- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwandishi wa Habari wa Thailand na Wakosoaji Dhidi ya Serikali ya Kijeshi Wakabiliwa na Makosa ya Uchochezi Kupitia Facebook

Mada za Habari: Asia Mashariki, Thailand, Censorship, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, GV Utetezi
[1]

Kutoka kushoto kwenda kulia: Pravit Rojanaphruk, Watana Muangsook, na Pichai Naripthaphan.

Wiki iliyopita, watumiaji watatu wa Facebook nchini Thailand walishitakiwa [2] kwa makosa ya uchochezi kufuatia kuikosoa serikali inayoongozwa kijeshi.

Mwanahabari nguli Pravit Rojanaphruk, Watana Muangsook wa Pheu Thai [3] chama cha siasa, na waziri wa zamani wa nishati Pichai Naripthaphan walitaarifiwa na polisi kuhusiana na makosa hayo ya uchochezi.

Jeshi lilijitwalia [4] madaraka mwaka 2014 na kuendelea kuliongoza taifa chini ya katiba iliyopitishwa mwaka 2016. mbali na kuvibana vyombo vya habari, serikali hii imekuwa ikiwashitaki watu kwa tuhuma za ama kumkahifu mtukufu Rais au serikali. Thailand inatumia sheria ya Lese Majeste (kutokumdhalilisha Kiongozianti-Royal Insult), ambayo wakosoaji wanaamini kuwa shetria hii inatumika vibaya na jeshi kwa lengo la kuwanyamzisha wakosoaji wa serikali.

Pravit, ripota mwandamizi wa tovuti ya habari Khaosod kwa Kiingereza, aliandika [5] mnamo Agosti 1, 2017 kile alichojifunza kufuatia kesi yake ya uchochezi:

NIlipokea simu kutoka kwa msaidizi wa wa kitengo cha Kukabiliana na Makosa ya Mstumizi mabaya Teknolojia akinitaarifu kuwa afisa wa polisi mwenye cheo cha Luteni Kanali ananishtaki kwa kosa la kukiuka sheria ya uchochezi kufuatia kuchapisha makala zinakadiriwa kufikia tano kwenye mtandao wa Facebook. Hata hivyo, nilisisitiza tena kuwa, nilikuwa ninaikosa serikali kwa lengo jema kabisa […] Nitaendelea kuikosa serikali batili hadi pale watakaponinyang'anya simu janja yangu.

Polisi hawakuweza kumfafanulia kuhusu makala ya Facebook aliyoiandika [6] na ambayo ilipelekea serikali kuiona kuwa ni ya uchochezi.

Pravit hapo awali ‘alialikwa’ na jeshi kwa ajili ya kupatiwa huduma ya namna ya ‘namna ya kurekebisha mwenendo’ [7]. Ushikiliwaji huu usio wa kawaida ni mbinu ya jeshi ya kukabiliana na wakosoaji wa serikali kupitia vyombo ya habari na majukwaa ya kitaaluma.

Akikutwa na hatia, Pravit anaweza kufungwa gerezani kwa kipindi cha hadi miaka 20.

Pichai, kwa sasa, nafanya kazi na waziri mkuu wa zamani, Yingluck Shinawatra [13], ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya rushwa [14]. Kwa mujibu wa Khaosod katika lugha ya English, Pichai alichapisha [2] ujumbe ufuatao kwenye facebook, ujumbe anadai kuwa aliundika [15] kwa ‘malengo mazuri’:

Ikiwa serikali haitafanyia kazi kwa wakati, hali ya uchumi itazidi kuzorota, kama ilivyo kwa chura ndani ya chungu ambacho taratibu kinaendelea kuchemka. Ninaimani kuwa serikali ya Thai na raia wake watalitambua hili bila kuchelewa, na hivyo kuwa kama chura aliyeruka kabla chungu hakijaanza kuchemka.

Watana ni mwanachama mwingine wa milki ya Yingluck ambaye anatuhumiwa [16] na polisi kwa kuipotosha jamii kuhusu mfumo wa mahakama na serikali ya kijeshi kupitia makala yake aliyoichapisha kwenye ukurasa wake Facebook.

Pichai na Watana walikuwa wanachama wa chama tawala kabla ya jeshi kuchukua madaraka mwaka 2014.

Wanasiasa hawa wawili walifunguliwa mashtaka wiki moja wakati Yingluck alipofika mahakamani kujibu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mpango wa mchele wa bei nafuu, jambo linalowafanya watu kujiuliza ikiwa tuhuma hizo zinalenga kuwanyamazisha wafuasi wa Yingluck.

Taarifa kuhusu kufunguliwa kwa kesi za uchochezi dhidi ya wakosoaji wa serikali ya kijeshi iliwafanya watumiaji wa twitter kutoa maoni yao kuhusu uminywaji wa uhuru wa kujieleza nchini humo:

Makala moja ya Twitter inamtaja Prayut, kingozi wa jeshi aliyeongoza mapinduzi ya mwaka 2014 na sasa ni Waziri Mkuu wa nchi:

Kufunguliwa kwa kesi hizi tatu tofauti— kwa wiki iliyopita pekee — dhidi ya wakosoaji wakuu wa serikali ya kijeshi, kunaongeza sitontofahamu ikiwa serikali ya kijeshi ipo tayari kurudisha utawala wa kiraia na wa kidemokrasia nchini.