Wataalam wa Teknolojia Nchini India Wanapambana Kubaini Ujumbe Bandia Unaoenezwa WhatsApp na Facebook

Mozilla L10N Hackathon mjini Punjab, India. Picha na Subhashish Panigrahi kupitia mtandao wa Wikimedia (CC BY-SA 4.0)

Wataalam wa program za kompyuta nchini India wanatengeneza tovuti maalum inayosaidia kubaini ujumbe bandia unasambazwa kwenye mtandao wa Whatsapp na Facebook. Ukifahamika kama check4spam.com, mtandao huo unategemea kwa kiasi kikubwa utafiti na uchunguzi unaofanywa na timu ya check4spam sambamba na watumiaji wake wa kujitolea.

Kikundi hicho kinalenga kukuza uwezo wa tovuti hiyo kutoa huduma za kuaminika kupitia zana za kiteknolojia. Wanaelezea mradi huo kama ifuatavyo:

Tunahakiki posti zozote kwa kufanya yafuatayo:

1. Tunawasiliana na mtu/taasisi iliyotajwa kwenye posti husika
2. Tunafanya uchunguzi wa kina (mtandaoni na nje ya mtandao) kupata taarifa zozote zinazohusu habari husika

- Tunavyofanya kazi, check4spam.com

Vyama 10 vya siasa vilivyokithiri kwa ufisadi duniani mwaka 2017 kwa mujibu wa BBC

India inashuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya mtandao wa intaneti, hata miongoni mwa wazee. Watumiaji wengi hawajui namna ya kutofautisha vyanzo vya habari vinavyoaminika na vile bandia au vya kitapeli. Na kuna tishio la kuwavutia watu kubofya viungo fulani, udanganyifu au program maalum zilizotengenezwa kwa mfumo wa Trojan mahsusi kuiba taarifa za vifaa vinavyotumiwa na watu mtandaoni.

Bal Krishn Birla na Shammas Oliyath waliotengeneza tovuti hiyo ni magwiji wa programu wanaoishi kwenye jiji la Bengaluru nchini India. Wakiwa na lengo la kutoa “huduma zisizo na masharti kwa ajili ya ubinadamu” na wakiongozwa na dira ya “kufanya maisha yawe rahisi kwa mtu wa kawaida na kufanya mambo yawe magumu kwa wasumbufu wa mtandaoni,” wameamua kuwaelimisha watu nchini India kuchukua tahadhari ya ujumbe wa kughushi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijami, na kuwaomba kuwasambazia wengine.

Uthibitisho wa usalama. Picha na tovuti ya Check4Spam.

Wameandaa namba maalum ya WhatsApp mwezi Agosti 2016 kwa ajili ya watu kutuma ujumbe wa maneno mafupi (arafa) kwa ajili ya kuthibitisha taarifa. Kwa mujibu wa Shammas, takribani ujumbe 100 hutumwa kila siku kwa ajili ya uthibitisho. Shammas husoma ujumbe huo wakati akiwa kwenye mapumziko ya chakula cha mchana yanayochukua saa moja na kuanza kufanyia kazi vyanzo vyake.

Check4Spam ni mradi usiotegemea ufadhili wa mtu mwingine. Hupata mapato madogo kutokana na matangazo kwenye tovuti hiyo yanayosaidia kugharamia uendeshaji wake, ikiwa ni pamoja na posti za kueneza habari zao kwenye mtandao wa Facebook.

#Check4Spam
1. Hifadhi namba +9035067726 kwenye simu yako
2. Nukuu ujumbe usiokuwa na uhakika nao
3. Tuma ujumbe huo kwa WhatsApp. Watakuambia ikiwa ujumbe huo ni wa kughushi ama la.

Mtandao huo wa check4spam.com unafanyia kazi ujumbe wa maandishi pekee, picha pekee na mchanganyiko wa mandishi na picha. Pia unaweza kugundua chanzo  cha ujumbe usijulikana umetoka wapi kwa kuwaomba watu waripoti ujumbe wa namna hiyo unaogundulika na watumiaji wenyewe. Kwa sasa ujumbe unaotumwa bila ridhaa ya mpokeaji umegawanywa katika makundi ya tetesi za mtandaoni, ajali, nafasi za kazi, taarifa za kitatibu, kupotea kwa mtu, miradi ya serikali na matangazo.

Mtandao huo hutembelewa na watu nusu milioni kwa mwezi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.