Sura 12 za Mwanamke wa ki-Ganda

Mwanamke wa Uganda anayehitaji kuwa mrembo na kufurahia uasili. Picha ya Spencer Montero na imetumiwa kwa ruhusa.

Kwenye maazimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Machi 8, 2017, jukwaa la This is Uganda [Hii Ndio Uganda] iliendesha kampeni kuonyesha nyuso mbalimbali za mwanamke wa ki-Ganda. Kwa kutumia alama ishara #SheRunsUg [#AnaisukumaUganda], walionesha picha 87 zinazoangazia namna wanawake wa Uganda wanavyoendesha maisha yao ya kila siku.

This is Uganda ni jukwaa linaloundwa na waandishi wenye vipaji wanaotoka Uganda ambao wanakusudia kuandika masimulizi yanayohusu Uganda kwa lengo la kupambana na mitazamo hasi dhidi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu ya 2014 iliyoendeshwa na Taasisi ya Takwimu nchini humo, wanawake wanafikia asilimia 51 ya idadi ya raia wote wa nchi hiyo wakati wanaume walikuwa chini kidogo ya nusu ya idadi ya watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi.

Hapa ni baadhi ya picha zilizoonyeshwa kwenye mtandao wa Twita kuwaenzi wanawake wa Uganda.

Pilika pilika za kila siku:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda

Wale wanaopinga mtazamo hasi:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda

Mwanamama kwenye sekta ya afya:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na @phionapaige

Spika wa sasa wa bunge, Rebecca Kadaga. Alivunja rekodi pale alipofanikiwa kuwa mwanamke wa kwanza nchini Uganda kuwa Spika wa Bunge mwezi Mei 2011.

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda

Phionah Mutesi, aliyezaliwa kwenye eneo kubwa zaidi la makazi holela nchini humo, alikuja kuwa mchezaji namba moja hodari zaidi nchini Uganda. Simulizi lake limeingizwa kwenye filamu za Hollywood movie The Queen of Katwe. [Malkia wa Katwe].

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda

Mwalimu:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda.

Mama:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na Seyhan Arik

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na p.a.c.e onlus

Afisa wa polisi:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na Kibuubi Media

Maisha binafsi:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na Prossy Babirye

Urembo wa asili:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda. Picha na Spencer Montero

Na mwishoni mwanamke anayepeperusha bendera ya Uganda juu:

Hapa anakuja mwanamke wa Uganda

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.