- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Kenya Yadaiwa Kuwalipa Watumiaji Maarufu wa Mtandao ya Kijamii Kutangaza Habari za “MadaktariWalafi”

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Afya, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Siasa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, GV Utetezi
[1]

Akina mama wakiwa kwenye foleni kupata matibabu, Hospitali ya Wilaya ya Sindo, Nyanza, Kenya. Picha imepigwa na Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza kupitia mtandao wa Flickr (CC BY-NC-ND 2.0)

Tangu Oktoba 2015, kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu the so-called “Wanablogu 36″ [2] — kikundi cha watu wenye ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wanaodaiwa kuajiriwa na serikali ya nchi hiyo kutetea maslahi ya serikali mtandaoni.

Wakati mwingine wakifahamika kama “Vijana wa Itumbi” au “Itumbots”, kikundi hicho kutengeneza mijadala ya mtandaoni, husambaza propaganda na wakati mwingi hufanya kzi ya kubadili matamshi yanayoonekana kukosoa vikali serikali ya sasa ya Kenya, kwa kutengeneza alama ishara zinazolenga kuwapotezea watu mwelekeo au wakati mwingine kuhujumu alama ishara husika zinazochafua sura ya serikali.

Inaaminiwa kuwa [2] wanablogu hawa wameajiriwa na Mkurugenzi wa Ikulu anayeshughulikia Mawasiliano ya Kidijitali Dennis Itumbi na wanafanya kazi chini ya Kitenfo cha Rais cha Mawasiliano wa Kimkakati kilichopo Ikulu.

#SemaNaRuto kwa nini umeajiri wanablogu 36 kueneza propaganda na kuharibu maoni yoyote ya kukosoa?

Suala hilo la wanablogu 36 limeshika kasi mtandaoni, kufuatia mgomo wa kitaifa [6] unaofanywa na madaktari wa Kenya. Mnamo Desemba 2016, madaktari wapatao 5,000 wa Kenya kutoka hospitali zote za umma waliingia kwenye mgomo [7]kupinga serikali kushindwa kutekeleza na kuheshimu Makubaliano ya Mjadala wa Pamoja (CBA) yaliyofanywa na kati ya serikali na [8] chama cha madaktari mwaka 2013. Ukiwa unaendelea tangu Desemba 5, uungwaji mkono unaofanywa na wananchi kwa mgomo huo umeongozeka kufuatia madai ya ubadhilifu wa mamilioni ya dola za Kimarekani kwenye Wizara ya Afya. Ufisadi huo unaathiri mfumo wa huduma za afya nchini humo [9].

Madhara ya mgomo huo yameongezeka mnamo Februari 13, 2017 wakati ambao jaji wa mahakama ya rufaa  alitoa hukumu kuwa maafisa saba [10] kutoka Chama cha madaktari, Mafamasia na Madaktari wa Tiba ya Kinywa nchini Kenya (KMPDU) wafungwe kwa kushindwa kuchukua hatua za kusitisha mgomo huo unaoendelea.

Alama ishara ya #GreedyDoctors (Madaktari Walafi)

Tangu kuanza kwa mgomo, wanablogu 36 walianzisha alama ishara nne: #DaktariRudiKazi [11]#GreedyDoctors [12] (MadaktariWalafi), #MyBadDoctorExperience [13] (Mabaya Niliyokutana Nayo kwa Daktari, and #DaktariMmetuchosha [14].

Alama ishara hizo zimepingwa si tu na wanachama wa chama cha madaktari, lakini pia na watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Kenya waligoma kuamini propaganda kuwa madaktari ni walafi, wasio na uwezo, wakiacha wa-Kenya wasio na hatia kupoteza maisha. Upinzani huu ulifanya jitihada za wanablogu hawa maarufu kugonga mwamba.

Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Mafamasia na Madaktari wa Afya ya Kinywa nchini Kenya (KMPDU), chombo kinachowaratibu madaktari wote wa Kenya, kilidai kuwa wanablogu 36 walikuwa wakilipwa fedha nyingi kuliko kiasi cha fedha kilichotengwa na serikali kwa ajili ya utafiti wa masuala ya afya nchini humo:

Kampeni hii (#GreedyDoctors) imefadhiliwa kwa Ksh milioni 20 (sawa na Tsh milioni 400) kwa ajili ya wanablogu 36 ukilinganisha na madaktari 5000 walioahidiwa Ksh milioni 11 (sawa na Tsh milioni 220) kwa mwaka kwa jili ya utafiti. Vipaumbele tafadhali!

Akaunti ya Twita ya chama cha madaktari pia ilihoji mantiki ya kampeni ya #GreedyDoctors, kwa kuchapisha muhtasari wa maudhui ya Makubaliano ya Mjadala wa Pamoja (CBA):

Madaktari walafi? “Ulafi” wetu ni kuwa na huduma bora za afya kama ilivyoainishwa kwenye Makubaliano ya Mjadala wa pamoja (CBA). @fnoluga [17] ameainisha “Ulafi” wetu hapa!

Akirejea moja wapo ya alama ishara nyingine, #DaktariRudiKazi [11], Dk. Mo aliweka bandiko la m-Kenya wa kawaida aliyekuwa akiwatetea madaktari kinyume na propaganda hizo chafu:

Hapa ni m-Kenya HALISI anayeona mambo kwa jicho la propaganda, ndimi mbili. #DaktariRudiKazi ni moja wapo ya propaganda hizo!

Omar Bond alitwiti:

Ninatamani wa-Kenya wawe na hasira na ufisadi mkubwa, wahujumu mishahara mikubwa ya wabunge na mawaziri kama wanavyohujumu kampeni ya #MadaktariWalafi. Wanafiki!

Poriot Teko aliainisha kuwa alama ishara hizo zilizotengenezwa na kikundi hicho zimekwama:

Alama ishara ya #GreedyDoctors imekwama, #mybaddoctorexperience imekwama sijui vijana wa @OleItumbi wafanya nini kesho

Ingawa kuna idadi fulani ya hospitali za misheni zenye kuhusishwa na madhehebu tofauti ya dini, uwezo wake umezidiwa kwa miezi miwili kufuatia idadi kubwa ya wagonjwa, wengi wakiwa ni wale wasiomudu gharama zinazotozwa na hospitali hizo binafsi

Strike takes a toll on public health

Si wa-Kenya wote wanaona janga hilo kwa mtazamo wa madaktari. Wengi walioathirika moja kwa moja wana ndugu wa karibu na wanaonesha kukatishwa tamaa na wanapinga pande zote mbili kwenye mgogoro huo. AbdulKarim Taraja, mwenye ndugu yake anayeteseka hospitali tangu kuanza kwa mgomo huo, alifikiri kuwa madaktari inabidi warudi kazini:

Ndugu yangu amekuwa akiteseka kwa miezi yote hii miwili akiwa hospitali. Sijali hata kama mtu analala sakafuni

John Muiru pia alijisikia kuwa madaktari wanahitaji kurudi kazini wakati majadiliano yanaendelea:

Je, madaktari wanaweza kukubali kanuni ya kurudi kazini, wakati vyombo vinavyohusika vikiendelea kutafuta hatima yao? Tunateseka!

Wakati huo huo, vifo vya wagonjwa mahospitalini vinaendelea kuongezeka. Hakuna idadi rasmi iliyotolewa na Wizara ya Afya ya wvifo vinavyoendelea kuongezeka kufuatia mgomo huo unaoendelea. Hata hivyo, kuna makadirio ya vifo 300 yalifanywa na kituo cha televisheni cha KTN:

Jana KTN ilikadiria kuwa watu 300 wamefariki tangu kuanza kwa mgomo wa madaktari

Baadhi ya mitazamo kama hiyo inapata nafasi kwneye mitandao ya kijamii nchini Kenya. Akiandika kuhusu vifo hivi, Soko Analyst alisema:

Vifo vya kizembe nilivyoviona vimenitisha kwa namna ambayo sina hakika kama nitasahau

Teddy Eugene alieleza

Wanawake watatu wajawazito walionyimwa huduma ya kulazwa kwenye hospitali ya Mwala, walipoteza vichanga vyao wakijaribu kujizalisha wenyewe

Wengine kama Kiprono hawaungi mkono mgomo huo kwa vyovyote kwa sababu ya vile madaktari wanavyowatendea wagonjwa wanaowatazama:

Ninaweza kuunga mkono mgomo wa madaktari lakini nikikumbuka namna wanavyowatendea wagonjwa hasa wale wanaokuwa kwenye hospitali za umma najisikia vibaya

Wanaoathirika na mgomo huu wa madaktari ni masikini ambao hawawezi kumudu gharama kubwa za huduma binafsi za afya, na wengi wao wanaamua kwenda kwenye hospitali kuu ya rufaa nchini humo, Hospitali ya Kenyatta.

Kadri vita ya kuboresha huduma za umma za afya inavyoendelea, vita ya alama ishara nayo ni dhahiri inaendelea kwenye mitandao ya kijamii.