- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kikundi cha ki-Islam Chadai Kuondolewa kwa Sanamu Mbele ya Mahakama Kuu Nchini Bangladesh

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Bangladesh, Dini, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala
[1]

Mahakama Kuu ya Bangladesh kama inavyoonekana kwenye makao makuu ya nchi hiyo Dhaka. Picha ya Wikimedia Commons. CC BY-SA 4.0

Nchini Bangladesh, kundi la kidini lenye msimamo mkali linadai [2] kuondolewa kwa sanamu maarufu kama Mwanamke wa Sheria mbele ya mahakama kuu. Wametishia [3] kuendesha harakati kuanzia Februari 24 kama madai yao hayatatekelezwa na mamlaka zinazohusika.

Sanamu hilo lilitengenezwa na chuma kisichoshika kutu na msanii maarufu Mrinal Hoque [4] na linatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili mwkaa huu. Sanamu hilo kwa sasa limewekwa mbele ya mahakama lakini bado linaendelea kunakshiwa.

Hefazat-e-Islam [5] na vyama vingine vya siasa chenye mrengo wa ki-Islam kama Islami Oikya Jote [6] vinadai sanamu la Mwanamke wa Haki linafanana na ‘mungu’ wa Kigiriki aitwaye Themis na linasababisha hisia mbaya za kidini [7] kwa wa-Islam walio wengi nchini humo. Wameomba serikali kufanya mageuzi makubwa katika mfumo wa mahakama nchini humo.

Mufti Foyzullah, katibu mkuu wa pamoja wa Hefazat-E-Islam aliwaambia waandishi wa habari: [3] “Hili [sanamu] limevalishwa sari [mavazi ya kiutamaduni] kwa namna inayofanya lisionekane kwa heshima.”

Kikundi cha Hefazat-e-Islam Bangladesh kilianzishwa mwaka 2013 wakati wa Maandamano ya #Shahbag [8] kudai kupigwa marufuku kwa vitendo vya watu kuchanganyika kijinsia na kuadhibiwa kwa “wanablogu wasiomini uwepo wa Mungu waliotuhumiwa kukufuru.” Walianzisha dai lao lenye vipengele 13 [9] mnamo Aprili 6, 2013 mjini Dhaka. Mbali na adhabu kubwa kwa kundi la watu waliodaiwa kukufuru walidai elimu yaki-Islam iwe lazima na iolewe amri ya kupiga marufuku kuenea kwa sanamu nchini humo.

Watu kadhaa kama Noor Hossain [10] wanaunga mkono dai hilo la kuliondoa sanamu hilo jipya:

গ্রিকপুরাণের কল্পিত দেবী থেমিস রোমানদের কাছে ন্যায়ের প্রতীক হতে পারে, কিন্তু সংখ্যাগরিষ্ঠ মুসলিম স্বাধীন দেশের নাগরিক হিসেবে আমরা তাদের ইতিহাস ও ঐতিহ্য থেকে ধার করে কেন হীন ঔপনিবেশিক ধ্যানধারণা লালন করবো? [..]

আমাদের প্রতিবেশী হিন্দু অধ্যুষিত ভারতের সুপ্রিমকোর্ট-প্রাঙ্গণে কোনো ধরনের মূর্তি স্থাপনের নজির নেই। [..] তাহলে আমাদের হাইকোর্টের সামনে কেন গ্রিক দেবীর মূর্তি স্থাপন করা হবে?

Huyu mungu Themis anaweza kuwa alama ya haki kwa Wagiriki kwa mujibu wa imani yao. Lakini kwa nini sisi, kama nchi huru yenye idadi kubwa ya wa-Islam, tuazime historia na urithi unaoendeleza mtazamo wa kutawaliwa na wakoloni? [..]

Hakuna tuio la masanamu hayo ya kigeni kuwepo kwenye mahakama mkuu za majirani zetu India. [..] Sasa kwa nini kuwepo sanamu ya mungu wa Kigiriki mbele ya Mahakama Kuu?

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mahbubey Alam alipuuza [11] madai hayo na kuyaita hayana maana wala msingi wowote. Sanamu hilo (Justitia), ni namna ya kuonesha kutokuwepo upendeleo katika mfumo wa utoaji wa haki na linapatikana kwenye nchini nyingi duniani, zikiwemo nchi za ki-Islam kama Iran, alisema.

Rafi Chowdhury [12] aliandika kwenye mtandao wa Facebook:

হেফাজত মূর্তি আর ভাস্কর্য এর অর্থ বোঝার মতো যথেষ্ট শিক্ষিত নয়।
মূর্তি অপসারণ হলে হেফাজত নিষিদ্ধ করার দাবি তুলবো।
এদেশ এদের কথায় চলবে না, চলবে ৭১ এর চার মূল নীতির উপর ।গনতন্র- সমাজতন্ত্র- ধর্মনিরপক্ষেতা-বাংগালী জাতিয়তার ভিত্তিতে ।

Hefazat hajaelimika vya kutosha kuelewa tofauti ya sanamu la mungu na sanamu la kawaida. Kama sanamu hilo litaondolewa, Nitaanza kudai kupigwa marufuku kwa Hefazat. Nchi hii isiendeshwe na madai yao, lazima tuenzi misingi minne ya kuanzishwa kwa nchi hii; demokrasia, ujamaa, uhuru wa din na utaifa wa Bengali.

Kulikuwa na miitikio ya hasira kwenye mtandao wa twita:

Hefazat nchini Bangladesh ambao ni wafanyabiashara wajanja wajanja sasa wameteuliwa kuwa mawakala na wakandarasi wanaolinda Uislam; utafikiri ni mali ya baba zao

Waislamu wenye msimamo mkali ikiwa ni pamoja na Hefazat-e-Islam siku moja watadai jina la nchi na lugha ya tiafa vibadilishwe kwa sababu havina u-Islamu

Sanamu moja kwenye mahakama kuu mjini Dhaka inatosha kuwafanya Hefezat-Islam watoe amri, vitisho na uimla

Abdur Rahim Rana aliandikwa kwenye Blogu ya Ishtishon [19]:

আজ হেফাজত বলছে ইসলামে মূর্তি হারাম তাই সুপ্রিম কোর্টের মূর্তিটি সরিয়ে ফেলতে হবে।
কিছু দিন পর বলা শুরু করবে, ইসলামে নারী নেতৃত্ব হারাম! শেখ হাসিনা গদি ছাড়। এই তো শুধু বলার বাকি।।। [..]

সাধুগন সাবধান, হেফাজতী আগ্রাসন না ঠেকাইলে অস্তিত্য খুজিয়া পাইবে না।

Sasa Hefazat wanasema Sanamu hiyo ni haramu kwenye u-Islam na hivyo sanamu iliy mbele ya Mahakama Kuu iondolewe. Baada ya siku si nyingi watasema mwanamke kuongoza taifa hili ni haram, na hivyo (Waziri Mkuu) Sheikh Hasina ang'atuke. Hili watalisema [..]

Tafadhali tuelewe, kama hutakuwa makini na ghadhabu za hawa Hefazati, usalama wako utahatarishwa siku moja.

Waziri wa masuala ya utamaduni, Asaduzzaman Noor, pia alikosoa [20] madai ya Hefazat:

হেফাজত এমনভাবে বলছে মনে হয় এটি গণপ্রজাতন্ত্রী বাংলাদেশ নয়, যেন ইসলামি প্রজাতন্ত্র বাংলাদেশ।

Hefazat kuongea hivi haimaanishi ndio sauti ya Jamhuri ya Watu wa Bangladesh, utafikiri ni Jamhuri ya Kiislam ya Bangladesh.

Bado haijafahamika ikiwa madai [21] ya Hefazat kuwa yatapokelewa na mamia ya maelfu ya watu ambao wako tayari kuingia mtaani kubomoa sanamu hilo kama halitaondolewa na serikali yanaweza kuwa na mantiki.