- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Manusura Wasimulia Kuhusu Hatari za Kuhama Kupitia Jangwa la Sahara

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Haki za Binadamu, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhamiaji na Uhamaji, Vita na Migogoro, Wakimbizi
[1]

Wahamiaji waliokolewa kutoka kwenye mashua ndogo. Picha na Jeshi la Maji la Marekani.

Wahamiaji wenye Ufahamu [2] ni kampeni katika vyombo vya habari iliyo na lengo la kuwahabarisha wahamiaji kutoka nchi 15 za Kiafrika [3] kuhusu hatari za kuhama kupitia jangwa la Sahara, Libya na bahari ya Mediterrania .

Kwa miaka kadhaa, maelfu ya wahamiaji na wakimbizi kutoka barani Afrika na Mashariki ya Kati wamekuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterrania kwenda Ulaya kuepuka umasikini na mashitaka ya kisiasa.

Huu mradi [4] uliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji [5] (IOM), kwa msaada wa ubunifu na ufundi kutoka kwa Horace [6] kampuni ya mawasiliano, na kufadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia [7], Idara ya Uhuru wa Wananchi na Uhamiaji.

Machi 10, 2017 iliripoti kuwa wahamiaji wapatao 19,567 waliwasili Italia kwa njia ya bahari lakini 521 walikufa baharini ambapo ni 50 zaidi ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka 2016. Wengi wa wahamiaji walikuwa wanatokea Ivory Coast, Naijeria, Guinea, Senegal na Gambia.

Baadhi ya wahamiaji waliiambia [8] IOM kuwa safari yao ilikuwa ni ya hatari kuliko walivyotarajia:

Wengi hawakuwa na ufahamu juu ya hatari za kuhama kwa msaada wa wasafirishaji haramu, sio kwa baharini au jangwani pekee, lakini pia katika nchi walizopita kama vile Libya. Wakikumbuka hatari dhidi ya maisha katika safari yao huwa inawasononesha sana na mara nyingi hutamani kusahau na kusonga mbele na maisha yao na hivyo wengi huwa hawapendi kushirikisha uzoefu na wenzao walio bado nyumbani.

Kampeni hii hutumia Facebook [9], YouTube [10], Instagram [11] na Twitter [12] kuwapa wahamiaji jukwaa katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya kubadilishana mitazamo na shuhuda kwa picha na video zilizokusanywa katika kipindi chote cha safari yao.

Tayari kampeni hii imeshazalisha video [13] 31 za shuhuda. Hapa chini ni simulizi ya Trika aliyesafiri kutoka Sebha mpaka Tripoli:

Paco alishirikisha mkasa wake wa mwaka mzima gerezani:

Lamin alipoteza wapendwa wake katika safari kutoka Libya:

Ebrima aliambiwa aende baharini au auawe nchini Libya au Tunisia:

Blessing alisema alibakwa na kupigwa kila siku:

Imasuen aliona watu waliokufa kwa njaa jangwani: