- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Jeshi la Nchini Thailand Lawaruhusu Watoto Kucheza na Bunduki halisi, Vifaru na Helikopta za Kijeshi

Mada za Habari: Asia Mashariki, Thailand, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vijana, Vita na Migogoro

Children's Day at the Chiang Mai Air Force base in Thailand. Photo from Wikimedia Commons [1] Maadhimisho ya Siku ya Watoto katika kambi ya Kijeshi ya Chiang Mai huko Thailand. Picha kutoka Wikimedia Commons[/caption

Siku ya watoto nchini Thailand ni sherehe ya kila mwaka ambapo shughuli mbalimbali huandaliwa kwa ajili ya kutoa hamasa kwa vizazi vijavyo. Hii ni siku ambayo watoto wanapewa fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali kama vile ya makumbusho, majengo ya serikali na hata kambi za kijeshi zilizosheheni silaha.
Ndiyo, ni ukweli mtupu, watoto wa Thailand wanapata fursa ya kucheza [2] na bunduki halisi za kivita, mitambo ya kurushia mabomu sambamba na kupakia kwenye vifaru pamoja na Helikopta za kivita.

Kwa watetezi wengi wa haki za binadamu, matukio kama haya ambayo kwa kiasi kikubwa yameshakuwa kama utamaduni kwa miongo kadhaa iliyopita, wanaona kuwa yanapelekea kuhamasisha machafuko katika jamii. Wakosoaji wa mamlaka iliyojitwalia [3] madaraka mwaka 2014, wanaona utamaduni huu kama tukio la kuwahadaa watu na kuhalalisha utawala wa kijeshi nchini, na pia, jeshi lenyewe haliweki juhudi kamili za kuondoa mtazamo huo.
Tangu mwaka 1930, jeshi limekuwa na zaidi ya majaribio kumi na mbili ya kupindua serikali nchini Thailand. the army has launched more than a dozen coup attempts in Thailand.

Taarifa katika chombo kimoja cha habari cha nchini Thailand, yenye jina “Hamasisha Furaha: Watoto wa Nchini Thailand, Wanatumia Vifaru, Ndege za kIvita, na Bunduki katika Siku ya Watoto”, mwanajeshi mmoja aliyekuwa pamoja watoto wa umri wa miaka mitano wakati wa maadnimisho ya siku ya watoto ya mwaka huu aliweka bayana [4] lengo la kutumia vifaa halisi vya kijeshi:

Tunachokifanya ni kuwafanya watoto walifahamu vyema jeshi pamoja na zana zinazotumiwa. Kwa uzoefu wanaoupata, wanajifunza kulipenda jeshi na hata kuwa wanajeshi hapo baadae.

Kwa upande wake, mwandishi wa habari [7] Andrew MacGregor Marshall, anaona kuwa Siku ya Watoto nchini Thailand kwa sasa imekuwa“siku iliyodhaminiwa na serikali ya unyanyasaji wa watoto.”

Lengo kubwa haswa la Siku ya Watoto ni kwamba, jeshi- ambalo halijawahi kupigana kwenye vita halisi dhidi ya maadui lakini mara kadhaa saa limekuwa likikandamiza uhuru nchini Thailand- kuwaalika watoto kwenye makambi ya kijeshi ambapo wanaweza kuhadaiwa na kukabidhiwa silaha ili wacheze nazo.

Mawazo yake yalisambazwa mtandaoni na wa tumiaji wa intaneti ambao hawakukubaliana na matumizi ya silaha katika kutoa elimu kwa watoto.

Tangu mwaka jana, jeshi limekuwa likitoa taarifa hatarishi za kampeni kadhaa zinazowalenga watoto zikiwemo za kubadili mitaala ya mashuleni ili kutilia mkazo Tunu za Thailand [16], kusajili polisi wa kuchunguza taarifa za mitandao ya intaneti pamoja na kuendesha mafunzo kwa watoto wa elimu ya awali.

Mwandishi John Draper anaeleza [17] kuwa mafunzo ya kijeshi kwa watoto wa elimu ya awali yanayofadhiliwa na serikali kuwa ni aina ya “mfumo rasmi wa kijeshi wa Kuwaaminisha watoto kuhusu taratibu za kijeshi.”

Kwa sasa, ni vigumu kufahamu ni lini haswa utamaduni huu wa kuwajengea imani za kijeshi watoto utasitishwa lini. dHow long that indoctrination will continue is impossible to guess. Ikiwa utawala wa kiraia utarejeshwa nchini Thailand, serikali mpya bado itaendeleza utaratibu wa kuwaruhusu watoto wadogo wacheze na bunduki nzito za kivita pamoja na vifaru?