- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msanii Duo wa Nepal Aweka Tumaini la Michoro ya Utupu Kuhamasisha Wanaume Kujipambanua Zaidi

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Nepali, Haki za Binadamu, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

Michoro ya utupu ya wanaume kwa hisani ya Kapil Mani Dixit. Picha na Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Hali ya uanaume katika muonekano tofauti ni jambo linalojitokeza sana kwenye sanaa nchini Nepali kwa karne nyingi. Hebu tazama Chakrasamvara Mandala [1],Nepali [2] ya karne ya 13 katika michoro ya paubha inayoonesha muungano wa miungu ya Chakrasamvara wafuasi wake wa Vajravarahi, au sanamu za mikao ya kimapenzi [3] zinazopatikana kwenye masinagogi ya Kihindu ya huko Kathmandu.

Hata hivyo, kuandaa michoro ya utupu na kuionesha hadharani ni jambo linalohitaji ujasiri nchini Nepali. Kiasili, mwanaume wa nchini Nepali ana wajibu wa kulea familia, jambo linaarishia kuwa mwanaumea anapaswa kuwa nguvu na mjasiri. Kama ilivyo sehemu nyingine duniani, hali hii ya “uanaume” inaashiria kuwa wanaume wa Nepali hawajisikii vizuri sana uanaume wao kuzungunziwa au kujadili kuhusu miili yao au jinsia yao.

Ili kunazisha mjadala kuhusu haswa mtu anajisikiaje kuwa mwanaume na kufurahia kuwa mwanaume, wasanii wawili wa nchini Nepali, Kapil Mani Dixit [4] na Roshan Mishra, [5] wameandaa maonesho [6] ya mfululizo wa michoro ya utupu ya wanaume kwenye Galari ya Mcube [7] jijini Patan until 19 February 2018 [8].

Akiongea na Global Voices, Kapil alitanabaisha kuwa, “Ikiwa wanaume wanathamini miili ya wanawake, kwa nini wao wanawaangalia wanaume kwa dharau?While men appreciate the female bodies, why do they sheepishly look at male bodies?”

Mungu aliwaumba wanaume na wanawake na kuwapa uzuri unaofanana. Wanaume ni wazuri kama ilivyo tu kwa wanawake. Basi na tuifurahie miili yetu. Kwa nini basi tunakwama kwenye kuzungumzia jinsi tulivyo?

“Rangi ya pinki kwenye mchro wangu unawakilisha namna ambavyo jamii imeshindwa kututhamini. Imetufunga pingu kama invyowakilishwa na na rangi hii ya pinki” anasema Kapil. Picha kwa hisani ya Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Washiriki wawili kwenye fremu moja-mmoja akiwa katika hatari, mwingine “amejikubali”. Ni jambo jema ukijikubali, ni vizuri, wanaume wanaweza pia kulia, wanaweza pia kujijali,” anasema Kapil. Picha na Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Roshan amekuwa akijitolea mfano katika mfulizo wa matoleo mbalimbali ya kazi zake. Anasema:

Kazi yangu inawakilisha dhana potofu iliyopo kwenye jamii yetu kuwahusu wanaume. Wanaume wangi wanaona aibu kuzungumza kuhusu miili yao na kuto a hisia zao, mawazo yao hata na ujinsia wao. Miongoni mwa kazi zangu, nane zinamuonesha mwanaume aliyenaswa na anayehangaika kujinasua kutoka kizimbani… Baadhi ya kazi zangu zinamuonesha mwanaume mwenye mtazamo hasi akiwa kwenye mazingira yanayopendeza sana na kazi nyingine zinamuonesha mtu akiwa amenaswa na kugubikwa na mitazamo ya jamii sambamba na hofu. Kwa kuonesha viungo vya mwili wangu kupitia maonesho haya, nimejaribu kuwafikia wanaume wale ambao wanajisikia kukata tamaa, kuona aibu, wapole, huzunika, changanyikiwa, waliokosa uelekeo au hata kujisikia kutazwa Zaidi. Ninachopenda ni kuona wanafurahia hali yao ya kuwa wanaume tuliyojaaliwa na Mungu na tuwe kama tulivyo. blockquote>

Michoro ya utupu iliyoandaliwa na Roshan Mishra. Picha na Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Michoro ya utupu iliyoandaliwa na Roshan Mishra. Picha na Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Michoro ya utupu iliyoandaliwa na Roshan Mishra. Picha na Sanjib Chaudhary. Imetumiwa kwa ruhusa.

Kapil aliongeza, “Watu wengi walishanifuata na kunieleza hapo awali walikuwa na mawazo kama ya kwangu lakini hawakuweza kuzungumia jambo hili”:

Hizi si hisia zatu pekee, tumewakilisha hisia za wanaume wote. Wanaume hawakuwahi kuzungumza kuhusu mambo haya.