Namna ya Kuandika kwa Ajili ya GV

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Habari ya GV

giphy (31)

Kabla ya kutuma andiko lako kwa ajili ya uhakiki, angalia maeneo yafuatayo:

  • Kichwa cha habari: Je, wasomaji watavutiwa na kichwa hicho cha habarina na kupenda kuisambaza habari hiyo kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na je, kina maneno muhimu yanayoweza kuonekana mtandaoni mtumiaji wa mtandao anapotafuta habari?
  • Utangulizi: Je, habari hiyo ina utangulizi unaovutia wenye maneno yasiyozidi kati ya 15-25 kwenye aya tatu za mwanzoni?
  • Picha: Je, juu ya habari hiyo kuna picha kubwa na nzuri yenye ukubwa angalau kuanzia 800×600 px? Na je, tuna ruhusa ya kuitumia picha hiyo? Je, ulihusisha maelezo yaliyopo kwenye picha na mahali ulipoitoa picha hiyo? Na je, maelezo hayo umeyaweka kwenye kipengele husika?
  • Mukhtadha: Je, umeoenyesha lengo letu la kueleza habari hiyo? Kwanini habari hiyo imejitokeza katika eneo husika na kwanini ni muhimu kwetu kuitoa? Je, umewasadiaje wasomaji wako kuelewa usuli wa habari hiyo?
  • Maoni: Je, umejumuisha twiti kati ya 1 mpaka 6 au maoni ya watumiaji wa mitandao ya kijamii? Husisha kwenye usuli wa habari na maoni ya mtu unayemnukuu. Je, anatumia jina halisi au anatumia jina la mtandaoni kuficha utambulisho wake –lazima tuliweke hilo wazi. Je, mtoaji wa maoni hayo ni mtalaam wa suala husika? Au ni mchekeshaji maarufu mwenye taarifa nyingi? Je, anafuatiliwa na watu zaidi ya elfu 10 kwenye mtandao wa twita? Tusiache kulisema hilo. Au ni shuhuda wa moja kwa moja wa tukio husika? Lazima tuseme wazi kwa nini sauti yake ni muhimu kunukuliwa.
  • Ujumbe Mkuu wa Kumalizia: Je, ungependa wasomaji wako wapate hisia gani wakati wanamalizia kusoma andiko lako? Je, unataka wasomaji waone ukubwa wa tatizo? Au unataka wawe na matumaini? Hakikisha maneno yako machache ya mwisho yanabeba ujumbe kwao
  • Vipengele: Je, katika andiko lako ulichagua kipengele kinachohusika na habari hiyo?
  • Mhutasari: Je, ulihusisha dondoo tofauti na utangulizi wa habari hiyo?
  • Mwonekano wa Picha: Je, ulikumbuka kuchagua muonekano wa picha uwe na ukubwa gani ?
  • Je, umehifadhi kwanza nakala ya HTML kwenye uwanja wa kuhariri kabla ya kutuma ili kusaidia endapo kutatokea makosa?
  • Je, umemjulisha mhariri wa eneo au lugha yako kwamba posti yako iko tayari kwa kupitiwa?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.