- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Siku ya Maombolezo Mjini Kyrgyzstan Kufuatia Ajali ya Ndege ya Mizigo, Iliyoua Watu Zaidi ya 30

Mada za Habari: Asia ya Kati, Kyrgyzstan, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia
Kyrgyzstan's Manas airport in Bishkek. Creative commons.

Uwanja wa ndege wa Maans mjini Kyrgyzstan karibu na mji mkuu wa Bishkek. Creative commons [1].

Kyrgyzstan imetenga siku ya Januari 17 kuwa ya maombolezo baada ya ndege ya mizigo ya Uturuki kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege mkubwa zaidi wa nchi hiyo kufuatia ukungu asubuhi, na kisha kuanguka kwenye kijiji [2] kilichokuwa karibu na kuua zaidi ya watu 30.

Video mbaya ikionesha yaliyotokea baada ya ajali ya ndege kukitekeleza kijiji cha Kyrgyzstan, na kuua watu 37

Waliokufa wengi wao ni wenyeji wa Kyrgyz wanaotoka kwenye kijiji cha jirani, na habari zaidi zinaendele kupatikana

Kijana mdogo aliamka na kwenda shule. Alipokuwa anakaribia kufika, ndege ilianguka nyumbani kwao na familia yake yote ilipoteza maisha. Tukio baya sana.

Serikali ilimlaumu rubani wa ndege hiyo inayoendeshwa na shirika la ndege ya ACT, ukweli uliowaudhi watu wengi.

Mwandishhi wa habari Anna Lelik alinadika [6] kwenye ukurasa wa Facebook:

На расследование авиакрушений уходят многие месяцы. Наши власти, не найдя еще черных ящиков, без расшифровок, спустя всего лишь несколько часов, умудряются уже публично делать достаточно уверенные заявления о предварительных причинах. Без расследования, на очень высоком уровне, успевают судить о происшествии, которое случилось не в ясную солнечную погоду, а в сильный густой туман (и да, за считанные часы до этого президентский самолет посадили в Тамчы, а не в Бишкеке). Я надеюсь, что по итогам должного расследования будет восстановлена объективная картина и оглашены причины, а всем пострадавшим оказана помощь.

Мои соболезнования семьям и близким всех погибших в последствиях авиакатастрофы около аэропорта “Манас”. Пострадавшим – здоровья и поскорее пойти на поправку. Спасателям и медикам, всем помогающим, спасибо за их работу в такой холод.

Uchunguzi wa ajali ya ndege huchukua miezi mingi. Mamlaka zetu bado hazijapata kile kisanduku cheusi, hapakuwa na rekodi za maelezo, lakini masaa machache baada ya ajali, waliweza kutoa tamko la kujiamini kuhusu kitu gani kilichotokea. Bila uchunguzi, na kwa kiwango kikubwa, walipata muda wa kufanya uamuzi kuhusu tukio hilo, ambalo lilitokea kwa katika mazingira ya hali ya hewa yenye ukungu (na ndio, masaa machache kabla ya ndege ya rais [kulazimishwa kutua] Tamcky, badala ya Bishkek [kwa sababu ya ukungu]. Ninatarajia kuwa picha sahihi itaonekana baada ya uchunguzi kamili, na kuwa wahanga wote watasaidiwa. Rambirambi zangu familia na ndugu wa watu waliopoteza maisha kwenye tukio hilo la ajali ya ndege iliyotokea karibu na uwanja wa ndege wa Manas. Kwa waliojeruhiwa, nawatakiwa afya na uponyaji wa haraka. Kwa wanaofanya kazi ya uokoaji na madaktari, shukrani nyingi kwa kazi yenu nyote mnaoifanya kwenye mazingira ya baridi.

Janga hilo limesababisha kufanyika kwa jitihada za kutafuta raslimali [7] ambayo ni moja wapo ya kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya nchi hiyo. Mpaka sasa jitihada za kuchangisha fedha na vifaa zaidi, ikiwalenga watu wanaoishi Kyrgyzstan.

Kama namna nyingine za michango zitaonekana mtandaoni, Global Voices itaongeza kiungo kwenye makala haya.