- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mchora Vibonzo vya Kisiasa Nchini Malaysia Zunar Aishitaki Polisi Kwa Kumkamata Kinyume cha Sheria na Kushikilia Vitabu

Mada za Habari: Asia Mashariki, Malaysia, Censorship, Maandamano, Sanaa na Utamaduni, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, GV Utetezi
[1]

Zunar anaitaka polisi irudishe vitabu  1,187 na tisheti 103 walivyochukua wakati walipomkamata hapo Desemba 17, 2016. Picha kutoka Ukurasa wa Mashabiki wa Vibonzo wa Zunar.

Mchora vibonzo wa Malaysia Zulkiflee S.M. Anwarul Haque, maarufu zaidi kama  Zunar [2], amefungua [3] kesi dhidi ya polisi kwa kumkamata na kuchukua  vitabu vyake vya vibonzo na tisheti hapo Disemba 17, 2016.

Zunar anawatuhumu polisi kwa kumkamata bila kufuata sheria na kutaifisha jumla ya vitabu 1,187 na tisheti 103 wakati wa tamasha aliloliandaa ili kukutana na mashabiki wake na kukusanya fedha za kutunisha mfuko.  Anaelezea [4] sababu za yeye kuchukua hatua za kisheria:

Vitabu vyangu havijafungiwa na nilikuwa naviuza tu kwa mashabiki wangu wakati wa tukio la kukusanya fedha za kutunisha mfuko. Kuna tatizo gani hapo?

Zunar  ameshakamatwa [5] mara kadhaa miaka michache iliyopita na akashtakiwa kwa uchochezi wa vibonzo vyake vilivyokuwa vikizikosoa sera za serikali, matumizi mabaya madaraka kwa serikali ya mseto ambayo imeshikilia siasa za Malaysia tangu 1950 na kukatiza haki na uhuru wa raia. Vitabu vingi vya vibonzo vya Zunar vimeshashikiliwa  na mamlaka kwa madai ya kutishia usalama wa nchi. Zunar amefahamika ndani na nje ya Malaysia kama mpigania uhuru wa habari.  Amepata tuzo ya utambulisho toka [6] Shirika la Haki za Binadamu, Kamati ya Mtandao wa Kimataifa wa Kulinda Haki za Wanahabari na Wachora Vibonzo.

Kukamatwa kwake hapo Disemba kulifungamanishwa na upelelezi wa polisi dhidi yake kwa Kifungu 124C cha adhabu kwa ” shughuli mbaya kwa demokrasia ya bunge.”

Alihojiwa kwa masaa sita na aliachiwa baada ya polisi kumuambia kuwa “watatumia sheria kuvifungia vitabu vyake vyote.” Alitoa [7] kauli hii muda mfupi baada ya kuachiliwa kwake:

Ninapenda kutoa msimamo wangu: kipaji sio zawadi ila ni wajibu. Ni wajibu wangu kama mchora vibonzo kufunua rushwa na matendo yasiyo haki. Je naogopa gereza? Ndio, lakini wajibu ni mkubwa kuliko hofu hiyo. Mnaweza kufungia vitabu vyangu, mnaweza kufungia vibonzo vyangu lakini hamuwezi kuifungia akili yangu. Nitaendelea kuchora mpaka tone la mwisho la wino wangu.

Zunar anahusishwa na  kashfa ya rushwa [8] iliyomuhusisha waziri Mkuu na 1MDB,  kampuni inayomilikiwa kwa ubia kati ya serikali na mtu binafsi. Waziri mkuu anatuhumiwa kuweka mfukoni dola milioni 680 kupitia malipo ya ajabu yaliyofanywa na 1MDB.

Mwanasheria wa Zunar, N. Surendran, anasema kufungua kesi dhidi ya polisi inakusudia kuionya [9]mamlaka kuhusu kukamata kwingine kusipo kwa kisheria:

Hakutakuwa na uvumilivu kwa aina ya tabia hii isiyo ya kisheria dhidi ya mtu ambaye kosa lake pekee ni kuikosoa serikali. Hiyo ni haki ya kidemokrasia ya kila m-Malaysia.

Zunar anaishinikiza polisi warudishe vitabu vyake na tisheti