- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wahindi Waomboleza Kifo cha Kishori Amonkar, Mmoja wa Waimbaji Wakubwa Wa Muziki Wa Jadi Nchini India

Mada za Habari: Asia ya Kusini, India, Muziki, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia
[1]

Picha ya Kishori Amonkar kutoka mtandao wa YouTube.

Kishori Amonkar [2], mwanamuziki gwiji wa muziki wa jadi wa Kihindi [3], aliaga dunia akiwa nyumbani kwake huko Mombai usiku wa tarehe 3, mwezi Aprili baada ya kuugua kwa muda mfupi. Alikuwa na umri wa miaka 84.

Amonkar alikuwa muimbaji mashuhuri wa Hindustani au India Kaskazini, utamaduni wa muziki wa jadi [4], ambao umekuwa ukibadilika tangu karne ya 12. Wahindi wanaotumia mitandao ya kijamii waliomboleza kifo chake wakikumbuka maisha yake.

Katika hali ya masikitiko kwa kumpoteza muimbaji gwiji Kishori Amonkar ji. Tumempoteza mtu muhimu sana kwenye tasnia ya muziki wa jadi India

Kishori Amonkar ameaga dunia. Licha ya muziki wake wa kiwango cha juu, yapo mengi yakujifunza kutoka kwake: werevu wa hali ya juu, na utetezi usioyumba wa sanaa yake.

Habari za kutisha. Nguli wa muziki wa kale wa Hindustani Kishori Amonkar wa Jaipur Gharana hayupo tena! Tutakukumbuka sana. Upumzike kwa Amani.

Amonkar alifanya kazi za muziki wa aina yake uitwao  khyal [9] pia muziki wa jadi maarufu kama thumri [10] na  bhajan [11]. Pamoja na hayo alikuwa mvumbuzi wa muziki uliotambulika kama Jaipur gharana [12].

Shrimati Kishori Amonkar – Raga Basanti Kedar # 2 na Bhajan https://t.co/cnNp6lMP8c [13]

Kwa mujibu wa Blogu ya Ulimwengu wa Muziki wa Hindustani ya Deepak Raja [15]:

Kishori Amonkar (alizaliwa: mwaka 1932) ni mwimbaji wa muziki wa Hindustani wa kike mwenye nguvu zaidi kuwahi kutokea tangu India ijitwalie uhuru wake. Ni binti wa mfuasi wa mila ya Jaipur-Atrauli Gharana, Mogubai Kurdikar [16], lakini alipata heshima yake kwa sababu ya uwezo wake wa kubuni vitu vipya akiwa kama mtafsiri wa hekima za muziki wa Gharana. Alibadilisha muziki wake wa kutoka kwenye mtindo wa Gharana ufanane na muziki wa mapenzi, hatua iliyomfanya apate upinzani kwa maoni ya wahafidhina lakini alishinda. Matokeo ya mapinduzi aliyoyafanya, yanaonekana hivi sasa kwani mtindo wake umekuwa alama ya mila ya uimbaji ya Jaipur-Atrauli, wakati mtindo wa kizamani ukiendelea kusahaulika.

Ingawa  Amonkar alianza kuimba akiwa bado na umri mdogo, aliweza kufahamika na akaanza kuimba kwenye mikusanyiko yenye watazamaji wengi miaka ya 1960 hadi 1970. Baada ya hapo , utendaji wake uliwafikia watu wa kaya mbalimbali huko India kupitia kanda za kaseti na rekodi. Lakini kiuhalisia, alikuwa akiishi maisha ya faragha.

Mwanamuziki anayeheshimika duniani Zakir Hussain [17]  alimuweka Amonkar miongoni mwa waimbaji wakubwa wa muziki wa Hindustani kwa wakati wote alipokuwa akihutubia mwaka 2011 kwenye filamu yake ya maisha halisi iitwayo “Bhinna Shadja [18]” (filamu inayomuhusu Amonkar iliyokuwa imefadhiliwa na wizara ya mambo ya nje nchini India):

Mwaka 2013, Harmonium [19], blogu ya muziki, walichambua uimbaji wa Amonkar:

Kuna sauti fulani ambazo zina uwezo wa kuteka hisia na moja ikiwemo ya Kishori Amonkar. Huwa napata hisia ninaposikiliza rekodi hii kwamba muziki hautoki ndani yake bali yeye mwenyewe ndio muziki tunaousikia. Haugawanyiki. Mmoja na ni uleule. Tunaelea pamooja nae. Tukijisikia wepesi na zaidi ya hayo kuunganishwa. Anapoimba tunalia na tunataka kuzingirwa na sauti yake, hautaki kuondoka.

Enzi za uhai wake, Amonkar alipokea tuzo mbili za kiraia kwa wa-Hindi: ikiwemo Padma Bhushan [20] mwaka 1987 sambamba na Padma Vibhushan [21] mnamo mwaka 2002. Mtandaoni, watu walikumbuka urithi wake kwa kusambaza baadhi ya kazi zake:

Siku yenye huzuni. Kishori Amonkar aliyekuwa mwenye akili zisizo na kifani. Mkubwa.Alijitolea mmengi kwa ajili ya muziki wa India.

— Ramachandra Guha (@Ram_Guha) aliandika haya Aprili 4, 2017 [28]

Marehemu Rageshree, mkuu sana, Kishori Amonkar alikuwa mwenye mamlaka na mtukufu.
Usikilize, na usikilize kwa mara nyingine

‘Mharo Pranam’ Nipo kwenye kitanzi tangu asubuhi. Bado natafuta maneno ya kuelezea uhalisia na uvumilivu wa huyu mtu.

Watu walikumbuka hata nukuu zake zilizokuwa maarufu:

Naamini kuwa muzuki wa India si kitu ila uwezo wa kuonyesha hisia. Kama nikisema nakupenda je, neno ‘nakupenda,’ unaweza kulipima? Unapaswa tu kuhisi mrindimo wa neno hilo.

Ni mchanganyiko wa akili na ubongo unaohitajika kwenye sanaa. Hutakiwi kuwa mtu wa hisia tu, usiyetumia akili. Panahitajika uwiano mzuri wa akili na moyo

Arnab Chakrabarty [32] aliandika haya kwenye Scroll.in:

Tasnia ambayo wataalam wenye mafanikio hujisikia kuridhika wanapokuwa na umri wa miaka 40 au 50, muziki wa Amonkar uliendelea kukua bila pingamizi hadi siku alipoaga dunia.

Mwili wa Amonkar atachomwa mnamo Aprili 4 baada ya mazishi [33] kwenye bustani ya Shivaji jijini Mumbai. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi kwake:

Kazi za Kishori Amonkar zinatarijiwa kuendelea kuvuma katika jamii kaya mbalimbali kwa miaka mingi baada ya kifo chake.