: Tume ya uangalizi wa watoto, vijana na haki sawa kwa wanawake; Tume ya Masuala ya Uchumi; Tume ya elimu, utamaduni, sayannsi, teknologia na mazingira.

hakuna ubaguzi wa rangi nchini

Kama kuna mada ambayo wananchi katika vyama vyao wanaikubali ni ubaguzi wa rangi. Kwa pamoja wapinzani na wafuasi wa serikali ya Cuba wanasema kutoka moyoni kwamba katika “Cuba wazungu na watu weusi ni sawa.” Kwa wafuasi wa serikali waliopo ndani na nje ya kisiwa hali ya unyanyasaji pamoja na jambo hili ni nzuri. Kwa wapinzani kokote kule, mambo katika Cuba ni ya kutisha na kila mwananchi ananyanyaswa sana kiasi kwamba ubaguzi wa rangi unahitaji tahadhali maalumu. Tofauti hizi zinateka mjadala na zinatuzuia kusonga mbele. Miongoni mwa jamii zinazoishi uhamishoni kwao radha ya ubaguzi wa rangi nchini Cuba ni zaidi ya uadui na serikali.

Picha ya haraka kutoka katika mtandao wa Facebook: “Diaz Canel sio mbaya. Ni “N*****-mzigo” ulioachwa [kumaanisha chuki, ubaguzi wa rangi, chuki kwa wageni na ufisadi Cuba] Raúl Castro karibu na serikali. Serikali ijayo ya Cuba, na uliundwa uhamishoni, inatakiwa kwaondoa wagombea weusi… hakuna ushirika na utawala, uchawi, uzembe, wizi na dhaifu”


Kwa sasa, tungekuwa tunatekeleza ufumbuzi, kwa mfano tatizo la uwingi wa wacuba weusi na wenye rangi mchanganyiko gerezani. Tayari ungekuwa na mwafaka juu ya miradi ya kujiajiri katika jamii.

Hata hivyo inanipa matumaini kwamba kuna wanasiasa wazoefu wanaowakilisha wacuba weusi japo si kwa ukamilifu. Makamu wetu wa rais watatu siwaombi chochote ambacho sikiombi kwa wabunge wengine, lakini kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika Cuba kunahitaji ushirikiano wa wajumbe wote kutokana na heshima na nafasi zao walizonazo.

taarifa hii ilionekana awali kwenye blogu Negra cubana tenía que ser. [10]