- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Waafrika Kusini Wanasimuliana Mambo ya Kuchekesha Waliyoyaamini Utotoni

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
[1]

Radi ikipiga aridhi. Baadhi ya watoto wa Afrika wameaminishwa kuwa radi inaweza kuwapiga wakivaa nguo nyekundi. Picha ya Creative Commons iliyowekwa mtandaoni na mtumiaji wa Wikipedia, Jessie Eastland.

Alama ishara ya vichekesho, #ThingsIBelievedInAsAChild [2] [Mambo niliyoamini Utotoni], imekuwa ikipata umaarufu nchini Afrika Kusini, ambapo watu wanaambiana imani kadhaa za kimila walizoamini enzi zao wakikua.

Hapa ni baadhi ya twiti zilizochanguliwa kwenye alama ishara hiyo.

Mtumiaji aitwaye “Divinity” ilibidi awe makini anapokula chungwa, kwa sababu:

Kama ukila mbegu za chungwa, mchungwa ungeanza kuota kwenye tumbo lako

“Big Boss” aliamini ilifaa kupiga mluzi wakati wa mchana:

Usipige mluzi usiku, utapata mikosi

Levi alifikiri kimo kilidumazwa na kurukwa:

Kama mtu angekuruka kwa mguu, hutarefuka mpaka afute mruko wake

Televisheni inafanyaje kazi?:

Watu wanaoonekana kwenye televisheni kimsingi wanaishi ndani ya televisheni

Ukiona gari lililobeba maiti linapita:

Ukiona gari hili, lazima ushike nywele mpaka likupite

Ilibidi uvae “Nguo kali za Jumapili”, siku ya Jumapili:

Ninaweza kuvaa nguo mpya siku ya Jumapili na sio siku nyingine za wiki

“#Avantgardehipster” aliamini:

Niliambiwa Albino hawafi bali hupotea
Mpaka sasa sijawahi kuona tangazo kuwa albino amefariki

Mtumiaji mmoja wa Twita aliweka picha ifuatayo sambamba na twiti yake:

Kula sana kunanifanya niwe na afya njema na mwenye nguvu

Anasemaje?:

Niliamini kwa hakika korodani ni zilikuwa mayai

Watoto hutokea wapi?:

Watoto hununuliwa hawazaliwi

Taa ya jokofu inajizimaje?:

Kwamba kuna mtu mdogo anayezima taa ya jokofu kila ninapofungua mlango wake

Unawezaje kuwatambua matajiri?:

Kama ulikuwa na kitu hiki nyumbani, basi wewe ni tajiri

Kama hutaki kuwa kibogoyo maisha yako yote…:

Ukishang'oa jino, usipolitupia kwenye bati jino jingine halitaota badala yake

“DJASH” alifikiri:

Dawa zote za mswaki ziliitwa Colgate
Dawa zote za kutoa madoa kwenye nguo ziliitwa JIK
Sabuni zote ziliitwa ama Lux au Sunlight

Jik, Colgate, Lux na Sunlight ni bidhaa maarufu kwenye eneo la kusini mwa bara la Afrika.

Angalia utabiri wa hali ya hewa kabla hujavaa nguo nyekundu:

Usivae nguo nyekundu kama kuna radi…radi inaweza kukupiga kirahisi sana