Kwa Kumbukumbu ya Aleppo

Picha na Lens Young Halabi ikionesha ukuta mwaka 2013  ukiwa na sentensi “tuko hai na tunabaki; kwa ajili ya ndoto zetu tunabaki”. Imetumika kwa ruhusa.

Kwa wote watakaoishi mahali tulipopaacha….

Tulishawahi kuwa na mapinduzi hapa. Sijawahi kuishi maeneo hayo ila nilikuwa nayatembelea, mgeni na desturi zangu ndogo dogo kama vile kusalimia majirani kwenye ngazi asubuhi, kutafuta vitu ambavyo haviuzwi hapa kwa kawaida, mazungumzo yangu  marefu na madereva taksi, ili kufahamu mlengo wao wa kisiasa na mitazamo yao juu ya vizuizi vya ukaguzi barabarani.

Bado tuna mapinduzi pale ndani ya Bustan Al Qasr. Pale utayaona—labda kama mafedhuli watakuwa wameyafuta picha ya kitoto ya askari na mwanaume mwenye ndevu na nyundo juu yao na maneno yaliyosema: “Mapinduzi yatakayo vunja vichwa”. Huu ulikuwa mwanzo wa mapinduzi yetu ya pili, haya yakiwa dhidi ya wale wanaotaka kubinafsisha haki zetu kwa nguvu ya silaha au dini. Lakini labda haufahamu kuhusu mapinduzi mengi tuliyofanya yaliyochorwa na Abu Maryam. Pengine usingeweza kusikia sauti zetu pale tunapokuambia Abu Maryam ni nani.

Tulifanya mapinduzi pale kwenye kituo cha upekuzi cha “Karaj IlHajez” baadhi ya marafiki zetu walipokea kipigo. Walikuwa wakiandamana ili kituo kifunguliwe kwa ajili ya raia.

Tulifanya mapinduzi pale kwenye kituo cha afya, tulipotoa heshima za mwisho kwa wazalendo mmoja baada ya mwingine na tukawa na mazungumzo yasiyohesabika, maongezi, marafiki na majeraha.

Tulifanya mapinduzi pale katika makaburi tulikuwa na marafiki. Wa karibu sana kwangu alikuwa Mustafa. Tulifungua shule pale iliyopewa jina lake. Iko pale pia. Shule ilitupa sababu ya kusonga mbele, tuliamini tulikuwa tunalipa deni letu. Kaburi la  Mustafa na shule yake vimekuwa vyenu sasa. Kama mkipita maeneo hayo basi mvitendee kwa heshima kwa sababu mtu huyu alikuwa amejaa upendo, kujitoa na ibada. Tulikuwa sehemu ya maono yake na tumeshindwa.

Tulifanya mapinduzi pale, mpiganaji wa kigeni mjinga alipoandika katika kuta kuwa: “Ujenzihuru umeisha”. Mara zote tulicheka ubovu wa sarufi yake. Na vita ilipotokea huko Leishmania na baadhi yetu tulikuwa na kampeni za kunyunyiza, tulikuwa na michoro yetu wenyewe katika kuta ikisema: “Leishmania imekwisha”.  Hivyo ndivyo tulivyokabiliana, hivyo ndivyo tulivyotafuta suluhisho. Hiyo ndiyo sababu utakuta shule zetu na hospitali zikiwa kwenye mahandaki. Tunakabiliana na mabomu. Tulikuwa tunajaribu kupinga. Tulikuwa na mapinduzi pale….

Hospitali ya macho! Pale tuliandamana tena na tena kupinga mahakama za sharia. Pale ISIS ilipowaua wenzetu 35. Pale, maandamano yetu yalipolipukuwa ya kuwafukuza. Pale, niipofungwa gerezani usilaani kwanza, kwani pale pia ndipo nilipoachiliwa huru kwa sababu tulifanya mapinduzi pale

Rudi pale hospitali. Sio kama hospitali zetu za kwenye handaki ila moja kwa watu wote. Mahali hapa panaungana na roho zitakazowaangalia wagonjwa.

Aleppo ya zamani palikuwa mahali pa amani. Pale nilizoea kwenda na kuimba, sisi magaidi wadhalimu tulipenda kuimba, kupendana, kupika na kula kila kitu katika  “Nyumba ya Falafel ” isipokuwa falafel.

Ungeshangazwa na mafungu ya mawe. Hizi zilikuwa nyumba za familia, nyumba ambazo labda ndicho kitu pekee walikuwa nacho. Walilazimishwa kuondoka. Chukua muda kidogo kuomboleza kwa ajili ya kumbukumbu zao.

Hautautambua tena. Nilizoea kuondoka kwa miezi kadhaa lakini sikuuzoea ukubwa wa uharibifu kila niliporejea. Hicho ndicho majirani zako walichopitia hivyo kuomboleza kwa ajili yao haitakuwa na madhara.

Ungekuta, kama wangeruhusu miili isiyohesabika kwenye vifusi. Haikuwa dhamira yetu kuiacha miili yetu namna ile bila maziko stahiki. Sio kwamba tulipuuzia, lakini ndege za vita zililenga makundi yote na ikawa sio rahisi kwa miezi kadhaa kuendesha gari.

Wapeni maziko stahiki kama mtaruhusiwa. Hamtaruhusiwa kuyafahamu majina yao hakika, lakini tafadhali msiwape namba kwa kubahatisha. Tumieni hisia zenu na wazikeni pamoja. Familia za wa-Syria zimetawanyika vya kutosha na hakuna anayependa kuzikwa peke yake.

Tulikuwa na mapinduzi pale. Waweza kuyalaani au kuyaomboleza. Ni pale katika miamba, ndani ya makaburi, katika ardhi na juu ya anga.

Katika kuta za makaburi tulishawahi kuandika: “Tuko hai, tutaendelea kusonga mbele,na ndoto yetu itaonekana”. Chukueni kila kilichosalia kwetu na endeleeni kuota. Muda mfupi ujao kila kilicho chenu kitataifishwa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.