- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mamlaka ya Habari ya Thailand Yaufungia Mtandao wa TV Uliomwita Kiongozi wa Junta Dikteta

Mada za Habari: Asia Mashariki, Thailand, Censorship, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vyombo na Uandishi wa Habari
[1]

Peace TV imefungiwa kwa mwezi mmoja. Picha kutoka Shirikisho la Muungano wa Vyombo vya Habari la Kusini Mashariki ya Asia, imetumika kwa ruhusa. 

Tume ya Taifa ya Habari Thailand (NBTC) imekinyang'anya [2] leseni kwa mwezi mmoja kituo kimoja cha televisheni ambacho kimekuwa kikikosoa sera za serikali inayoongozwa kijeshi.

Ikiwa imesainiwa hapo Agosti 9, 2017, amri ya NBTC itaanza kufanyiwa kazi pale barua itakapofikiswa kwa Mtandao wa Peace TV.

Peace TV ina uhusiano na Muungano wa Kidemokrasia Dhidi ya Udikteta (UFDD) kundi linalojulikana pia kama  “Shati Jekundu” [3] ambalo viongozi wake wakuu ni wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra. Baadhi ya “shati jekundu” wanafahamika kama wakosoaji wa  sheria ya Lese Majeste (kinyume na watukanaji wa Mfalme), ambayo serikali imekuwa ikiitumia kuwahukumu wanaharakati na wanasiasa walio kinyume na Junta.

Jeshi la Thailand lilinyakua [4] mamlaka mwaka 2014 na limebakia madarakani kupitia katiba iliyoitengeneza. Liliapa kurudisha mamlaka ya kiraia pale marekebisho ya kisiasa na uchaguzi yatakapo tekelezwa. Tangu 2014, junta wamekuwa wakividhibiti vyombo vya habari na kuwakamata watumiaji wa mitandao ya intaneti wakituhumiwa kwa [5] kutukana mamlaka.

NBTC ilisema kuwa Peace TV ilivunja sheria pale iliporushwa vipindi vilivyoidharau Mamlaka ya Kifalme ya Kikatiba, usalama wa Taifa na “Maadili mema” hapo Julai.  Hata hivyo, haikubainisha ni sehemu zipi za vipindi hivyo zilizochochea umma kuipinga serikali.

Hii ni mara ya tatu kwa Peace TV kufungiwa kurusha matangazo na NBTC. Kipindi kilichopita ilikuwa ni  Aprili 2015  na Julai 2016 kwa madai ya kutishia usalama wa nchi.

Baadhi wanaamini kuwa Peace TV ilifungiwa kwa sababu ilidhubutu kumuita Waziri Mkuu wa zamani  Prayut Chan-o-cha dikteta:

Mamlaka za #Thailand [6] zimeipiga kofi @peacetvnews [7] kwa kuwafungia kwa siku 30 kwa kumuita kiongozi wa #junta [8]

Shirikisho la Muungano wa Vyombo vya Habari la Kusini Mashariki ya Asia lilihoji [1]kuhusu uongozi mkali wa NBTC kwa sababu itaathiri vipindi vyote na watumishi wa Kituo hicho cha televishenil:

Tunaona amri ya kufungiwa ilikuwa kali mno, hasa kwa kuwa NBTC ilivitambua vipindi maalum na tarehe maalum viliporushwa hewani na kuvunja sheria za habari za Thailand. Amri inawaadhibu kituo kizima vikiwamo vipindi vyote bila kujali mahudhui, na watumishi wote bila kujali majukumu yao.

Kundi hili lilionya pia kuwa amri ya  NBTC itaenda mpaka katika udhibiti wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Thailand:

Mamlaka pana na yenye kufagia kama hii hasa chini ya sheria za mara kwa mara lazima itumike kwa kujizuia na kwa uwiano, ikizingatiwa kuwa inaweza kutengeneza utangulizi wa kuzuia uhuru wa habari na Haki za umma kusikia na kufahamu habari kutoka pande zote za mijadala ya kisiasa katika jamii ya Wa-Thai.

Maafisa wa Peace TV walisisitiza [12]kuwa sehemu za vipindi vilivyoelezewa na NBTC havikuueleza umma kupingana na junta. Waliongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja wa kufungiwa, vipindi vya Peace TV vitakuwa vikirushwa mubashara kupitia Facebook.

Pia wamehusianisha amri ya kufungiwa kwao na kusikilizwa kwa shauri la rushwa dhidi ya Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra hapo Agosti 25. Lakini Waziri Mkuu Prayut alikana [13] kuwa Televisheni hiyo ilifungiwa ili kuwanyamazisha vyombo vya habari vinavyowaunga mkono “Shati Nyekundu” wakati wa shauri la Yingluck. Alisema kuwa ingekuwa hili ndilo kusudio la serikali, basi vyombo vyote vya habari vingefungiwa na NBTC.