Video ya Muziki Inayoigiza Utawala wa Junta Rule Nchini Thailand

Picha iliyopigwa kwenye video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Bendi maarufu ya Pop nchini Thailand imeachia video ya muziki ikiigiza mtindo wa Junta ambaye alitwaa madaraka mwaka 2014 na anaendelea kutawala nchi hiyo kinyume na ahadi yake ya kurejesha utawala wa kiraia.

Wimbo mpya wa Bendi hiyo iitwayo Tattoo Colour ‘Dictator Girl’ unahusiana na kijana anayeelezea sheria zake kwa msichana wake.

Ingawa hauhusiani moja kwa moja na siasa, wimbo huo unazungumzia unazungumzia kwa kificho utawala wa kijeshi unaoendelea.

Bendi hiyo inasifika na mashabiki na watumiaji wengine wa intaneti kwa ujanja wake wa kuielezea hali ya mambo nchini humo.

Video ya wimbo huo ilitawanyika haraka sana mtandaoni. Wakati makala hii ikiandaliwa, video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook tayari imetumwa mara 1,254 na kuvutia watumiaji 8,800.

Mpaka sasa, video hiyo bado inapatikana kwenye mtandao wa YouTube jambo ambalo si la kawaida kwa kuzingatia kwamba serikali ina tabia ya kuchukua hatua upesi na kuyazuia maudhui yoyote yanayoikejeli serikali.

Mwezi uliopita, hata kipande cha video ya Charlie Chaplin, kiitwacho ‘The Dictator’ kilifungiwa nchini Thailand baada ya wanaharakati kuuhamasisha umma kuitazama.

Video hiyo inaweza kutafsiriwa kama namna ya kuelezea siasa za Thailand kwa ubunifu na vicheesho, hususani kuhusu mwenendo wa mmabo chini ya utawala wa Junta. Tazama pihca hizi zilizopo kwenye video hiyo zinavyohusiana na masuala ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kwa zaidi ya miaka mitatu.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

‘Sheria 44 za msichana’ zinaweza kuwa na maana ya Kifungu cha 44 kwenye Katiba ya Muda kinachompa mamlaka makubwa mkuu wa majeshi kuamua masuala muhimu ya kitaifa.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Sheria namba 11: ‘Rekebisha Mtazamo Wako’, inahusiana na is about the infamous ‘attitude-adjustment’ maelekezo ya ‘kubadili mtazamo’ yaliyotolewa kwa waandishi wa habari, wanafunzi, wanazuoni, wanasiasa, na wengine wanaoonekana kuwa wakosoaji wakubwa wa Junta.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Picha hiyo juu inaashiria utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao yenye vipengele vyenye tafsiri zisizowazi na pana vinavyotumiwa na serikali kuwakamata wanaharakati na wakosajia wengine wa serikali. Kikosi cha jeshi kinafuatilia maudhui ya mtandaonina kuwashitaki watu wanaotuhumiwa kuutukana utawala huo. Thailand inatumia sheria ngumu ya Lese Majeste (Matusi dhidi ya Ufalme).

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Mnamo Mei 20, 2014, sheria ya kijeshi ilitangazwa nchini Thailand. Siku mbili baadae, jeshi lilifanya mapinduzi.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Moja wapo ya masuala yanayokwamisha utawala wa Junta ni uamuzi wake wa kununua nyambizi ghali bila kujali wachambuzi wa usalama walioonya kwamba ununuzi huo haukuwa wa lazima na ulikuwa ni upotevu wa bure wa fedha za walipa kodi.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Hata suala la watu waliotekwa na kutupwa ndani ya gari jeusi kabla ya kupelekwa kwenye makambi ya utesaji lilionekana kwenye video hiyo.

Picha ya video ya muziki iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Vyombo vya habari vinaendelea kukabiliana na sheria kali; baadhi ya waandishi wa habari wamewekwa ndani kwa kudaiwa kusababisha “mtafaruku” kwenye jamii, na watuaji wa Intaneti wanakabiliwa na vifungo virefu gerezani kama watautukana utawala wa nchi hiyo.

Wakati huo huo, tangazo la kuutambuliza wimbo huo unaonesha waimbaji wa bendi hiyo wakitoa ishara ya heshima kwa wimbo wa ‘Hunger Games’ iliyotumiwa na wanaharakati wanaopinga mapinduzi wakati wa maandamano ya mwaka 2014.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.