Baada ya Mwanablogu Kuhukumiwa Adhabu ya Kifo, Kesi yake Kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Nchini Mauritania

Picha kwa hisani ya Hani Amir kupitia Flickr (CC BY 3.0)

Mapema Januari 31, Mahakama kuu ya nchini Mauritania inatarajia kutoa hukumu ya kesi kesi ya mwanablogu Mohamed Cheikh Ould Mkhaitir, ambaye alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2014 kufuatia makala yake iliyochapishwa kwenye tovuti ya gazeti la Aqlame.

Katika makala hayo yaliyokuwa na kichwa cha habari “Dini, , Ufia dini na Mafundistadi”, ambayo hata hivyo yalishaondolewa kwenye tovuti hiyo, bado yanapatika mtandaoni, Ould Mkhaitir alikosoa matumizi ya dini katika kuhalalisha mfumo kandamizi wa kimatabaka, huku akitolea mifano hai ya maisha ya Mtume Muhammad.

Mohamed Cheikh Ould Mkhaitir

Serikali ya Mauritania ilimtia nguvuni Ould Mkhaitir manamo Januari 2 2014, siku mbili mara baada ya makala yake kuchapishwa, na Desemba 2014 Mahakama ya Mwanzo ya Nouadhibou ilimhukumu adhabu ya kunyongwa kwa”kuasi dini” chini ya kifungu namba 306 cha sheria ya Makosa ya Jinai nchini Mauritania , kwa kumzungumzia “kirahisi” mtume. Mapema April 2016, mahakama ya rufaa ilimkuta na hatia na kisha rufaa yake kupelekwa mahakama kuu, iliyo na mamlaka ya kumpunguzia adhabu na kuwa kifungo cha gerezani pamoja na fidia, kama ikijiridhisha kuwa mshitakiwa “alijutia”.
Kifungu namba 306 kinaeleza kwamba “Mwislam yeyote akikutwa na hatia ya kuasi, ama kwa maneno au kwa matendo kwa kukusudia au kutokukusudia, ataitwa ndanni dya kipindi kisichozidi siku tatu kwa ajili ya kutubu. Ikiwa mtuhumiwa atashindwa kutubu ndani ya siku hizi tatu, atahukumiwa adhabu ya kifo na mali zake zote zitateketezwa na serikali.” Kifungu hiki kinadelelea kueleza kuwa, ikiwa mshitakiwa “atatubu” kabla ya hukumu yake kutekelezwa, Mahakama Kuu ya Mauritania inaweza kutengua huku hiyo na kuwa ya kifungo cha kati ya miezi miwili hadi miaka miwili, pamoja na fidia ya UM5,000–60,000 (takribani dola za Marekati kati ya 14 – 170).

Kufuatia kukamatwa kwake, Ould Mkhaitir alichapisha makala akiwa gerezani na kusema kuwa, yeye hakuwa na lengo la kumchafua mtume, na kuwashutumu wapuinzani wake kwa “kueneza hisia za kidini” zinazolenga kumchafua yeye. Ould Mkhaitir ameshatubu, hata hivyo, kinachosubiriwa ni uamuzi wa Mahakama Kuu kuamua ikiwa toba yake inatosheleza au la.

Hivi karibuni [Februari 1, 2016]: Mahakama Kuu ya Mauritania ilishindwa kumpunguzia adhabu ya kunyongwa Ould Mkahitir. Mahakama Kuu ilirudisha kesi yake kwenye mahakama ya rufaa kufuatia kukosewa kwa taratibu kadhaa. Mahakama ya rufaa hapo awali ilimkuta na kosa la “uasi wa dini” na hivyo kuhukumiwa adhabu ya kifo. Hapo awali katika katika kesi yake, Ould Mkahitir alituhumiwa kwa kosa la “unafiki”, hali iliyoonesha kuwa toba yake usaliti wa dini ilionekana kuwa haikuwa ya kutoka moyoni.

‘Ngome ya Mwisho ya Utumwa’

Ukosoaji wa mfumo wa kitabaka bado unabaki kuwa ni jambo lisilokubalika kabisa Mauritania, nchi ambayo imekuwa ikielezewa kama “ngome ya mwisho ya utumwa.” Mauritania ilikuwa ndio nchi ya mwisho duniani kutokomeza biashara ya utumwa mnamo mwaka 1981 na kuichukulia rasmi biashara hiyo kuwa ni kosa la jinai mwaka 2007. Pamoja na hili, umoja wa Mataifa, inakadiria kuwa idadi ya watu wanaoishi katika hali ya utumwa inafikia kati ya laki 340 nadi laki 680, ambao ni kati ya asilimia 10 hadi 20 ya watu wote duniani. Idadi dya mshtaka chini ya Sheria ya Kupinga Utumwa ni “ndogo sana” kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2014 iliyotolewa na Waangalizi maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu hali ya sasa ya Utumwa, huku wanaharakati wa vita dhidi ya matendo ya kitumwa wakikabiliana na kesi za jinai.

Mwaka 2014, wanaharakati kadhaa akiwemo Biram Dah Abeid ambaye mwaka 2014 alikuwa miongoni mwa wagombea Urais nchini Mauritania sambamba na kuwa Rais wa Jukwaa la kutetea vitendo vya kitumwa na unyanyaswaji, walikamatwa na who ran for Mauritania's 2014 presidential election on an anti-slavery and anti-discrimination platform, were arrested and  kufunguliwa shitaka  la kuendesha kampeni za kutokomeza utumwa. Mwaka 2012, Dah Abeid, kama ilivyokuwa kwa Ould Mkhaitir mwaka 2014, alihukumiwa adhabu ya kifo kwa”kuasi dini” kufuatia kuendesha kampeni ya kutokomeza utumwa ambapo alichoma moto maandiko ya dini yaliyoandikwa katika karne ya 8 na mwanazuoni wa Kiislam yaliyokuwa yakionesha bayana uhalali wa utumwa na kisha kutoa hotubah akiwakosoa hadharani wale wate wanaotumia dini kuhalalisha utumwa na unyanyasaji:

Kuna kundi la watu wabaya wanaouongoza Uislam na kuutumia kwa kadiri ya wanavyopenda wao, na ambapo kundi hilo linaigawa jamii, ambapo wengine wanakuwa tabaka la chini na wengine tabaka la juu-sio kutokana na yale wanayoyafanya, au kwa namna walivyo, lakini ni kutokana na rangi za ngozi zao.

Baadae, Dah Abeid alionekana kuwa hakuwa na hatia. Hata hivyo, mwaka 2015, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kwa sababu ya uanaharakati wake wa kupinga vitendo vya kitumwa.

Katika nchi kadhaa katika eneo la Uarabuni ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, pamoja na Yemen, “Uasi wa dini” ni kosa la jinai linalopelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo. Tuhuma za Kuasi dini pamoja na kukashifu dini mara kwa mara hutumiwa “kama kisingizio cha namna ya kulipiza visasi vya kisiasa, au namna ya kulipiza kisasi dhidi ya mtu”, kama mwanahabari Brian Whitaker, mwandishi wa kitabu Waarabu Bila Mungu, alivyoandika wakati wa kesi ya Ould Mkahitir mwaka 2014.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.