- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Brazil Yatambulisha Kanuni Ngumu Dhidi ya ‘Habari Zisizo za Kweli’ Kuelekea Uchaguzi wa 2018

Mada za Habari: Brazil, Censorship, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi

    Wakati Brazil wakitengeneza mbinu mpya ya kupambana na ueneaji wa habari zisizo za kweli, wanaharakati wa mtandaoni wanahofia kuwa hili litazuia uhuru wa kujieleza. Picha na Digital Spy on Flickr, imetumiwa kwa ruhusa: CC BY-NC-SA 2.0

Mwanzoni mwa Disemba 2017, serikali ya Brazili iliunda kamati ya kuratibu na ikibidi kufungia taarifa zisizo za kweli katika mitandao ya kijamii kuelekea uchaguzi wa Rais utakaofanyika mwaka 2018. Habari hiyo imeamsha hisia kuhusu udhibiti huo miongoni mwa jamii.

“Baraza la Ushauri kuhusu Mtandao wa Intaneti na Uchaguzi” litafanya kazi chini ya mwamvuli wa Mahakama Kuu ya Masuala ya Uchaguzi likihusisha wawakilishi kutoka katika Mahakama, Wizara ya Sheria, Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Jeshi, Shirika la Ujausi la Taifa, Jeshi la Polisi, SaferNet (shirika lisilo la Kiserikali nchini Brazili (NGO) ambalo hupambana na uhalifu wa.mitandaoni ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya Jamii) na Chuo binafsi cha Getúlio Vargas Foundation.

Katika kikao chake cha kwanza, Baraza lilipendekeza [1] kutengenezwa kwa zana ambayo watumiaji wa mtandao watakuwa wakitumia kutoa taarifa dhidi ya habari wanazozitilia shaka. Hii itapanua wigo ukijumlisha na uwepo wa simu ya moja kwa moja na fomu katika tovuti ambazo wapiga kura watakuwa wakitumia kufikisha malalamiko yao dhidi ya vyombo vya habari.

Baraza halikueleza zaidi jinsi zana au kifaa hicho kitavyokuwa kikifanya kazi katika kuyataka makampuni ya mitandao ya kijamii kuondoa habari zisizo za kweli au jinsi itakavyowalenga watu na vikundi vitakavyokuwa vimetoa habari za uongo. Wajumbe walisema kuwa walikuwa wanajadili kuungwa mkono na makampuni ya mitandao ya kijamii lakini haifahamiki uelekeo wa suala hili utakuwa upi.

Kipindi Facebook walipotambulisha kipengele cha “ripoti taarifa isiyo kweli” hapo Disemba 2016, ilionesha kuwa watumiaji wengi waliripoti [2] mahudhui yasiyo ya kweli kama jitihada za kukataa taarifa au mawazo ambayo wao hawaafikiani nayo hata kama mawazo hayo ni hakika na yamethibitishwa.

Mpango huu umekuja wakati kukiwa na mkanganyiko mkubwa wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu nchini Brazili, ambapo utakuwa uchaguzi wa kwanza ukifuatia tuhuma tata [3] dhidi ya Dilma Rousseff, Raisi wa Chama cha Wafanyakazi hapo 2016.

Mgombea halisi wa chama kwa mwaka 2018 ni Raisi wa zamani Luiz Inácio “Lula” da Silva, ambaye anaongoza [4] kwa kura za maoni kwa 34% na amekuwa akizuru nchi na kukusanya umati wa watu ingawa amehukumiwa hapo Julai kifungo cha miaka karibu kumi kwa kosa la kupokea rushwa kutoka kwa makampuni ya ujenzi katika kipindi cha Uongozi wake. Mahakama inatarajiwa kusikiliza rufaa yake hapo Januari 24.

Upelelezi dhidi ya rushwa kubwa umewafunga [5] makumi ya wanasiasa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kufungua milango kwa watu wa nje na wale wa mrengo wa kulia kama vile Jair Bolsonaro, Msaidizi wa Kamanda na Afisa wa Jeshi Mstaafu, anayejulikana kwa kunanga mapenzi ya jinsia moja pamoja na kuwa na mijadala mikali dhidi ya uhalifu na wauza dawa za kulevya.

Lazima hukumu ya Lula ikizingatiwa [6], tutegemee mgawanyiko, ubaguzi na mgogoro mkubwa katika uchaguzi

Sheria zaidi zakusudiwa katika kupunguza ‘habari zisizo za kweli’

Kamati hii ni moja kati ya matokeo ya haraka ya Mahakama ya Masuala ya Uchaguzi iliyojazwa na ‘habari za uongo’. Majaji wametetea wazi kuundwa kwa mfumo wa ziada wa kisheria kuwajibisha habari zitakazodhaniwa kuwa ni za uongo.

Katika kuwasilisha sheria za uchaguzi wa mwaka 2018, Jaji Luis Fux, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa mahakama kuanzia Februari alizungumza kuhusu kuunda hatua za tahadhari [7] za kuzuia kuenea kwa bahari za uongo. Hili litahusisha kutaifisha mali na hata kifungo kwa wale watakaokuwa ” wamejiandaa kuendelea na mpango huu mbovu, hivyo ni kusema kuwa kwa lugha isiyo rasmi, kuyeyusha baadhi ya nafasi za uteuzi”

Kwa kuongezea, Bunge la Brazili linachambua muswada [8] ambapo kutoa taarifa zisizo kweli katika mitandao ya kijamii litakuwa kosa la kuadhibiwa kwa kifungo cha miezi miwili hadi nane gerezani au faini ya fedha za Kibrazili 1,500 hadi 4,000  ambazo ni (dola za Marekani500-1200) kwa siku. Muswada unafanya “kuchapisha au kushirikisha kwa njia yoyote kwenye intaneti habari za uongo au habari ambayo haijakamilika na uongo huo kusababisha madhara kwa makusudi kwa mtu binafsi au kiongozi, kuwa kosa la jinai.”

Wanaharakati wa Uhuru katika waongea

Wanaharakati wa uhuru wa mitandaoni wameelezea wasi wasi wao kuhusu mswada na kuundwa kwa Baraza la Ushauri. Barua ya wazi [9] iliyochapishwa na Direitos na Rede (Muungano wa Kugombea Haki za Mitandao) wakati wa Jukwaa la Intanet Brazili (mkutano wa kanda ulioutangulia mkutano wa ulimwengu kuhusu uendeshaji wa Intaneti) ilikosoa rekodi mbaya ya jeshi katika kuheshimu uhuru wa raia katika mwaka huu (Brazil ilitawaliwa na Marekani-ikisaidiwa na utawala wa kiimla wa jeshi kuanzia 1964 mpaka 1985):

As Forças Armadas não podem monopolizar o controle da veracidade dos fatos porque 1) não possuem essa competência constitucional; 2) não têm as condições técnicas para isso; 3) não detêm o conhecimento para distinguir fake news; e 4) não são neutras na política. Para piorar, essas instituições deixaram violentas e profundas marcas na história recente do país ao promoverem o cerceamento da liberdade de expressão e de manifestação dos brasileiros/as durante a ditadura civil-militar.

Majeshi yenye silaha hayatahodhi ukweli wa mambo kwa sababu 1) hawamiliki mamlaka ya kikatiba; 2) hawana uwezo wa kitaalamu kuhusu hiki 3) hawana utaalamu wa kutofautisha habari ya uongo; na 4) hawako sawia katika siasa. Kuifanya kuwa mbaya zaidi, taasisi hizi zimeacha vurugu na makovu makubwa katika historia ya nchi ya hivi karibuni kwa kuhamasisha kukatishwa kwa uhuru wa kujieleza na maandamano ya waBrazili wakati wa utawala wa kiimla wa kiraia-jeshi.

Kuundwa kwa kamati na Mahakama ya Masuala ya Uchaguzi pia ilitajwa katika taarifa ya pamoja iliyosainiwa na mashirika 38 kutoka Amerika ya Ulatini na Karibiani kama mfano wa jinsi mjadala wa habari zisizo kweli unavyoweza kuzuia uhuru wa kujieleza.

Barua [10] ilielezea mashaka jinsi hofu juu ya habari zisizo za kweli ilivyogubika jitihada za muda mrefu za kuwa na sheria bora za kuhodhi vyombo vya habari [11] ambapo imeshikilia vyombo vikuu vya habari katika ukanda na vimekuwa na historia ya kushiriki katika kampeni kuhusu kutoa taarifa zisizo sahihi wakati wa uchaguzi au vinginevyo:

Hatuwezi tukapoteza miaka ya kazi na majadiliano kwenye harakati za kidemokrasia ya mawasiliano na kuchukua kauli ya “habari zisizo za kweli” kama kitu kipya kabisa katika Amerika ya Ulatini. Kutokutilia mkazo uwiano baina ya mamlaka mpya na za zamani kuhusu umiliki wa vyombo vya habari, kuhodhi mitandao ya kijamii na kiu ya mamlaka za Kisiasa kudhibiti na kutawala mawasiliano ndani na nje ya mipaka inafungua mlango wa madhara yasiyo mithilika.