
Picha na Héctor Vivas (@hectorvivas) kwa mtoa taarifa wa Derecho (@DerechoInformar). Imetumika kwa ruhusa.
Uhuru wa wa vyombo vya habari umeendelea kukutana na changamoto inayoibuka duniani kote. Nchini Mexico, hatari ya kutoa habari imefikiwa viwango vipya.
Mamlaka zenye nguvu- kuanzia kwa maafisa wa serikali, kwa wasimamizi wa sheria, mpaka kwa wakuu wa magenge ya wauza dawa za kulevya kwa zamu na kwa utaratibu maalum wameendelea kuwashughulikia waandishi wa habari na vyanzo vya habari kuwazuia wasichunguze rushwa na vurugu zinazohusianishwa na dawa za kulevya nchini humo. Juhudi za kuvinyamazisha vyombo vya habari hufanywa katika kivuli kwa kuwalazimisha wahanga kuchagua kati ya kujidhibiti binafsi au uhamisho wa lazima au kuhatarisha maisha yao wakiwa wanafanya kazi zao.
Bado, waandishi wa habari na wanahabari wa kiraia wameendelea kutoa taarifa kutoka katika maeneo yenye migogoro katika kanda zote za nchi. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kitengo cha Haki za Binadamu cha Universidad Iberoamericana, zaidi ya makaburi elfu ya pamoja yamepatikana yakiwa na miili 2,014 idadi ambayo ni kubwa kuliko iliyotolewa na maafisa wa serikali. Mapigano ya risasi baina ya vikundi vyenye silaha yameacha idadi kubwa na ya kutisha ya vifo vilivyohesabiwa. Ndani ya miezi 4 ya mwanzo wa mwaka 2017, Mexico imevunja rekodi ya nyuma ya mauaji rekodiya matukio 7,727, matukio 392 zaidi, ambayo ni asilimia 5.3% zaidi ya 2011, ambao ni mwaka uliokuwa na rekodi ya matukio ya kikatili zaidi hapo nyuma, hii ni kulingana na Katibu Mtendaji wa Usalama wa Taifa.
- Salvador Adame ni mwanahabari wa saba kuuawa nchini Mexico kwa mwaka 2017
- ‘Hapana kwa Ukimya': mauaji ya Javier Valdez yanaonesha hatari inayoendelea dhidi ya wanahabari wa ki-Mexico
Mwanahabari Javier Valdez, mhariri na mwandishi wa chanzo cha habari cha nyumbani cha Ríodoce, aliuawa hapo Mei 15, 2017. Valdez, aliyekuwa anafikiriwa kama mtaalamu kinara katika masuala ya usafirishaji wa dawa za kulevya nchini Mexico, amekuwa mwanahabari wa sita kuuawa nchini Mexico tangu mwaka huu wa 2017 umeanza.
Valdez aliifahamu hatari ya kazi yake nchini Mexico, lakini hakukata tamaa. Pia hata wenzake wengi:
Acha watuue sisi wote, kama hiyo ndiyo hukumu ya kifo kwa kutoa taarifa za jehanamu hii. Sio Ukimya – Javier Valdez

‘Huwezi kuuua ukweli kwa kuwaua waandishi wa habari”. Picha na Article 19 huko Flickr. Imetumika chini ya misingi ya kuwaenzi waandishi wa habari waliouawa. Picha na Article 19. Imetumika chini ya CC BY-NC 2.0.
Anabel Flores, Ricardo Monlui, Cecilio Pineda, Miroslava Breach, Javier Valdez, Salvador Adame na makumi zaidi ya waandishi waliouawa ni ushuhuda wa kuwa vitisho mara zote huzaa matunda. Wanahabari wanauawa majumbani mwao, wengine wakielekea kazini, mara kwa mara mchana kweupe na madhara ni kidogo kwa washambuliaji hao. Kwa mujibu wa Article 19, wanahabari 107 (akiwamo Salvador Adame) wameuawa ndani ya nchi tangu mwaka 2000. Hakuna shaka ndio maana Mexico imetambulishwa kama moja ya nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari.
Wakati baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea kufanya kazi katika hali hii, mauaji na hofu iliyowagubika imeacha tundu jeusi la taarifa nchini, ikiwasukuma baadhi ya waandishi wa habari kuepuka kugusa habari hatarishi na kupunguza uwezo wa jamii kupata taarifa kuhusu rushwa ndani ya serikali, unyanyasaji katika mashirika, ukatili wa makundi mbali mbali na uvunjifu wa haki za binadamu
Rushwa na ukatili umeyafikia matawi yote ya serikali ya Mexico na kufanya iwe ngumu kutofautisha uhalifu wa kupanga na ule wa watumishi wa umma. Katika hali kama hii inakuwa ngumu kufahamu ni nani hasa anatakiwa kuwalinda na kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari.
- Vita vya dawa za kulevya nchini Mexico vinamfanya kila mmoja kuwa Mlengwa
- Wajibu wa Vyombo ya Habari Mexico ‘Umeifungia’ Demokrasia
- Mexico: “Sisi ndio Tatizo Kwa Sababu Tunaisumbua Serikali na Wauza Dawa za Kulevya
Wakati huo huo, tangu kuanza kwa muhula wake, Rais Peña Nieto amejaribu kuiweka Mexico kuwa chaguo la juu katika uwekezaji wa fedha na kama mfano wa kuigwa katika demokrasia na uhuru katika nchi za Amerika. Husisitiza kuwa serikali yake imejizatiti katika kulinda vyombo vya habari. Lakini katika nyakati tofauti tofauti, wakati kashfa ya rushwa inapokuwa wazi kwa wananchi Rais na maafisa wake hukataa au kupuuza malalamiko yanayohusu rushwa wakati wale wanaoyaweka masuala hayo wazi huitwa waongo, hushtakiwa, au hufukuzwa kazi.
Wakati taarifa zisizofurahisha za kinachoitwa vita dhidi ya dawa za kulevya zinapofuata mkondo wake katika vyombo vikuu vya habari, mara zote shukrani kwa juhudi za waandishi wa nyumbani ni kutishiwa na serikali pamoja magenge ya uhalifu . Na tamko lililotolewa na Article 19 katika kikao cha 35 cha kamati ya Umoja wa Mataifa Haki za Binadamu linasema:
Tunasikitika kuwa serikali imekataa kutambua hadharani, hata kulaani mashambulizi dhidi ya wanahabari yaliyofanywa na; au kwa amri ya maafisa wa serikali. Hii inajumuisha pale wanahabari wako chini ya uangalizi wa mamlaka za shirikisho. Serikali imerusha lawama zote za mashambulio haya kwa magenge ya uhalifu lakini ARTICLE 19 imegundua muunganiko uliopo baina ya maafisa wa serikali na mashambilio hayo kwa asilimia 53% ya mashambulio yaliyorikodiwa 2016.

Madhabahu kwa ajili ya kuwaenzi wanahabari wa Mexico waliouawa. Photo by Article 19 on Flickr. Imetumika chini ya leseni ya CC BY-NC 2.0.
Mwanasheria mkuu asiyefanya kazi
Taifa la Mexico lina ofisi iliyojitoa kipekee katika nadharia ya kutafuta haki katika uhalifu uliofanyika dhidi ya wanaofanya uhabarishaji au wengine wanaofanyia kazi uhuru wa kujieleza bila mipaka ya kisheria.
Ofisi maalum ya mwendesha mashitaka ya uhalifu dhidi ya uhuru wa kujieleza (FEADLE) inafanya kazi chini ya Mwanasheria Mkuu wa Mexico. (PGR).
Hata hivyo, FEADLE ni tawi moja wapo lenye mfumo wa urasimu mkubwa nchini, unaonyonya kwa sehemu kubwa rasilimali za Taifa wakati inatoa mrejesho finyu. Mwaka 2017 bajeti iliyopangwa inakadairiwa kuwa ni dola milioni 1, wakati kwa mwaka 2016 walipokea kiasi cha dola milioni 1.4.
- #LeyTelecom: Mahakama kuu ya Mexico yaridhia mpango wa kufuatilia aliko mtu uhifadhi wa takwimu kubwa
- Muswada wa sheria za mitandao wa Mexico umekufa. Lakini ni kitu gani watunga sheria watakachofikiria baadaye
Kati ya mauaji saba yaliyofanywa dhidi ya waandishi wa habari kwa mwaka huu tu, hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa. Tovuti huru ya Wamexico Animal Político iliripoti:
En algo más de seis años – de julio de 2010 al 31 de diciembre de 2016 – se registraron 798 denuncias por agresiones contra periodistas.
Pues bien, de esas 798 denuncias, de las cuales 47 fueron por asesinato, la FEADLE informó en respuesta a una solicitud de transparencia que solo tiene registro de tres sentencias condenatorias: una, en el año 2012; y otras dos en 2016. O en otras cifras: el 99.7% de las agresiones no ha recibido una sentencia.
Ndani ya miaka karibu sita kuanzia Julai 2010 hadi Disemba 31, 2016, kulikuwa na taarifa ya mashambulizi dhidi ya wanahabari 798.
Kwa hiyo, nje ya malalamiko haya 798, 47 yalikuwa ni ya mauaji, FEADLE iliripoti ikitaka uwepo uwazi kwamba kuna hukumu tatu pekee zilizosajiliwa: moja mwaka 2012 na nyingine mbili mwaka 2016. Kwa maneno mengine ni kwamba 99.7% ya mashambulizi hayakutoa mwelekeo wa kesi za jinai.
Hakuna mtumishi wa umma yeyote ambaye alishawahi kuchukuliwa hatua kwa ukosefu wa haki katika jambo hili. Hakuna malalamiko yalishatolewa kuamua sababu ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu kushindwa kwa kiwango kikubwa kuwafikisha wauaji mbele ya sheria.

Kwenye Ukurasa wa mbele wa gazeti: “Uandishi wa Habari chini ya Rais Calderón, biashara hatari sana”. Picha na Article 19 kupitia mtandao wa Flickr. Imetumika kwa leseni ya CC BY-NC 2.0.
Upelelezi
Waandishi wa habari sio tu wanakumbana na ukosefu wa ulinzi, pia wako chini ya uangalizi mzito wa serikali ya Mexico.Taarifa za hivi karibuni zinathibitisha kuwa serikali imekuwa ikitumia zana za kupeleleza kwa nia ya kuwafuatilia wanaharakati, wanasheria na wanahabari bila kuwa na ruhusa ya mahakama, na hii sio halali nchini Mexico.
Zana hizi zilikusudiwa kutumika dhidi ya uhalifu, zimekuwa zikitumika kinyume kwa wananchi kuwazuia kupata ukweli na kuviweka vitendo vya rushwa hadharani. Pia Article 19, ililirejea suala hili pia katika tamko lake kwenye Baraza la Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa:
Kati ya mashambulizi 426 dhidi ya wanahabari tuliyoyarekodi mwaka uliopita, 72 yalikuwa mitandaoni na wanahabari wanawake na wanablogu waliathirika kwa kiasi kikubwa. Ufuatiliaji nao ni suala lingine: mashirika mengi yamejiondoa kwenye Muungano kwa Serikali iliyo Wazi (OGP) kwa sababu ya shutuma za kupelekwa kwa zana pelelezi kulikofanywa dhidi ya mashirika ya kutetea Haki za Binadamu na wanahabari.
- Ni kwa jinsi gani serikali ya Mexico inawaweka wananchi wake chini ya ufuatiliaji maalumu
- Mwanasheria mkuu wa Mexico alinunua kwa siri zana za kupeleleza zenye gharama ya juu (Tena)
- Mexico ilikuwa inadukua Timu namba moja mteja wa zana za kupeleleza
Mexico imekuwa kituo kikuu cha soko la teknolojia za ufuatiliaji Amerika. Mikutano ya biashara imekuwa ikifanyika kwa mwaka na uhusiano baina ya watengenezaji, wasambazaji na serikali ya Mexiko umeimarika haraka kwa kipindi chote cha muhula wa Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto. Upelelezi huru na wa kihabari uliofanywa na mashirika ya kiraia pamoja na habari mbalimbali zilizovuja ndizo zilizoweka wazi uhusiano huo hapo 2013.
Uhalifu na vitisho dhidi ya wanahabari
- Salvador Adame ni mwanahabari wa saba kuuawa nchini Mexico mwaka 2017 (June 27, 2017)
- ‘Hapana kwa Ukimya': Mauaji Javier Valdez yanaonesha hatari inayoendelea dhidi ya wanahabari wa ki-Mexikoy (May 22, 2017)
- Ripoti ya Jamii ya Mitandaoni: Wanahabari wa ki-Mexico walitishiwa mtandaoni, kisha Wakauawa (April 20, 2017)
- Mauaji ya wanahabari Mexico yanafufua Hasira juu ya ukatili unaofanywa dhidi ya Wanahabari (March 26, 2017)
- Anabel Flores anakuwa mwanahabari mwingine tena kutoka Mexico Veracruz aliyeuawa (February 22, 2016)
- Unaweza pia kudai haki kwa ajili ya wanahabari waliouawa Mexico (August 25, 2015)
- Tishio kubwa kwa wanahabari wa Mexico sio Magenge ya wauza dawa za kulevya tena (August 4, 2015)
- Wanahabari 14 kutoka Veracruz, Mexico wameshauawa katika kipindi cha utawala wa Gavana Duarte (August 4, 2015)
- Ukandamizaji wa Vyombo huru vya habari Mexico vyatishia redio ya asili huko Oaxaca (June 12, 2015)
- Fuatilia uchaguzi wa muhula wa kati wa Mexico kwa #VunjaHofu (June 8, 2015)
- Shajala ya Mwanahabari Pedro Canché Herrera, ‘Mfungwa wa Dhamiri’ ndani ya Mexico (March 9, 2015)
- Nchi hatari zaidi kwa wanahabari kutoka Ulimwengu wa Magharibi (February 13, 2015)
- Wanahabari wa kiraia walitekwa na kuuawa nchini Mexico kwa kutoa habari za magenge ya uhalifu (October 17, 2014)
Udhibiti, Ufuatiliaji na Udanganyifu wa Serikali
- Mradi wa Picha unawaomba wa-Mexico kamwe wasisahau Uhalifu ambao haukuadhibiwa (March 18, 2017)
- Ripoti ya Watumiaji wa Mtandao: Ndani ya Kenya na Mexico wananchi walihisi Udanganyifu wa Serikali, Twitter (February 16, 2017)
- Vita ya Alama Ishara: Inatengeneza ramani ya mazungumzo yaliyoigubika bei ya gesi Mexico (February 15, 2017)
- Utata wa ‘Sheria ya Mawasiliano’ Mexico sasa uko mahakama Kuu (April 27, 2016)
- Kutana na kampeni ya kulipiwa na watu dhidi ya udhibiti na Bots (April 6, 2015)
- Barua ya Pedro Canché Mfungwa wa Dhamiri kwa mwanahabari Carmen Aristegui (March 26, 2015)
- Bila Carmen Aristegui, Mawimbi ya hewa kwa Mexico hayako sawa tena (March 23, 2015)
Global Voices itaendelea kuripoti juu ya matukio haya na kazi za wanahabari wa nyumbani, wanahabari wa kiraia na watumiaji wa mitandao ya jamii watakaoviweka vitisho hadharani. Tunatafuta kuwawezesha na kuwalinda wote ambao wamejitoa kueleza habari zinazojiri Mexico.