Mwanablogu wa Algeria Merzoug Touati Anaweza Kutumikia Jela Miaka 25 Kwa Kufanya Mahojiano na Afisa wa Israel Kupitia Mtandao wa You Tube

Pilisi wakikabiliana na waandamanaji wakati wa machafuko ya mwaka 2011. Picha kwa hisani ya: Magharebia alichapisha kwenye Flickr kwa makubaliano ya idhini ya Creative Commons

Serikali ya Algeria yamtuhumu mwanablogu Merzoug Touati kwa kosa la “kutoa taarifa za kiintelijensia kwa afisa wa kigeni”, kupitia video ya mahojiano aliyoifanya na msemaji wa Wisara ya mambo ya nje ya Israel.

Polisi ilimkamata Touati mapema tarehe 18 Januari na kisha kuharibu kabisa Kopyuta na kamera yake, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Utetezi wa Haki za Binadamu wa Algeria (LADDH). Mwanasheria wa umoja huu ndiye anayemtetea Touati mahakamani.

Mwanasheria wa LADDH, Ikken Sofiane aliiambia Tovuti ya Habari za Algeria El-Watan, kuwa Touati walikutwa na hatia chini ya kifungu namba 71 cha sharia kinachoeleza kuwa kifungo cha miaka 29 gerezani kitamhusu mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya “kutoa taarifa za kiintelijensia kwa afisa wa nchi ya kigeni inayoweza kuhatarisha hadhi ya jeshi au kimahusiano ya Ageria kimataifa au mambo muhimu ya kiuchumi.”

Merzoug Touati anaweza pia kukabiliana na kifungo cha miaka 1-5 Zaidi gerezani kwa kosa la “Kuchochea maandamano dhidi ya Serikali to armed protests against the State.” Tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yake bado haijatajwa.

Merzoug Touati. Picha iliyokuwa imechapishwa kwenye ukurasa wa facebook wa Blogu yake Alhogra

Mapema tarehe 9 Januari, Touati alichapisha kwenye YouTube pamoja na kwenye blogu yake Alhogra video ya mahojiano na Hassan Kaabia, msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje wa Israel kwa upande wa lugha ya Kiarabu. Mahojiano hayo yalilenga kuhusu maoni ya jamii kuhusu sharia la Fedha ya 2017, inayojumuisha ongezeko la thamani, mapato na ushuru wa vitu pamoja na kupungua kwa ruzuku ya nishati. Mara baada ya sharia hiyo hiyo kuanza kufanya kazi rasmi Januari 1, mandamano na machafuko yalizuka huko Kaskazini mwa jimbo la Bejaia pamoja na sehemu nyingine za nchi.

Waziri wa serikali ya Algeria aliyalaani mata ifa ya nje kuingilia mambo ya ndani ya nchi pamoja na kuchochea maandamano. Katika mahojiano hayo, Touati alimuuliza kuhusu tuhuma zilizotolewa na serikali ya Algeria.

Pia, Kaabia alimjuza Touati kuwa kabla ya mwaka 2000 kulikuwa na “mawasiliano” kati ya serikali za Algeria na Israel, lakini hakuthibitisha ikiwa hapo awali Algeria ilikuwa na balozi anayeiwakilisha nchi ya Israel. Algeria pamoja na muungano wa nchi za Kiarabu, ukiondoa nchi za Egypt na Jordan, hazitambui au kuwa na mahusiano ya kimataifa na nchi ya Israel kutokana na uvamizi wa Israel nchini Palestina. Hata hivyo, siku za hivi karibuni na hata kipindi cha nyuma, baadhi ya serikali za kiarabu zimekuwa na utaratibu wa mawasiliano na au kuwa na ofisi zinazoiwakilisha Israel. Mahusiano haya kwa kawaida hufanywa kwa usiri mkubwa miongoni mwa mataifa ya Kiarabu kutokana na mchango unaotolewa na mataifa haya nchini Palestina.

Katika blogu yake ya Alhogra, Touati mara kwa mara amekuwa akichapisha habari za maandamano ya kupinga hatua ya serikali ya kubana matumi, masuala ya ajira sambamba na matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na mamlaka za serikali ya Algeria. Mapema Desemba 22, alichapisha mahojiano aliyoyafanya na Tilelli Bouhafs, ambaye baba yake Slimane Bouhasf, kwa sasa anatumikia miaka mitatu gerezani kwa makosa ya kutukana Uislam kupitia makala zake za mtandaoni.

Kwa tukio la kukamatwa kwa Touati, ni mwendelezo wa matukio ya serikali ya Algeria wa kunyamazisha wakosoaji wake na wale wote wanaotumia uhuru wao wa kujieleza mitandaoni. Mwezi Disemba 2016, kampeni hiiiligharimu maisha ya mwanablogu Mohammad Tamalt ambaye alipoteza fahamu kwa kususia kula kwa muda wa miezi miwili kama namna ya kuonesha kutokukubaliana na kitendo cha yeye kushikiliwa kwa kosa la kuchapisha katika ukurasa wa Facebook shairi lililokuwa linamkosoa Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.