- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanahabari wa Mexico Aliyeuawa Cándido Ríos: ‘Silaha Zetu Hazirushi Risasi. Silaha Zetu Hurusha Ukweli’

Mada za Habari: Amerika Kusini, Mexico, Censorship, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi
Cándido Ríos Vázquez. Imagen ampliamente compartida en Twitter.

Cándido Ríos Vázquez. Picha iliyotumiwa kwa wingi huko Twitter.

Mwanahabari wa Mexico  Cándido Ríos, ambaye anafahamika kwa wenzake na watu wa kwao kama  “Pavuche,” aliuawa hapo Agosti 22, 2017, katika shambulio la risasi huko Hueyapan de Ocampo, Veracruz, [1] katika pwani ya mashariki ya Mexico, kulingana na vyanzo vya nyumbani [2].

Chazo huru cha habari Animal Político kilitoa taarifa zaidi kuhusu kifo chake [3]:

Ríos, conocido entre sus colegas como “Pavuche”, falleció mientras era trasladado al hospital debido a las heridas de bala de alto calibre que recibió, según dijeron a AFP fuentes conocedoras del caso.

Ríos, anayefahamika kama “Pavuche” miongoni mwa wenzake, amefariki wakati akisafirishwa kwenda hospitali baada ya kujeruhiwa kwa risasi AFP.

Jina la Ríos linaungana na orodha ya wanahabari  ambao wameshauawa nchini Mexico mwaka huu ambayo ni pamoja na Salvador Adame [4], Miroslava Breach [5]na Javier Valdez. [6]Kulingana na kikundi cha kutetea uhuru wa kujieleza Article 19, Ríos ni mwanahabari wa tisa [7]aliyeuawa nchini kwa mwaka 2017.

Ríos alikuwa mwanzilishi wa gazeti la kila juma La Voz de Hueyapan na alikuwa akiripotia gazeti la nyumbani  Diario Acayucan [8] kwa miaka kumi. Kazi yake ilikuwa inajumuisha kuandika habari za polisi na rushwa. Animal Político walitaarifu [3]:

El periodista era conocido por su larga trayectoria cubriendo nota roja, y por haber tenido conflictos con algunos exalcaldes de la región debido a su labor periodística.

Mwanahabari huyu alifahamika katika kazi yake kama mwandishi wa habari za uhalifu na kwa kuwa na migogoro na baadhi ya mameya  waliopita wa mji katika ukanda huo kutokana na kazi yake.

Mtumiaji wa Twitter Diana Gabriela alishirikisha video [9] aliyochagua ambayo Rios aliitengeneza mwenyewe, siku tisa tu kabla ya kuuawa, ambapo alitoa tuhuma nzito dhidi ya wanasiasa wa Hueyapan de Ocampo. Ndani ya video hiyo alisema kuwa: “Hatutumii bunduki. Wanatuua wakijua kuwa silaha zetu hazirushi risasi. Silaha zetu zinarusha ukweli.”

Cha kushitua ni kwamba  Ríos alikuwa chini ya ulinzi wa mamlaka za mji baada ya kupokea vitisho dhidi ya maisha yake kwa kazi yake ya uhabarishaji. Gazeti La Jornada limeripoti [12]:

Jorge Morales, de la Comisión Estatal de Atención y Protección a Periodistas, informó que Cándido Ríos tenía presentadas varias denuncias contra algunas autoridades municipales de la región, por agresiones a su persona.

Jorge Morales, kutoka Tume ya Kulinda Wanahabari aliripoti kuwa Cándido Ríos alitoa malalamiko kadhaa dhidi ya wanasiasa wa ukanda huo kwa kutishia maisha yake.

Kituo cha Habari Huffington Post kilielezea [13]:

Su afán por denunciar injusticias le ganó amplia popularidad entre los lectores, pero también enemigos como el exalcalde de Hueyapan, su pueblo natal, quien lo amenazó de muerte en numerosas ocasiones, según recuerda su colega y director del Diario de Acayucan, Cecilio Pérez.

Jitihada zake zisizokoma kukemea udhalimu vilimletea umaarufu miongoni mwa wasomaji, lakini pia maadui kama vile Meya wa zamani wa Hueyapanal, mji wa nyumbani kwao Ríos’ ambaye alimtishia kumuua mara kadhaa alisema mfanyakazi mwenza wa zamani Cecilio Perez, mkurugenzi wa Diario de Acayucan.

Wakati huo huo, chanzo cha habari MX Politico kilishea picha zake huko Twitter:

Vyombo vya habari nchini viliripoti kidogo sana kuhusu mauaji ya Ríos’. Vingine vilitoa taarifa zenye matoleo tofauti tofauti ya sababu za kuuawa kwakwe. Chanzo cha habari za mitandaoni  Milenio kilionesha maoni  [18]kutoka kwa afisa wa serikali ya Mexico aliyesema kuwa Ríos hakuwa mlengwa katika tukio alilouawa:

El periodista Cándido Ríos Vázquez no era el objetivo del ataque en el que murieron él y otras dos personas frente a una gasolinera en el municipio de Hueyapan de Ocampo, dijo Roberto Campa Cifrían, subsecretario de Derechos Humanos de la Secretaría de Gobernación.

Mwanahabari Cándido Ríos Vázquez hakuwa mlengwa wa shambulio ambalo yeye na watu wengine wawili waliuawa katika kituo cha mafuta huko Hueyapan de Ocampo, Veracruz, alisema Roberto Campa Cifrian, Naibu Katibu wa Sekretarieti ya Mambo ya Ndani na Haki za Binadamu.

Jaqueline Dorantes alishirikisha ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake: