Mamlaka za Uturuki Zawatia Kizuizini Wapigania Haki za Binadamu Maarufu Wakiwa Kwenye Warsha ya Uwezeshaji

Sita kati ya wapigania Haki za Binadamu waliowekwa kizuizini Julai 5, 2017. Picha zimetumiwa kwa mapana katika mtandao wa Twita chini ya alama ishara ya #İnsanHaklarıSavunucularınaDokunma.

Wapigania Haki za Binadamu nane wa nchini Uturuki Eight of Turkey's best-known human rights defenders were walikamatwa wakati wakiwa kwenye semina na usalama na usimamizi wa taarifa za kidigitali katika moja ya visiwa vya Istanbul, Buyukada, hapo Julai 5.

Wawezeshaji wawili pia walikamatwa pamoja na wapigania Haki hai. Polisi walimuweka kizuizini kwa muda mmiliki wa hoteli ambapo warsha hiyo ilikuwa inafanyika. Kati ya hao waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu Uturuki, Idil Eser.

Chanzo huru cha habari cha Bianet kiliripoti kuwa polisi waliovalia kiraia walivamia warsha hiyo, kuwaweka kizuizini washiriki na kuchukua vifaa vya kielektroniki zikiwemo kompyuta na simu za mkononi. Raia hao tisa wa Uturuki watawekwa kizuizini kwa siku saba kabla ya kufunguliwa mashitaka.

Chini ya mwezi mmoja uliopita Mwenyekiti wa Shirika la Haki za Binadamu la Uturuki, Taner Kilic aliwekwa aliwekwa rumande gerezani. Shirika la Haki za Binadamu limeachia waraka hapo Julai 6:

kizuizi pasipo mawasiliano kwa (Idil Eser) na wapigania Haki za Binadamu wengine waliokuwa wanahudhuria mafunzo ya kawaida, ni utumizi mbaya uliopitiliza wa sheria na inaonesha ni hali ya namna gani inayowakumba wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini. Idil Eser na wote waliowekwa kizuizini naye, lazima waachiwe huru haraka na bila masharti.

Muitikio wa nyumbani na ule wa nje umekuwa wa haraka, na wanaowaunga mkono kupitia Twitter wanashinikiza kuachiliwa kwa wanaharakati hao nane, ambao ni wataalam katika sekta zao wakitumia hashatag za #İnsanHaklarıSavunucularınaDokunma na #freehumanrightsdefenders.

Hakuna taarifa zimetolewa kwa mawakili, wanahabari na wanasheria. Wanajifanya kuwa walivamia shirika fulani hivi muhimu na la hatari sana.

Shirika la habari linaloiunga serikali mkono Ahaber kwa haraka lilianza kukemea wanaharakati hao kama ” washirika” wa tukio kama hilo lilitokea 15 Julai 2016 kabla ya jaribio la mapinduzi nchini Uturuki:

15 TEMMUZ TOPLANTISINI AKILLARA GETİRDİ ​Büyükada'da bir otelde, 15 Temmuz darbe girişiminin yapıldığı gün giriş yapan, çoğunluğu yabancı 17 kişilik grup, 2 gün boyunca toplantı yapmıştı. Toplantıda CIA'ya çalışan ABD'li profesör Henri Barkey'in de bulunması dikkat çekmişti.

KWENYE MAWINDO YA WASHIRIKA

Kundi la watu wapatao 17, likiwa na raia wa kigeni, walipanga kwenye hoteli ya Buyakada mnamo 15 Julai. Walifanya mkutano kwa siku mbili. Mmoja wa washiriki aliyevuta hisia za wengi ni mtumishi wa CIA, Profesa wa ki-Marekani Henry Barkey.

Ahaber ilisema tukio la uwezeshaji ni kama “ukumbusho wa kikao kilichofanyika Julai 15,” lakini hawakutoa dondoo zaid kuhusu nani aliyehudhuria mkutano huo wa mwaka jana.

Uongozi wa Chama cha AKP (Justice and Development Party) nchini Uturuki wameendelea kutuhumiwa kutumia jaribio la mapinduzi la mwaka jana kama haki ya kuisafisha serikali ya watu wasio waaminifu na kuvunja masalia ya jumuiya za kiraia na vyombo huru vya habari nchini.

Nchi imebaki katika “hali ya hatari” inayotoa wigo mpana kwa mamlaka za ulinzi.

Akijibu habari ikiyotolewa na Abaher, mmoja wa wanasheria mashuhuri nchini Uturuki aliandika hivi huko Twitter:

Ndani ya nchi hii, mtu yeyote anaweza kutajwa kama gaidi saa yoyote. Hata wale ambao wamekuwa wakiilinda haki ya kuishi.

Watu waliotajwa katika habari hii ni watu ambao wameyatoa maisha yao katika Haki za Binadamu. Siku itakuja pale watakaposimama kwa ajili ya haki za hao walio nyuma ya habari hii ovu.

Kizuizi hiki kilifanywa usiku wa Julai 6 pale Kamishina wa Umoja wa Ulaya Johannes Hahn alipotembela Ankara kujadili kuhusu jitihada zilizokwama za kukabidhi madaraka, baada ya Bunge la Ulaya kutaka kusimamishwa kwa majadiliano hayo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.