Mauaji ya Mwandishi Nchini Mexico Yafufua Hasira Dhidi ya Ukatili kwa Waandishi wa Habari

Miroslava Breach Velducea 1962-2017. Foto tomada del perfil público de Twitter de La Jornada.

Miroslava Breach Velducea 1962-2017. Picha imechukuliwa kutoka kwenye  kiwakilishi cha Ukurasa wa Twitter ya La Jornada na imesambazwa kwa mapana na uhuru katika mitandao ya kijamii

Habari mbaya tena kutoka Mexico, wakati huu ni kutoka upande wa kaskazini katika mpaka wa jimbo la Chihuahua.

Mapema wiki hii mwandishi wa habari Miroslava Breach, ambaye anafanya kazi na vyombo kadhaa ya habari, likiwamo gazeti la Serikali liitwalo La Jornada na tovuti ya nyumbani iitwayo Norte, aliripotiwa kuuawa nje ya nyumba yake na mtu ambaye hakutambulika mara moja.

Tukio hili la kikatili, kulingana na magazeti ya serikali ya El Universal na Excélsior, lilitokea wakati wa asubuhi. Kinachojulikana tu ni kuwa, mwanaume alimkabili Miroslava na akampiga risasi nane kichwani kwa kutumia silaha yake.

Kwenye safu yake katika gazeti la Milenio, mwandishi Ricardo Aleman aliandika:

Miroslava Breach fue asesinada por ejercer su profesión, el periodismo de investigación, crítico e independiente. (…) Dicho de otro modo, mataron a Miroslava por hablar, por hacer pública la información que reclama la sociedad y molesta al poder, en cualquiera de sus formas.

Miroslava Breach aliuawa kwa sababu ya kutumia taaluma yake kama mwandishi wa habari huru na za uchunguzi. (…) Kwa maneno mengine, wamemuua Miroslava kwa kuongea, kwa kuweka hadharani taarifa zile ambazo umma ulizitaka na zilizowakera wenye mamlaka, kwa namna yoyote ilivyokuwa.

Mauaji ya Miroslava yanafuatia mauaji ya waandishi wengine wawili ndani ya mwezi huu, kama gazeti la Ki-Hispania la El País lilivyoripoti:

El asesinato se ha producido cuatro días después del ataque contra Ricardo Monlui, otro periodista que murió a tiros en el Estado de Veracruz el pasado 19 de marzo. Cecilio Pineda, un periodista del sureño Estado de Guerrero, fue ejecutado el pasado 2 de marzo. Suman ya 30 periodistas asesinados durante el mandato de Enrique Peña Nieto, ha informado la organización Artículo 19.

Mauaji yalitokea siku nne baada ya shambulio dhidi ya Ricardo Monlui, mwandishi mwingine wa habari aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Veracruz hapo Machi19. Cecilio Pineda, mwandishi kutoka jimbo la kusini la Guerrero, aliuawa hapo Machi 2. Waandishi wapatao 30 wameshauawa katika muhula wa Enrique Peña Nieto's, na hii ni kwa mujibu wa organization Article 19.

Huko Twitter, Article 19 ilishirikisha ujumbe ufuatao:

Epifanio Diaz pia alilaani mauaji ya waandishi wa habari:

Mexico ni kati ya nchi hatari sana kwa waandishi wa habari katika Amerika ya Ulatini na ni nchi ya tatu hatari duniani, ikiwa na kiwango cha juu sana cha uhalifu ukilinganisha na Syria na Iraki, na hii nii kwa mujibu wa Takwimu za Uhalifu Duniani 2016.

La kushangaza ni kuwa 95% ya makosa yote nchini Mexico hayahadhibiwi, na ni kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Mamlaka ya Ushindani Mexico.

Rais Enrique Peña ameongea akionekana kupendelea uhuru wa habari wa zamani.

Hapo Oktoba 2016, kwa mfano, alisema:

Una nación democrática como lo es México, no puede explicarse sin medios de comunicación que ejerzan a plenitud esa libertad (de expresión). Por eso el gobierno de la República defiende la pluralidad de ideas como una conquista democrática y un derecho irrenunciable de los mexicanos.

Nchi ya kidemokrasia kama Mexico haiwezi kujieleza yenyewe bila kutumia njia ya mawasiliano ambayo inaruhusu uhuru wa (kujileza). Ndiyo maana serikali ya Jamuhuri inalinda wingi wa mawazo kama ushindi na haki isiyohamishika kwa wa-Mexico.

Lakini haya ni maneno matupu na kukwepa kuwaadhibu wahusika wa uhalifu na ukatili dhidi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari na kwa ujumla limeshakuwa sehemu ya maisha nchini Mexico. Hivi karibuni, mihemuko hiyo ya kihisia imeelekezwa kwenye mitandao ya kijamii kwa hashitagi za #ImpunidadMata na #YaBastaDeBalas (#MauajiyaKikatili, #TayariRisasiZimetosha)

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.