Mwanablogu na Mwanaharakati wa Maldives Yameen Rasheed Auawa kwa Kuchomwa na Kitu chenye Ncha Kali

Picha Kutoka kwenye video ya Yameen Rasheed akiwa katika mahojiano na Mwandihsi wa habari na Mwanablogu wa Nepal Ujjwal Acharya.

Mwanablogu na mwanaharakati wa Maldive Yameen Rasheed, miaka 29, alichomwa na kitu chenye ncha kali na kupoteza maisha katika mji mkuu wa Male majira ya asubuhi ya Aprili 23 2017.

Kupitia Blogu yake ya The Daily Panic na katika ukurasa wake wa Twitter @Yaamyn, Rasheed amkuwa akifahamika kama mkosoaji mkubwa wa serikali pamoja na Uislam wa msimamo mkali. Raia wa Maldives wakiwa wameshtushwa na kifo hiki, walitumia mitandao ya kijamii kuonesha huzuni na mshtuko walioupata, huku baadhi yao wakishinikiza jamii ya kimataifa kuingilia kati.

Rasheed alikutwa kwenye sehemu ya ngazi za makazi yake majira ya saa 9 usiku akiwa na majeraha kadhaa ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na alipoteza maisha mda mchache mara baada ya kufikishwa hospitali. Alikutwa na majeraha 16 mwilini mwake, 14 ya kifuani, moja la kwenye shingo na moja la kichwani. Mara kadhaa alikua akipokea  vitisho vya kuuawa kupitia ujumbe mfupi na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali na watu wenye misimamo mikali ya kidini, ambapo vitisho hivi alishavitolea taarifa polisi.

Mbali na makala zake za mtandaoni, Rasheed alikuwa pia ni mwanaharakati. Mei Mosi ya 2015, yeye pamoja na dazeni ya wanaharakati wenzake walikamatwa kufuatia kushiriki kwao kwenye mandamano ya kuipinga serikali na kuwekwa kizuizini kwa siku 21.

Rasheed alikuwa akifanya kazi na Soko la Hisa la Maldeves kama mtaalam wa Mawasiliano na Teknolojia. Kwa heshima ya Rasheed, Ofisi ya Soko la Hisa ilifungwa mnamo Aprili 23.

Msemaji wa Rais Abdulla Yameen katika ukurasa wake wa Twitter alisema kuwa serikali “itatenda haki”. Raia wanaombwa pia kutoa ushirikiano ili kurahisisha kumalizwa kwa kesi hii.

Rais wa zamani wa Maldive Maumoon Abdul Gayoom aliwakilisha hisia watumiaji wengi wa mtandao kwa kuandika katika ukurasa wake wa Twitter:

Rais mwingine wa zamani, Mohamed Nasheed, alihimiza upelelezi huru kufanyika:

Marafiki wa Rasheed wa Watetezi wa Haki za Binadamu pia waliomboleza kifo cha rafiki yao:

Rafiki yake, raia wa Madives anayeishi ugenini Muju Nasim, aliandika kuhusu mfululizo wa video za mtandaoni zilizojumuisha kazi alizowahi kuzifanya Rasheed:

Kwa yeyote anayependa kumfahamu zaidi Yameen Rasheed na aina ya utu aliokuwa nao, unaweza kutazama mfululizo wa video za mtandaoni (This week in Maldives) ambazo tulikuwa tukifanya pamoja.

Tulieza kurekodi matoleo machache kwani tuliamriwa tuache makala hiyo kwa kuhofia usalama wake kwani kwa wakati huo mimi nilikuwa nikiishi nje ya nchi ka takribani miaka mitano.

Maldives ina historia mbaya ya mauaji ya kujichukulia sheria mkononi yakiwalenga zaidi waandishi wa habari, wanaharakati na wanablogu.

Mwanablogu, mwanaharakati wa LGBT na mwanahabari Ismail Khilath Rasheed, anayefahamika pia kama Hilath, aliuawa kwa kuchomwa na kitu kikali Juni 2012 na Waislam walio na msimamo mkali.

Likifanana kabisa na tukio la mauaji ya Rasheed, Dk Afrasheem Ali, mwanachama wa Chama cha Kimaendeleo cha Maldives (PPM), aliuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali nje kidogo ya nyumba yake manamo Oktoba 2012.

Rasheed alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Ahmed Rilwan Abdulla, mwanahabari mwingine maarufu sana wa nchini Maldeves, mwanablogu na mtetezi wa haki za binadamu ambapo alitekwa na kisha kupelekwa pasipojulikana mwaka 2014 (see Taarifa ya Global Voices). Tangu 2014, Rasheed alikuwa akishinikiza vikali kupatikana kwa haki dhidi ya kutoonekana kwa Rilwan, na hivi nkaribuni alikuwa akishirikiana na familia ya Rilwan kufungua kesi dhidi ya polisi wa Maldives kuhusu upelelezi wa kifo Rilwan.

Mwanablogu Amira kwa amaoni yake aliona kuwa tukio la mauaji ya Rasheed lilikuwa la kupangwa:

Tukio hili haliwezi kuwa ni la bahati mbaya kana kwamba linafanywa na mtu asiye na akili timamu kwa kuua watu kila mahali. Ninaona kuna kila dalili kuwa tukio hili lilipangwa na kisha kutekelezwa.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mickail Naseem aliilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitisho vya kuuawa kwa Rasheed:

Siwezi kuwaamini watu wa Polisi ya Maldives ambao waliamua kufumbia macho matishio ya kuuawa kwa Rasheed kufanya upepelezi usiofungamana na upande wowote wa kifo chake.

Pia, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Naafiz Abdulla walionesha wasiwasi wake kuhusu mauaji yanayowalenga raia wa kawaida:

“Ile inayoitwa” Paradiso ya duniani haihakikishii raia wake usalama. Kesho inaweza kuwa ni mimi, wewe au yeyote miongoni mwetu.

Zifuatazo ni baadhi ya jumbe za Twitter mkuhusu kifo cha Rasheed:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.