Unaweza kupendekeza Washindani wa Tuzo za Blogu Kenya 2017

Baadhi ya washindi wa tuzo za BAKE 2016. Picha imetumiwa kwa ruhusa.

Tuzo za Blogu Kenya  kwa sasa inapokea mapendekezo  kwa ajili ya sherehe za mwaka huu. Wito wa kutuma majina yanayopendekezwa umeanza Januari 9 na zoezi hilo litaendelea mpaka Machi 10. Wanablogu na mashabiki wanaweza kutuma mapendekezo yao katika makundi tofauti.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012 na Chama cha Wanablogu Kenya (BAKE), shindano la Tuzo za Blogu Kenya , zinazofahamika pia kama Tuzo za BAKE, huwatambua na kuwaenzi wanablogu wanaofanya kazi zenye ubora. Shindano hilo, kwa mujibu wa waandaaji, liko wazi kwa wa-Kenya wote na makampuni yanayofanya kazi zao nchini Kenya.

BAKE ni taasisi ya kijamii inawakilisha kundi la wabunifu wa maudhui ya mtandaoni nchini Kenya, ikiratibu miradi kadhaa kama vile mafunzo ya kidijitali, Tuzo za Blogu Kenya, na tovuti ya uandishi wa kiraia iitwayo Kenya Monitor.

Kuongezeka kwa tuzo mbili mwaka huu, Blogu bora ya mtindo wa maisha na Blogu bora ya Haki za Binadamu, kunafanya idadi ya washindani kuwa makundi 21. Waandaaji wameweka kanuni kwamba washindi wa tuzo tatu au zaidi kukosa sifa za kushiriki shindano la mwaka huu.

Mapendekezo yote yatakapopokelewa, hatua ya maamuzi itakuwa kati ya Machi 11 na Machi 24, kabla ya kufunguliwa kwa zoezi la kupiga kura kwa watu wote, kuanzia Machi 27 na kuhitimishwa Mei 9.

Hatimaye, sherehe zitafanyika mnamo Mei 13 kwenye Hoteli ya Radisson Blu jijini Nairobi, ambapo washindi wa mwaka 2007 watatangazwa.

Mwaka jana, kwa mujibu wa waandaaji, Tuzo za BAKE zilipokea mapendekezo 4,899 katika makundi 19 na zaidi ya kura wazi 500,000. Waandaaji pia walibaini kuwa wanawake walifanya vizuri kwa kupigiwa kura na wanawake, kama vile Jamila El-Jabry (lifeinmombasa.com), Dk. Claire Kinuthia (theycallmedaktari.com), Maryann Waweru (mummytales.com), Rachael Muthoni (safari254.com), Diana Kaluhi (kaluhiskitchen.com) na Lucia Musau (luciamusau.com) — wote hao wakishinda kwenye makundi tofauti.

Unaweza kutazama orodha kamili ya washindi wa mwaka 2016 hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.