
Mpiga picha anayeishi Tehran Fatemeh Behboudi alipata picha ya Chaharshanbeh Suri akisherehekea kwenye mitaa ya Tehran mnamo Machi 16, 2016. Tazama zaidi kwenye Ukurasa wake wa Instagram/a>.
Sherehe zilizozoeleka nchini Irani za kucheza na moto, zinazofahamika kama Chaharshanbe Suri, zimethibitisha kuwa Donald Trump alikuwa sahihi sana — hata kama bila kujua — alipoituhumu Iran “kucheza na moto” mwezi uliopita.
Mwanzoni mwa mwezi February, Rais wa Marekani Trump alituma twiti kadhaa zenye maneno makali kuhusu Irani, kufuatia amri yake ya kuwazuia raia wa Iran (miongoni mwa wengine) kusafiri kwenda Marekani.
Iran is playing with fire – they don't appreciate how “kind” President Obama was to them. Not me!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) February 3, 2017
Iran inacheza na moto – hawajashukuru kwa kiasi gani Rais Obama aliwanesha “upole”. Sio mimi!
Trump alikosoa sera ya Rais Obama ya kufufua upya uhusiano wake na Iran, ambayo ilifikia hatua ya kuwa na makubaliano juu ya silaha za nyuklia na kuondoa vikwazo kadhaa vilivyokuwa vimewekwa dhidi ya Iran.
Mwishoni mwa Januari, Iran ilifanya majaribio ya kombora lake lililosafiri maili 600, ikionekana dhahiri lengo lilikiwa ni kujaribu kupima msimamo wa Rais Trump juu ya ahadi za makubaliano ya nyuklia na Iran, ambazo ziliweka mwanya kwa Iran kufanya majaribio ya makombora yake.
Iran has been formally PUT ON NOTICE for firing a ballistic missile.Should have been thankful for the terrible deal the U.S. made with them!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) February 2, 2017
Iran IMEWEKWA KWENYE NOTISI rasmi kwa kulipua kombora. Walipaswa kuwa na shukrani kwa makubaliano ya ajabu ambayo Marekani ilifikia nao!
Kwenye mtandao wa intaneti, Trump kutumia maneno “kucheza na moto” kuliwashangaza wengi waliokuwa wanafahamu Chaharshanbe Suri, “Sherehe za Kale za Moto,” ambazo wa-Irani walikuwa wakisherehekea kwenye mkesha wa JUmatano ya mwisho kabla ya Mwaka Mpya.
Trump is wrong about Iran playing with fire, Chaharshanbe Suri isn't until March. ? ??
— Alkaline Trejo (@alkalinetrejo) February 3, 2017
Trump hayuko sahihi anapozungumzia Iran kuchezea moto, Chaharshanbe Suri itafanyika Machi
@realDonaldTrump hey mothafucker do you know chaharshanbe suri?
We don't play , we jump it.— × گنگستر بنگ گستر × (@EmiroSharif) February 3, 2017
Wewe mpumbavu unajua chaharshanbe suri?
For once in your life you tweeted the truth! We DO play with fire! It's called Chaharshanbe Suri & it's a beautiful ancient tradition. ? ?? https://t.co/Np6WmClBG4
— تینا (@tinahassannia) February 4, 2017
Angalau mara moja maishani mwako umetwiti ukweli! Tuna TABIA ya kucheza na moto! Inaitwa Chaharshanbe Suri. Ni utamaduni mzuri wa kale
Kalenda ya Iran huanza mwanzoni mwa majira ya masika ya ncha ya kaskazini ya dunia, mnamo Machi 21. Maadhimisho ya Mwaka Mpya, hata hivyo, huendelea jioni kabla ya Jumatano ya mwisho wa mwaka, ambapo watu hutengeneza moto na kuuruka, wakati wakiuzima.
Wakati watu wanaosherehekea wakiruka moto, wanasema:
زردی من از تو ک سرخي تو از من
Chukua unjano wangu, nipe wekundu wako.