Serikali ya Uganda Yapanga Kutoza Kodi Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kwa Kuendekeza Umbea

Wakati Rais Mseveni wa Uganda akipanga kutoza kodi mitandao ya kijamii kama njia ya kuzuia umbea, raia wa mtandaoni wanahoji kuhusu uhuru wa kujieleza. Picha na Pixabay kupitia CC0 Creative Commons, na imetumiwa kwa ruhusa.

Rais wa Uganda Yoweri Mseveni anataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwajibika kwa umbea wao—na wakati huo pia watunishe pato la Taifa.
Mapema mwezi Aprili 2018, Rais Mseveni alielekeza Wizara ya Fedha kuanzisha kodi kwa ajili ya mitandao “maarufu” ya kijamii kama vile facebook, Twitter na WhatsApp.
Rais Mseveni anawaona watumiaji wa mitandao ya kijamii hutumia majukwaa hayo ya habari mtandaoni kwa kile anachokiita ‘lugambo’ (maana yake umbea katika lugha ya lugwere). Kwa kauli yake iliyokaririwa na gazeti la Daily Monitor, Rais Museveni anaeleza msimamo wake:

Sipendekezi kodi itozwe kwa wanaotumia intaneti kwa madhumuni ya elimu, utafiti au rejea…..madhumuni hayo yatabaki bila kutozwa chochote…. Hata hivyo, lugambo katika mitandao ya kijamii (maoni, chuki, matusi, maongezi ya kirafiki) na matangazo kupitia Google na hata kupitia mtandao mwingine wowote lazima yatozwe kodi kwa sababu tunahitaji rasilimali ili kukabili athari za lugambo…

Rais alilalamika kuwa kwa sasa serikali inakosa kodi ya mapato na kuishtumu Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato ya Uganda kwa kuzembea kuainisha vyanzo vipya vya kodi.
Mkazo wa serikali juu ya matumizi ya mitandao mikubwa ya kijamii inaibua suala lililokuwepo muda mrefu ambalo serikali nyingi zimechukua itifaki ya matumizi ya mawasiliano ya kimtandao kama WhatsApp, ambazo zipo huru bila tozo kwa mtu yeyote anayetumia mtandao. Watendaji wa serikali (katika Uganda na nchi nyingine) kwa muda mrefu wanapata hasara ya maduhuli ya uendeshaji wa mawasiliano ya taifa ambayo wao walikuwa wa kwanza kutoa (na wapanga gharama) huduma hizi.
Rais Mseveni anawahakikishia wananchi kuwa kodi hii haitawathiri wale ambao watatumia mtandao kwa madhumuni ya kielimu, itaathiri wale wote ambao watatumia intaneti kwa ajili ya udaku.
Maoni ya gazeti la Daily Monitor, Daniel Bill Opio aliita kuwa kodi inayotozwa kwenye mitandao ya kijamii ni “kirudisha maendeleo nyuma”:

Mitandao ya kijamii inatumiwa sana kwa mawasiliano na pia kama njia ya kupata habari, kuiwekea kodi ni kuzuia haki mbalimbali zilizopo katika kutumia mitandao.

Kiukweli, viongozi hawajaeleza namna (au nani) ya kutathmini ubora wa maudhui ya habari ya mitandao ya kijamii. Kama tetesi zikichukua mrengo wa kisiasa, je zinaonesha kuelekea kwenye kodi au ni sensa isiyo rasmi ya kujua ukosoaji wa kisiasa?
Pia,Wananchi wameeleza wasiwasi juu ya mantiki ya kiuchumi ulioko nyuma ya pendekezo hili. Raisi wa chama cha demokrasia Norbert Mao aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook:

Wakati nchi nyingine zikipunguza gharama za kutumia intaneti, Rais Museveni yeye anataka kuongeza gharama kwenye mitandao ya kijamii. Hakika tunahitaji kufanya gharama za intaneti kuwa bure.

Wananchi wengine wanahoji kama kweli kodi zitakazotolewa zitanufaisha waganda au zitamnufaisha Mseveni mwenyewe, kamailivyo kuwa ikidaiwa siku za nyuma:

Serikali ya Uganda inataka kufaidika mahali ambapo haijawekeza. Wamiliki wa mitandao ya kijamii hutoa bila kutoza kodi, wewe unataka walipe kodi? Je ni fursa ya kuongeza maduhuli, au kukwepa kukosolewa au ni tamaa?!!

Ukweli ni kwamba tarehe 18 Februari, 2016 siku ya uchaguzi katika nchi ya Uganda, mitandao ya kijamii ilizimwa mara mbili, na mwezi Mei siku rais anaapishwa mwanasheria wa haki za binadamu na muimbaji wa mashairi Kizza Ebron alizuiwa.

Pendekezo la kutoza kodi mitandao ya kijamii lina usuli unaokera. Kwa kipindi kilichopita serikali ya Uganda imezima mitandao ya kijamii mara mbili.

Eron analinganisha mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vikubwa:

Mitandao ya kijamii ni barabara kuu. Kodi inayopendekezwa kutozwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ni kama kizuizi cha kijeshi barabarani.

Usitukumbushe nyakati zile…

Kyambadde Ronald, wakili wa haki za kijamii na afya aliaandika kwenye ukurasa wa tweeter:

Kuna wakati serikali ya Uganda inapaswa kufahamu kuwa raia siyo migodi ya dhahabu, kiasi cha kuwatumia hadi tone la mwisho la damu yao, unawezaje kukubali, matukio yanayoendelea ya kodi mpya- kodi za mitandao ya kijamii, kodi za huduma za benki n.k? Tumechoshwa na ukandamizaji wenu#hakizakiraia

Tovuti ya Internet World Stats inaripoti kuwa Uganda ina takribani watu milioni 19 waliojisajili kwenye huduma ya intaneti, ambapo asilimia 43 ya idadi ya watu wake wanapatikana mtandaoni. Azma ya kutoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii itaongeza pengo katika kutumia mtandao.
Hii ni mojawapo ya namna inayolenga kuminya nafasi ya mahusiano ya kiraia nchini Uganda. Ripoti ya Januari 2018 ya shirika lisilo la kiserikali la UNwanted Witness la nchini Uganda, liliandaa picha iliyofifia kwa ajili ya kudai uhuru wa kutoa maoni mtandaoni nchini Uganda:

Mwaka 2017 ni mwaka ambao kulikuwa na orodha kubwa ya waganda walitiwa nguvuni kutokana na maoni yao ya mtandaoni, kamatakamata inayolenga kukwamisha utoaji huru wa habari na uhuru wa kujieleza kupitia mtandao wa intaneti.

Mwezi Machi 2018, Tume ya mawasiliano nchini Uganda ilitoa maelekezo kwa waandaaji wa maudhui ya habari za mtandaoni kuandikisha tovuti zao, hali inayoongeza kikwazo kingine katika uhuru wa kutoa maoni kupitia mtandao wa intaneti. Mwongozo huo unasomeka:

Watoa huduma za taarifa za mawasiliano mtandaoni, ukijumuisha wachapishaji, majukwaa ya habari za mtandaoni, waendeshaji wa redio na runinga za mtandaoni, wanashauriwa kutuma maombi na kupata kibali kutoka Tume mapema iwezekanavyo.

Mpaka sasa, haijajulikana wazi tetesi za kutoza kodi zitatekelezwa au kuratibiwa kwa namna gani au ni lini zitaanza kutekelezwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.