Salvador Adame ni Mwandishi wa Habari wa Saba Kuuawa Nchini Mexico Tangu Mwanzoni mwa 2017

Salvador Adame. Imagen circulada ampliamente en Twitter.

Salvador Adame. Picha imesambazwa sana Twitter.

Mwili wa Salvador Adame, mwanahabari na mwanzilishi wa kituo cha habari cha 6TV, was uligunduliwa huko katika jiji la Michoacan, Magharibi mwa Mexico ukiwa umechomwa moto, serikali ilitaarifu mapema Juni 26:

Después de realizar la toma y cotejo de muestras que marca la ley en estos procedimientos, por parte de especialistas de la Dirección de Genética, las pruebas de ADN permitieron comprobar que estos restos corresponden a quien en vida se llamó a Salvador Adame Pardo.

Mara baada ya kuchukua na kulinganisha alama za vidole za sampuli iliyohitajiwa kisheria na wataalamu kutoka kitenngo cha vinasaba, vipimo vya vinasaba vinatufanya kuhitimisha kuwa mabaki ya mwili huu ni ya Salvador Adame Pardo, kama alivyofahamika wakati wa uhai wake.

Mwezi mmoja kabla, Adame alitekwa na kundi la wanajeshi, hii ni kwa mujibu wa taarifa za gazeti la erikali la La Jornada.

Eneo ambalo mwili wake ulikutwa, linafahamika zaidi kama eneo la Joto, na ni moja ya maeneo yanayofahamika sana kwa ghasia huko Michoacán, jiji ambalo kwa miaka michache iliyopita  limekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya kihalifu yanayodhaniwa kupangwa kwa usiri mkubwa na serikali za mitaa.

Kituo cha habari cha Animal Político cha kujitegemea kilitaarifu kuwa kabla ya kifo chake, kwa nyakati tofauti Adame alipokea taarifa za vitisho na kupewa tahadhari ya kuachana na shughuli ya uandishi wa habari. Mke wake Frida Urtiz alisema kuwa, naye alikuwa na wakati mgumu sana kwa kuwa alikuwa akifanya kazi na Adame:

Mi esposo y yo somos los dueños del canal, teníamos convenios de publicidad con el municipio de Múgica de difundir la labor que todas las administraciones tienen la obligación de hacerle saber a la ciudadanía y desistimos de ello ante la presión que recibíamos.

Mume wangu na mimi ni wamiliki wa chombo cha habari. Tullingia mkataba wa matangazo na Manispaa ya Múgica kwa ajili ya kufanya kile mamlaka yoyote inachopaswa kukifanya: kuwapa wananchi taarifa. Tuliahirisha kwa sababu ya vipingamizi tulivyokutana navyo.

Taarifa fupi iliyotolewa na 6TV yenyewe ilimuelezea Adame kwa namna hivi:

El periodista, quien hace pocos más de un año fue sujeto de vejaciones policiales, mantuvo una directriz activa, crítica, sagaz, atrevida, desafiante, al escenario delictivo que prevalece en la zona, también conocida como Cuatro Caminos, corazón de la entidad y epicentro de interminables disputas gansteriles.

Mwanahabari huyu aliyekuwa akikabiliwa na uonevu wa polisi kwa takribani mwaka mmoja uliopita, alisimamia vita dhidi ya matukio ya uhalifu kwa uimara, weledi, na ukakamavu yanayoendelea kushamiri katika eneo hili, ambalo pia hujulikana kama Cuatro Caminos, kitovu cha jiji na eneo la mapigano yasiyokoma ya kamundi ya wahalifu.

Adame ni  ni mwandishi wa habari wa saba kuuawa nhcini Mexico kwa mwaka 2017, kama alivyobainisha mtetezi wa haki za binadamu, Cencos. Walichapisha picha iliyoelezea namna Adame mwili wa adame ulivyopatikana, kudai haki kutendeka na kuhitimisha na maelezo, “Ukweli haufi kwa kumuua mwandishi wa habari”:

#SalvadorAdame nni mwandishi wa habari wa saba anauawa tangu kuanza kwa mwaka huu. Tunahitaji uwazi na kukomeshwa kwa kila aina ya ukatili. #HakunaKunyamazishwa.

Madhara ya mahsambulio haya dhidi ya waaandishi wa habari nchini mexico siyo tu kwamba yamekuwa makubwa zaidi ya kuwaathiri waandishi wa habari peke yao. Frida Urtiz, kwa mfano, alikubwa na matatizo makubwa ya kiafya mara baada ya kuuawa kwa mume wake.

Hivi karibuni, kiongozi wa juu wa idara ya wizara ya mambo ya ndani, Roberto Campa, alionekana kupunguza makali ya hali ya mambo pale aliposema ikilinganishwa na serikali zilizopita,  hiki siyo kipindi kibaya sana cha uonevu dhidi ya waandishi wa habari nchini Mexico.

Hata hivyo, ni kweli kuwa uonevu dhidi ya waandishi wa habari nchini Mexico siyo jambo geni. Mwaka 2015, mwandishi wa habari Isabel Uribe aliandika:

En el periodismo mexicano la tinta segrega un constante olor a muerte, nueve periodistas asesinados en lo que va de 2015 confirman que México es uno de los lugares más peligrosos en todo el planeta para ejercer la profesión, una caja de pandora que esconde las más terribles atrocidades: agresiones, intimidaciones, tortura, desaparición, autocensura y muerte.

Uanahabari wa Mexico, wakati wote wino unanuka harufu ya damu. Mauaji ya waandishi tisa wa habari tangu kuanza kwa mwaka 2015 inathibitisha ni kwa jinsi gani tasnia ya uandishi wa habari nchini Mexico ilivyo ya hatari ukilinganisha na maeneo mengine duniani, yani ni boksi la maovu lililoficha ukatili wa kutisha kuliko mwingine wowote ule: matumizi ya nguvu, kutishwa, kufuatiliwa na kifo.

Mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Adame, Luis De Tlacuilo, mtumiaji wa Twitter, alitoa maoni yafuatayo:

Inasikitisha sana kwa mtu kuuawa akiwa anatimiza wajibu katika taaluma yake. #SalvadorAdame

Mwadishi wa habari Jenaro Villamil aliishutumu serikali ya mtaa:

Another journalist killed. #SalvadorAdame. Mara baada ya wiki kadhaa za kutoroshwa chini ya serikali dhaifu ya Michoacan.

Mamlaka inayohusika na utetezi wa haki za binadamu nchini mexico imezitaka taasisi nyingine zilizo chini ya serikali kuchukua hatua:

CDNH inazitaka mamlaka katika ngazi zote tatu za serikali kufanya uchunguzi na kubaini wahusika wa mauaji ya #SalvadorAdame.

Salvador Adame anakuwa ni miongoni orodha ya watu waliouawa tangu kuanza kwa mwaka 2017, orodha inayowajumuisha Miroslava Breach na Javier Valdez.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.