Mkutano wa Wapoland Kudai Mahakama Huru Dhidi ya Marekebisho Yanayofanywa na Chama Tawala

Wakazi wa Warsaw wakiwa wamekusanyika mbele ya Ikulu. Picha na Anna Gotowska, CC-BY.

Mwaka 2017 ni karne moja tangu kuundwa kwa mahakama kuu ya Poland, lakini badala ya kusherehekea wa-Poland wanaandamana barabarani kwa ajili ya kutetea Uhuru wa mahakama.

Chama cha Utawala wa Sheria na Haki (PiS) ambacho kimekuwa madarakani kwa mwaka mmoja na nusu sasa, kimekuwa kikiingilia na kuchukua mamlaka ya Mwendesha Mashtaka wa Umma, Baraza la Katiba Usuluhishi wa Katiba na Baraza la Sheria la Taifa ambalo ndio huteua na kuwapandisha vyeo majaji.

Na sasa chama tawala kimeyaelekeza macho yake kwa Mahakama Kuu. Mabadiliko kadhaa ya kisheria yalifanyika wiki iliyopita na kupigiwa kura na kamati ya bunge Julai 18, ambayo yaliwaondoa papo hapo watumishi wa kada ya juu ya jopo la rufaa nchini Poland, ambapo lina majaji wa juu 83. Watu hao wataondolewa siku moja baada ya sheria hiyo kupitishwa. Upendeleo pekee utafanywa na Waziri wa Sheria, pia mwanachama wa Sheria na Haki. Baraza la Sheria la Taifa lililotajwa hapo kabla, chini ya mamlaka ya chama litajaza nafasi itakazoachwa wazi.

Mahakama Kuu iliyofanyiwa marekebisho itakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya rufaa zote za madai ya kiraia na kesi za jinai. Muswada huo pia unatoa mwanya wa kuundwa kwa kitengo cha nidhamu ndani ya mahakama Kuu, ambacho kitakuwa kikisimamia na kuchukua hatua dhidi ya makosa yote yatakayofanywa na majaji wa nchi nzima.

Kwa namna ya kushangaza, wakati muswada ukiendelea kujadiliwa hapo Julai 18, Rais Andrzej Duda, mwanachama wa zamani wa Chama cha Sheria na Haki, alitangaza kuwa hatatia saini muswada unaodhibiti Mahakama Kuu mpaka pale marekebisho ya muswada wake mpya dhidi ya Baraza la Sheria la Taifa uliopitishwa wiki moja kabla utakapokubaliwa. Marekebisho haya yanatoa muongozo kuwa wanachama wa baraza lazima wachaguliwe na tatu ya tano ya wabunge wote, badala ya mapendekezo ya awali ya muswada huo, na hii inafanya iwe vigumu zaidi kwa wawakilishi wa Haki na Sheria kuchagua wagombea wao. Hata hivyo, wengine wanadhani kuwa sheria mpya haipo kikatiba na kusema pendekezo la Rais likipokelewa hakuna kitakachobadilika.

Kwa kuyajibu hayo, wakazi wa Warsaw na miji mingine mikuu ya Poland waliingia mitaani wakimtaka Rais apeleke muswada huo kwenye kura ya veto. Makusanyiko hayo yalikuwa muendelezo wa maandamano yaliyoanza mwishoni mwa juma na kuongezeka zaidi siku bunge lilipokuwa linajadili kuhusu muswada huo wenye utata.

Waandamanaji walikusanywa na Chama cha Majaji Poland “Iustitia” na Akcja Demokracja (Demokrasia kwa Vitendo) ndani ya miji 33 ya Poland.

Video ya hapo chini, ilichukuliwa na mmiliki wake hapo Julai 18, ikionesha washiriki wakiimba wimbo wa Taifa la Poland huko Warsaw:


Na katika video hiyo wakazi wa Warsaw walipiga kelele kuwa “Tunataka Veto! Mahakama Huru!”

Alama ishara zilizoanzishwa na Akcja Demokracja ni pamoja na #ŁańcuchŚwiatła (inamaanisha”mnyororo wa nuru”), #wolnesądy (inamaanisha “Mahakama Huru”) na #chcemyweta (“tunataka Veto”).

Mjadala motomoto ndani ya Bunge ulidumu mpaka usiku wa manane, kukiwa na kundi dogo linalopinga kupitishwa kwa muswada wa Mahakama Kuu. Kura za mwisho inatarajiwa zitapigwa hapo Julai 19.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.