- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Podikasti ya Chile Yafanya Nyota za Anga Zionekane na Kila Mtu

Mada za Habari: Amerika Kusini, Chile, Sayansi, Uandishi wa Habari za Kiraia
Pantallazo del episodio "San Pedro de Atacama, lo que nadie ve", disponible en Youtube. [1]

Picha iliyopigwa kwenye filamu ya “San Pedro de Atacama, what nobody sees”, inapatikana kwa ki-Hispaniola kwenye mtandao wa Youtube.

Chile ina historia ndefu ya utamaduni wa kutazama anga za mbali [2], ukienda sambamba na mazoea ya siku nyingi ya kuzungumzia mambo ya anga. Huu ndio mwanzo wa filamu ya  AstroBlog [3] iliyoandaliwa na mtayarishaji wa filamu na vipindi vya televisheni Ricardo García Sotoand sambamba na toleo lake la Kiingereza, Astronomy Et Al [4]. Msomi wa masuala ya anga na msimuliaji wa sayansi, García Soto anajaribu kuweka mazingira ya masuala ya anga yafahamike kwa hadhira ya aina yoyote. Mpango wake ni kujenga daraja linalounganisha na kuwashirikisha watu masuala ya uvumbuzi wa kisayansi, ikiwa ni pamoja na kumsha moyo wa udadisi na utafiti ambavyo, kimsingi, ndivyo vinavyohitajika kwenye sayansi.

Mi gran deseo para todos es que recuperemos el niño interno y nos sorprendamos con las maravillas de nuestros COSMOS.

 Shauku yangu kubwa kwetu sote ni kiwa tumgundue mtoto anayeishi ndani yetu na kushangaa maajabu ya ulimwengu tunaoishi

Podikasti hiyo inapatikana kwa lugha ya ki-Hispaniola kwenye iTunes [5] na Ivoox [6] (pamoja na toleo la Kiingereza [7]likipatikana pia). Inakwenda sambamba na Chaneli ya YouTube [8]maalum kwa ajili ya kutazama kwa ukaribu namna mbalimbali za kuchunguza na kudadisi maarifa ya anga za mbali. Posti ya video, “Namna gani ya kujifunza masuala ya nyota” ni mfano wa kumfuatilia García Soto anapozungumza na wanafunzi na watafiti wa masuala ya anga wanaojifunza masuala ya anga pekee. Si tu inatuweka karibu na sayansi yenyewe, lakini pia inaturuhusu kuishi maisha ya wale wanaoifanya sayansi.

Sehemu ya kile kinachofurahisha kuhusu video hizi ni namna zinavyofunua mambo ya anga yasiyofahamika, ikiifanya sayansi isionekane kama taaluma ya wenye akili sana isipokuwa kujitoa, juhudi na ushirikiano.

Mifano mingine, kama inavyopatikana kwenye Atacama Desert [9], inaweka kumbukumbu za utafiti na kutupa mbinu za kuchunguza anga kutokea Chile…na kuna dondoo kwa wale wanaopenda kutengeneza blogu za video [10]: