Wanamazingira wa Siberia Wachoshwa na Mamlaka za Nchini Kwao, Waomba Msaada Kwa Leonardo DiCaprio

Wana mazingira wa Krasnoyarsk wakata rufaa kwa Dr. DiCaprio. Picha: Vkontakte

Kulingana na hadithi maarufu wanazojifunza Warusi shuleni, katika karne ya 11 watu wa Urusi walialika “mameneja” kutoka Skandinavia kuja na kutawala ardhi yao. Waliitwa “Wa-Varangia” wakuu wa kabila (wakitokea katika mamlaka za Sweden na Norway iliyostaarabika) wakiwa na ujuzi katika uongozi bora na walisaidia sana katika Urusi ya zamani,hadithi inaendelea.

Enzi ya Wavarangia ilikuja na kuondoka, lakini baadhi ya Warusi leo bado wanatafuta mkombozi kutoka nje. Katika mji wa Krasnoyarsk, ambao ni mji wa tatu kwa ukubwa, huko Siberia, wanamazingira wa humo walimpata mwanaume wao: Nyota wa Hollywood, Leonardo DiCaprio.

Ili kuvuta umakini juu ya uchafuzi wa hali ya hewa unaokabili nyumba zao, wanaharakati hao hivi karibuni waliweka bango kubwa likionesha uso mzuri wa Leonardo DiCaprio na maneno yenye wakha yanayosomeka “Leon, iokoe Krasnoyarsk kutoka kwenye mkaa!”

Hiki kilikuwa kitendo kipya kabisa katika kampeni dhidi ya vinu vya kufulia nishati zilizodumu kwa miaka kadhaa sasa. Kwa mfano mwezi uliopita, wananchi waliitisha maandamano wakitaka vinu vya makaa ya mawe vizimwe na itumike gesi asilia, ambapo wanamazingira wanaamini kuwa itapunguza uchafuzi wa hali ya hewa.

Muanzilishi wa shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori mwaka 1998 na balozi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi katika Umoja wa Mataifa, Leonardo DiCaprio anasifika kwa kazi zake za Uanamazingira. Wakati akipokea tuzo yake ya Oscar mwaka jana, alitoa hotuba yake akilenga katika masuala ya tabia nchi.

Wanamazingira wa Krasnoyarsk kuelekeza kilio chao kwa DiCaprio inawakilisha mwenendo wa ulimwengu mzima, ambapo wanaharakati hutumia miaka kadhaa wakiziwinda mamlaka ambazo hazina mwitikio, kabla hazijakata rufaa kwa jumuiya za kimataifa, na kwa wakati huu wakimtumia mtu maarufu duniani kuvuta umakini katika suala lao.

Mwanazuoni Ethan Zuckerman (mshirika-mwanzilishi wa Global Voices) aliunda “kanuni ya paka mzuri ya uanaharakati wa dijitali,” ambayo inapendekeza kwamba kati ya picha nzuri za paka na picha (selfie) za wakati wa chai ya saa nne, ndipo muundo mpya wa wanaharakati wa kijamii wanaweza kustawi.

Kwa kuning'iniza mabango yakukata rufaa kwa Leonardo DiCaprio, wanamazingira wa Krasnoyarsk hawaweki msisitizo wa moja kwa moja kwa maafisa wa mamlaka za miji lakini tangazo hilo linaweza kulileta jambo hilo katika ufahamu wao kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na labla yaweza kuwa njia bora zaidi kuliko utamaduni wa migomo ya nje ya ukumbi wa mji.

Tatizo la kawaida kwa kampeni kama hizi huwa ni kupambana kuondoa mapambano haya wenye skrini ya kompyuta kwenda mitaani. Kuna uwezekano pengine kile kilichokuwa msaada kwa kampeni za Krasnoyarsk kikaweza kuwa na kwa Dicaprio kutangaza suala la mji huo.

Na wakati huo huo, watumiaji wa mitandao nchini Urusi wanafanya mzaha juu ya wito huo wa umma wa Krasnoyarsk. “Ingekuwa bora zaidi kama wangetafuta msaada kwa Chuck Norris. Leo anaweza kushughulika na masuala ya kwenye maji pekee,” baadhi ya watu walitania. Wakionesha ufahamu na kuvutiwa na uigizaji wa DiCaprio, wengine waliandika katika maoni yao mitandaoni: “Wangemwita Tarantino aje kusaidia uhalifu mitaani.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.